Sunday, October 27, 2013

Kupiga ni adhabu stahili kwa mtoto?

                                                     

Adhabu ya viboko kwa mtoto imekuwa na mtazamo tofauti kwa baadhi ya watu. Wako ambao huona ni sahihi mtoto kuchapwa anapokosea, wapo wengine wanaoiunga mkono lakini kwa masharti, wapo pia wanaoamini njia nyingine ya adhabu na siyo viboko.
Binafsi nikiwa pia ni mzazi naweza kuona jambo moja. Kutokana na mazingira au mtindo wa maisha, wakati mwingine watoto wetu hufanya makosa yanayostahili kupata adhabu. Lakini je, unafahamu kuwa kwa kumchapa mtoto unaweza kupandikiza ugonjwa mwingine mkubwa zaidi ya kosa alilofanya? Miongoni mwa mambo yanayoweza kuzalishwa kutokana na tabia ya kuwachapa watoto ni usugu, ujeuri na hata visasi.
Unapomjengea mtoto mazoea ya kumchapa kila anapofanya kosa, na yeye hutengeneza mpango wa kupambana na fimbo zako, hivyo kuona kama sehemu ya maisha yake.
Pengine kwa akili ya kitoto inawezekana akaangalia kosa alilofanya kama ni jambo sahihi, hivyo kutengeneza mpango wa kulipa kisasi. Kwa mfano; Umemwadhibu mtoto kwa kosa la kumpiga mwenzake, hivyo kutokana na maumivu atakayosikia atakachofanya siyo kuacha kumpiga mwenzake bali ni kuweka kisasi na kumtafutia kitu kingine cha kumuumiza.
Wataalamu wa malezi ya watoto walikuja na njia mbadala ya kuwapa mwongozo watoto mara wanapofanya makosa mbalimbali.
Wataalamu hawa wanasisitiza kwamba, ikiwa njia hizi zitatumika kwa ufasaha watoto wetu watakuwa wasikivu. Badala ya kumpa vitisho mchagulie mtoto wako kitu cha kufanya.
Kwa mfano; Ikiwa mwanao amekosa wakati wa kula, unaweza kumwambia akae chini ale badala ya kula mezani na wenzake au badala ya kumwambi ukirudia tena huu ‘ujinga’ nitakuunguza mikono yako. Mwezeshe mwanao kujifunza kutokana na makosa yake
Ikiwa umemchapa mwanao kwa sababu anafanya kosa au jambo baya na akaacha, itakuwa tu ameacha kwa sababu ya hofu ya kuchapwa tena.
Wakati unapomfundisha mtoto athari ya kile alichokifanya itamjenga na kumfanya asirudie tena kwani atakuwa ameelewa zaidi.
Kwa mfano; Mtoto wako ameharibu mdoli wa mwenzake. Wewe kama mzazi ukachukua pesa ukalipa, kisha ukamchapa na kumwambia amwombe msamaha mwenzake. Atafanya hivyo kwa hofu tu na siyo ajabu akarudia tena kosa lile.
Lakini ikiwa utamshirikisha katika mashauri ya jinsi gani mnatakiwa kulipa kile alichoharibu na kumpa tafsiri yake, itasaidia kumpa uelewa kuwa alichofanya ni kosa.
Kwa mtindo huu atakuwa amejifunza kutokana na makosa yake.
TUPE MAONI YAKO....
src mwananchi

DEAR READER LEAVE A COMMENT BELOW

SHARE THIS POSTS TO YOUR FRIENDS BELOW==>>

DONT HESITATE TO JOIN OUR FACEBOOK PAGE BELOW FOR MORE BREAKING AND HOT RESEARCHED NEWS

0 comments em “Kupiga ni adhabu stahili kwa mtoto?”

Post a Comment

 

Mambomseto Copyright © 2011 -- Template created by MAMBOMSETO TEAM -- Powered by MAMBOMSETO

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter