Mtu mmoja amefariki na mwingine kujeruhiwa kwa kupigwa risasi na Askari polisi wilayani Lushoto mkoani Tanga baada ya askari huyo kudai kujeruhiwa na watu hao kwa kukatwa mapanga manne katika kichwa chake na mkono wa kushoto.
Kamanda wa polisi Mkoa wa Tanga Costantine Massawe amesema hili tukio limetokea saa nne na nusu jana usiku kwenye kijiji cha Shume tarafa ya Mlola ambapo askari huyu aitwae Oforo, amejeruhiwa alipokwenda na wenzake wawili kumkamata mtuhumiwa kutokana na kibali kilichotolewa na Mahakama wilayani humo kufuatia mgogoro wa ardhi.
Walipofika, walitokea watu wawili waliowashambulia askari kwa mapanga kitendo kilichofanya askari huyu kuwafyatulia risasi na kumuua mmoja wao ambae alifariki akifanyiwa matibabu kwenye hospitali ya Lushoto huku aliejeruhiwa akiendelea kupata matibabu.
DEAR READER LEAVE A COMMENT BELOW
SHARE THIS POSTS TO YOUR FRIENDS BELOW==>>
DONT HESITATE TO JOIN OUR FACEBOOK PAGE BELOW FOR MORE BREAKING AND HOT RESEARCHED NEWS