Mtoto aliyefariki |
Mtoto Matrida Michael mwenye umri wa miaka 9, mkazi wa Mtoni kwa Azizi Ally, wilayani Temeke jijini Dar es Salaam, amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Oktoba 23, mwaka huu kufuatia majeraha ya moto aliyoyapata.Marehemu Matrida na watoto wenzake wawili, Tatu Mapunda (9) na Flora Mapunda (7), waliungua moto Oktoba 16, mwaka huu saa tano usiku wakiwa wamelala baada ya chumba chao kulipuliwa kwa petroli na mtu anayedaiwa kwa ni Brighton Mnamwa.
Inadaiwa kwamba chanzo cha Mnamwa kuamua kulipua watoto hao ni ugomvi baina yake na mkewe Janeth Lwena, waliyekuwa katika mzozo wa kumgombea mtoto wao wa miaka mitatu aitwaye Tulizo.
Watoto ambao wako hoi |
Mama mdogo wa marehemu Mary Ivo ambaye alikuwepo msibani hapo, alisema kwamba dada yake yupo Muhimbili anawauguza majeruhi wawili waliobakia na kwamba wakati wa ugomvi wao, mke alimzidia nguvu mumewe.
Aidha aliendelea kueleza kwamba baada ya mke kumzidi nguvu, mume alizusha ugomvi mkubwa huku akitishia kumuua kwa panga, hata hivyo mke alimdhibiti.
‘Baadaye mume huyo inadaiwa kwa aliondoka hapo nyumbani na haikujulikana alikoenda, ndipo mke alienda chumba cha jirani na kumuomba Matrida abakie na watoto pale chumbani akatoe taarifa polisi lakini mtoto aliyekua akigombewa alienda naye kituoni,’ alisema mama mdogo.
Habari zinasema kwamba yule mume alienda kituo cha mafuta kununua petroli ili aweze kuwatekezeza wote, lakini hakujua kama mkewe pamoja na mtoto aliyekua akigombewa hawakuwepo.
Taarifa zaidi zinaeleza kwamba baada ya mume huyo kurudi, alimimina mafuta hayo katika chumba hicho kisha kukilipua wakati watoto hao watatu wakiwa katika usingizi na wananchi walipojitokeza walikuta chumba kikiteketea huku sauti ya watoto ikisikika wakiomba msaada.
Wananchi waliokuwepo kwenye eneo la tukio walisema kwamba walipatwa na uchungu hivyo walijitosa kuuzima moto ule na kuwaokoa watoto hao watatu huku wakiwa wameungua vibaya, waliwakimbiza Hospitali ya Temeke na kutokana na hali yao kuwa mbaya walipelekwa Muhimbili ambapo Matrida alifariki dunia.
Naye Michael Melkiori Kess, baba wa marehemu alisema kwamba amesikitishwa na kitendo hicho na amedai ni cha kinyama hivyo ameiomba dola kumsaka mtu huyo hatari kwani huko aliko kwa sasa bado anaweza kusababisha majanga megine.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mtoni Sabasaba, Mwita Mang’ana alisema kwa kitendo hicho ni cha kinyama kwani amesababisha kujeruhi watoto wasiokua na hatia na amewataka wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kuhakikisha kuwa mtuhumiwa anapatikana .
Naye Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba msako wa kumtafuta mtuhumiwa unaendelea sambamba na uchunguzi wa tukio.
DEAR READER LEAVE A COMMENT BELOW
SHARE THIS POSTS TO YOUR FRIENDS BELOW==>>
DONT HESITATE TO JOIN OUR FACEBOOK PAGE BELOW FOR MORE BREAKING AND HOT RESEARCHED NEWS