Akizungumza na Bongo5 leo kwa njia ya simu Nay amesema amekuwa akivaa mlegezo kwa kipindi cha miaka ishirini hali ambayo itamwia vigumu kubadilika kutokana ni mtindo ambao ata mashabiki wake wengi wameuzoea.
“Nahisi kuna kitu kingine wanakitaka toka kwangu kuhusu muziki wangu ndiyo maana wananitishia kunifungia wakati mimi nafanya muziki kama ndiyo maisha yangu, kwahiyo kubadilika kwa haraka kuvaa mlegezo siwezi labda baada ya miaka 3 ila inategemea” Alisema Nay.
Aidha katika mahojiano mengine na kipindi cha Showtime kupitia kituo cha RFA ya Mwanza Nay amesema kuwa Baraza hilo lina majukumu mengi ya kufanya kwaajili ya kuboresha maslahi ya wasanii badala ya kuhangaika na kumzuia kuvaa mlege ili hali wanaovaa hivyo ni wengi.
“Sasa hata baraza la sanaa Tanzania wana shughuli nyingi sana za kufanya nyingi sana ili sanaa yetu isonge mbele mambo yetu yaani wasanii tuishi maisha mazuri lakini si swala la kufuatilia mlege wa Nay, hapana kuna kitu behind ambacho kinaendelea sijui ni nini maybe wameamua waanzie hapo ili wastopishe kile ambacho nakifanya.”
DEAR READER LEAVE A COMMENT BELOW
SHARE THIS POSTS TO YOUR FRIENDS BELOW==>>
DONT HESITATE TO JOIN OUR FACEBOOK PAGE BELOW FOR MORE BREAKING AND HOT RESEARCHED NEWS