Friday, October 25, 2013

VITUO VYA MWENGE NA UBUNGO KUHAMISHWA JIJINI DAR....!!

Vituo vya daladala vya Ubungo na Mwenge vinahamishwa kupisha Mradi wa Mabasi yaendayo Haraka Dar es Salaam (DART), ambao miundombinu yake inaendelea kujengwa.

Ofisa Habari wa Manispaa ya Kinondoni, Sebastian Mhowera amekaririwa akisema yafuatayo:-
  • Kituo cha Ubungo kitahamishiwa nyuma ya jengo la Mawasiliano lililopo Barabara ya Sam Nujoma.
  • Kituo cha Mwenge, kitatumika kwa ajili ya kushusha abiria pekee.
  • Magari ya Mwenge, yatakuwa na uamuzi wa ama kuishia kwenye stendi ya Makumbusho au kwenda hadi kituo hicho kitakachohudumia magari ya Ubungo (kilichoko Mawasiliano).
  • Wakati wowote kuanzia sasa vituo hivyo, vitabomolewa kupisha mradi huo.

Kuhusu hatua zinazochukuliwa na manispaa, kuwezesha wafanyabiashara ndogo kupata maeneo ya kuendesha shughuli zao alisema, hakutakuwa na mfanyabiashara atakayeruhusiwa kuuza bidhaa zozote katika kituo kipya, kama ilivyo sasa kwa vile hakutakuwa na nafasi kutokana na  eneo lote kutumika kwa ajili ya barabara.

Akasema kwa hali hiyo wafanyabiashara watalazimika kwenda katika maeneo waliyopangiwa: “ Kwa hiyo ni bora wakaanza kujiondosha wenyewe mapema kabla hatua ya kuondolewa na ujenzi kuwafikia,” alisema na kuongeza kuwa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya kazi hiyo yapo katika masoko mbalimbali likiwemo la Kijitonyama.

Habari leo

DEAR READER LEAVE A COMMENT BELOW

SHARE THIS POSTS TO YOUR FRIENDS BELOW==>>

DONT HESITATE TO JOIN OUR FACEBOOK PAGE BELOW FOR MORE BREAKING AND HOT RESEARCHED NEWS

0 comments em “VITUO VYA MWENGE NA UBUNGO KUHAMISHWA JIJINI DAR....!!”

Post a Comment

 

Mambomseto Copyright © 2011 -- Template created by MAMBOMSETO TEAM -- Powered by MAMBOMSETO

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter