Showing posts with label MATUKIO. Show all posts
Showing posts with label MATUKIO. Show all posts

Friday, November 8, 2013

AKATWA NYETI KWENYE MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI...

MBALI na mtu mmoja kufariki dunia na wengine 24 kujeruhiwa na kulazwa kwenye Hospitali ya Bwagala, Turiani mkoani hapa, mwanaume mmoja amekatwa nyeti zake katika mapigano ya wakulima na wafugaji Jumanne iliyopita.
Mapigano hayo yaliyoshuhudiwa na mwandishi wetu yalipoteza amani iliyokuwa  kwenye Kijiji cha Dihombo Kata ya Hembeti Wilaya ya Mvomero.
Mashuhuda kadhaa walimwambia mwandishi wetu kwamba, mtu aliyekatwa  nyeti alikutana na wakulima hao wenye hasira waliokuwa wakimvamia mgeni yeyote waliyemuona  mbele yao.
“Wakulima walikuwa na silaha za jadi kama vile mapanga, mishale ya sumu na marungu, walimkuta mtu huyo aliyekuwa akipita na kumvamia kisha kumpiga na alipoanguka chini mkulima mmoja alimkata nyeti zake,” alisema shuhuda aliyejitambilisha kwa jina la Kibwana.
Mtu aliyekatwa nyeti (angalia picha ukurasa wa mbele) hakufahamika jina lake mara moja, lakini baadhi ya watu walioshuhudia tukio hilo walisema kwamba alikimbizwa hospitali ili kunusuru maisha yake.
Hata hivyo, baadhi ya wakulima nao waliumizwa vibaya katika tukio hilo lililosababisha kifo cha mfugaji Yusuf Mdutu.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile amethibitisha kutokea kwa mapigano hayo huku akisema kuwa msako mkali unaendelea kuwakamata wahusika.

HURUMA SANA ....MTOTO ANYOFOLEWA JICHO NA LINGINE LAANZA KULEGEA

MTOTO Khalidi Juma mwenye umri wa miaka minne, mkazi wa Vingunguti jijini Dar es Salaam, yuko katika mateso makali baada ya jicho lake moja kutolewa katika harakati za kumnusuru na ugonjwa wa Kansa, huku lingine nalo likilegea.
Mama wa mtoto huyo Hadija Kilindo.
Akizungumza  mama wa mtoto huyo Hadija Kilindo, alisema alimzaa mtoto huyo akiwa na afya njema, lakini alipofikisha umri wa miezi tisa ndipo alipogundua kitu cheupe kwenye mboni ya jicho lake.
Baada ya hali hiyo, alisema alimpeleka katika hospitali inayotibu watu wenye ulemavu mbalimbali ya CCBRT iliyopo Msasani jijini Dar, ambako baada ya kupimwa, aliambiwa mwanaye alikuwa na kansa.
Mtoto Khalidi Juma  jicho lake moja limetolewa katika harakati za kumnusuru na ugonjwa wa Kansa.
“Baada ya kuambiwa mtoto wangu ana ugonjwa wa kansa sikuwa na jinsi, nilikubali afanyiwe upasuaji kwa ajili ya kuliondoa jicho hilo ili kuokoa maisha yake,” alisema.
Mama huyo alisema ilipofika mwaka 2012, jicho lingine lilianza kumuuma huku likiwa linavimba, lakini alipompeleka katika Hospitali ya Muhimbili, aliambiwa kansa imeshaenea mpaka kwenye ubungo, hivyo arudi naye nyumbani kwani hawezi kuishi kwa muda mrefu.
“Kwa kweli nilivyoambiwa hivyo nilinyong’onyea mwili mzima nikawa sina jinsi kabisa na nikapoteza matumaini kabisa ya mwanangu kuendelea kuishi tena,”alisema.
Alisema alirudi nyumbani huku maumivu ya kijana wake yakiendelea na mwishoni, jicho lake likawa halioni tena. Kuhusu jicho lililotolewa, mama huyo alisema alikuwa akilitoa na kulirudisha kwa ajili ya kulisafisha, lakini hivi sasa hawezi kulitoa tena kwa vile kuna nyama zilizolishika na hivyo kumsababishia maumivu makali mno mwanaye hasa kichwani.
“Unavyotuona hapa usiku hatulali kabisa, mtoto ni kulia kwa maumivu, amefikia wakati hawezi kula vizuri na anatumia muda mwingi kulia,” alisema.
Mama huyo aliongeza kueleza kuwa kutokana na hali ya mwanaye, anakosa muda wa kufanya chochote cha kujiingizi kipato, hivyo kuwa katika wakati mgumu mno kimaisha, hasa kwa vile baba mzazi wa mtoto huyo alimkimbia tokea alivyoanza kuumwa.
“Mimi naamini kabisa labda nikipata msaada nikienda hata kwa wachina nitapata hata dawa ya kumpunguzia mtoto wangu maumivu anayoyapata kwa hivi sasa,” alisema.
Kwa ye yote ambaye ataguswa na habari hii na angepeta kutoa msaada wa aina yo yote, anaweza kuwasiliana na mama mzazi anayetumia simu nambari 0656 042017.

HIVI NDIVYO AJALI YA PIKIPIKI ILIVYOCHUKUA ROHO ZA WANACHUO WAWILI WA CBE DODOMA, SOMA NA TAZAMA PICHA HAPA...ZINATISAHA !!!

Na John Banda, Dodoma 
WANAFUNZI wawili wa chuo cha biashara  wamepoteza  CBE wamekufa papo hapo kwenye ajali baada ya kugonga tela la mizigo lililokwama barabarani baada ya kuhalibika.
Ajali hiyo ilitokea jana majira ya saa 1.00 usiku baada ya kugonga tela la lori la mizigo kwa nyuma wakati wanafunzi hao walipokuwa wakitokea kwenye mwaliko wa sherehe ya rafiki zao iliyofanyika katika kijiji cha ihumwa manispaa ya Dodoma.
Gazeti hili lilishuhudia msongamano mkubwa wa magari katika barabara hiyo iliyopo pembezoni mwa kambi ya jeshi ya Ihumwa kwa takribani saa zaidi ya tatu kabla ya polisi wa usalama barabarani kufika na kuongoza utaratibu wa kuondoka.
Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Dodoma Suzan Kaganda alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi wa wanafunzi hao wakati wakiendesha pikipiki hiyo  yenye namba za usajili T 420 CCN  waliokuwa wakukitokea barabara ya morogoro kuingia mjini.
Suzan aliwataja kuwa ni Ramadhan Lesso na Gerger Lwandala wanafunzi wa CBE  na kwamba uzembe wa Dereva wa lori hilo lenye namba za usajili T 477 ABM na huku Tela lake ni T 838 AAZ aliyeliacha barabrani zaidi ya wiki bala kuweka alama yoyote huku matengenezo ya barabara hiyo yakiendelea katik eneo hilo.
Aliongeza kuwa miili ya marehemu hao iliyokuwa imehalibika vibaya kutokana na kufumuka fuvu la kichwa cha aliyekua dereva wa pikipiki hiyo  na ubongo kusambaa katika eneo hilo imehifadhiwa katika hospital ya mkoa.

Kwa picha za ajali hiyo bofya soma zaidi 

lakini tunaomba radhi kwa picha hizo zinaleta usumbufu ukiziangalia
 Miili ya Marehemu Ramadhan Lesso na Gerge Lwandala inaonakana kabla ya kuondolewa katika kijiji cha Ihumwa barabara ya Morogoro Dodoma kabala ya kuondolewa na kuhifadhiwa katika chumba cha maiti hospital ya mkoa.
 Baadhi ya watu wakiisogeza miili ya Wanafunzi wa CBE Dodoma  walikufa kutokana na kuligonga tela la lori kwa nyuma kutokana na mwendo kasi huku lori hilo likiwa limetelekezwa zaidi ya wiki bila alama yoyote barabarani hapo.
 
 Baadhi ya asikari wa Jeshi la wananchi walionekana kujaribu kutoa msaada katika ajali hiyo iliyosababisha vifo vya wanafunzi wa chuo cha biashara CBE Dodoma.
 Asikari wa wasalama barabarani akisaidiana kupima upana wa barabara sehemu ilipotokea ajali hiyo ilihusisha pikipiki na lori la mizigo.

Thursday, November 7, 2013

HUZUNI..HABARI KAMILI KUHUSU MUME ALIYEMUUA MKEWE KIKATILI NA KUFICHA MWILI WAKE STOO .....!!

Marehemu Hamida Urembo
Ni kifo cha kusikikisha cha mwanamke huyo pichani Hamida Urembo na muhusika wa mauaji hayo ni mumewe wa ndoa waliyeishi kwa miaka mitatu.Hamida alikuwa mwanafunzi wa chuo kikuu na mwaka watatu na alikuwa anatarajia kugraduate mwezi huu chuoni hapo.


Hamida na mumewe yahaya walibahatika kupata mtoto wa kike mwenye miaka mitatu sasa.Kwa mujibu wa dada wa Hamida ndoa yao ilikuwa ya misuko suko sana.Mume alikuwa sio mwaminifu mara nyingi alikuwa akizini nje.Ukiacha hilo alikuwa akimpiga sana mkewe mpaka kumzimisha.


Matatizo ambayo ndugu walikuwa wakiyajua na walishasuluhisha mara nyingi na Hamida kurudi kwa mume kuendelea na maisha.Hii ya mwisho ndio ilikuwa kubwa zaidi.Mume alikuwa akimtongoza housegirl hapo nyumbani na alipokuwa kesho housegirl akamfahamisha mama.


Akamueleza jinsi gani muwewe amekuwa akimsumbua kumtaka kimapenzi.Hamida akamwambia anataka tu uthibitisho kama ni kweli.Siku ya siku Yahaya akamlazimisha Hamida kwenda kwao na Hamida akakubali akijua kuna jambo.Akasindikizana na mumewe mpaka kituoni mume akijua mkewe hayupo kumbe mke aligeuzia njiani akarudi nyumbani akajificha chini ya uvungu chumbani kwa housegirl wake.Baadae mume akawasilia na housegirl kuwa anarudi nyumbani,aliporudi akaendelea kuomba mambo tena akavua nguo kabisa akabaki na boxer.Wakati huo yupo chumbani kwao na mkewe.Housegirl akamwambia wahamie chumbani kwako hapo sio salama.Basi wakahamia chumbani na akawa ndio anamuinamisha dada ili amfanye Hamida akatoka chini ya uvungu ili kumuokoa dada na kumuonyesha mumewe kuwa alikuwepo na amejua usaliti wake.Na alipokuwa chini ya uvungu alikuwa akirekodi kila kitu kwenye simu na alipotoka na picha akapiga.
Huyu ndiye Yahaya  aliyekuwa mume wa marehemu Hamida 
Hamida alitoka hapo akashitaki kwao na kwao wakamwambia aende kwa mjomba wa mumewe kumueleza matatizo ya mtoto wao. Alipofika kwa mjomba akaambiwa wanaume ndivyo walivyo avumilie tu arudi kwa mumewe.


Hamida akarudii kwao akiwa hana hana raha lakini uamuzi aliouchukua ni kuachana na mumewe kwani alikuwa kashachoka. Wakawa wakivutana sana mume akimsihi arudi nyumbani walikokuwa wakiishi Mbagala ila Hamida hakuridhia.


Hamida alishaenda mpaka Bakwata ili mumewe aamriwe kutoa talaka.


Mwisho wa Hamida kuonekana nyumbani ni siku ambayo yeye na ndugu zake walikuwa waende kijijini kwao kwenye viwanja walivyopewa na babu yao.Ila siku hiyo Hamida alitoa udhuru kuwa haendi na akamtaarifu mama yake kuwa Yahaya kamuita akachukue vitu vyake vilivyobakia.Mama akamkatalia kwenda akamwambia kuna kaka zake wakubwa aache wataenda kuvifata kwani huyo mume ni mshenzi anaweza kumfanyia kitu kibaya.Hamida akamwambia mama anataka kwenda mwenyewe kwani kuna vyeti vyake muhimu akavichukue.


Basi mama akamuacha aende kishingo upande lakini mama akamwambia basi nenda hata na mdogo wako.Akaenda na mdogo wake lakini kufika kule mume akamkatalia mdogo mtu kuingia ndani.


Wakabishana sana kwa nini asiingie mdogo mtu kuepusha shari akaenda kukaa kwa jirani asubiri kuitwa. Akakaa na muda kupita kukawa kimya akajua wale wameelewana ndio maana hakuna makelele hivyo akaendelea kusubiri.


Akakaa weee mpaka jioni giza lilipoanza kuingia kidogo Yahaya akampigia simu kwa kutumia simu ya Hamida akimwambia aondoke tu arudi nyumbani wao wameshaondoka na vyombo wamebeba.


Mdogo mtu akaondoka kurudi nyumbani kwao Tabata akijua mke na mume wameelewana kumbe dada yake ameshakufa ndani.


Mdogo mtu akafika nyumbani saa mbili usiku na kumwambia mama jinsi Hamida alivyomuudhi kamuacha yeye kwa jirani na akaondoka na mumewe Yahaya.Mama machale yakamcheza akanyanyua simu akampigia Yahaya kumuuliza mwane yupo wapi.Yahaya akamjibu kuwa ameachana nae kitambo mama akamwambia sio kweli mwanangu hawezi kuchelewa kurudi nyumbani na hana kawaida hiyo.Yahaya akamjibu atarudi tu Hamida mtu mzima.


Mamam tayari alishajua kuna jambo akampigia simu baba Hamida aliyekuwa Arusha kumtaarifu kilichotokea. Baba Hamida akampigia Yahaya lakini hakupokea simu.Wasiwasi ukazidi kutanda na ndugu kupeana taarifa zaidi.Asubuhi kulipokucha wakaenda Mbagala kwa Yahaya lakini wakatoa taarifa polisi.Polisi wakawaondoa wasiwasi kwamba hao wanajuana wenyewe labda wameamua kukumbushiana.


Ndugu hawakuridhika wakaenda kwa mjumbe awaruhusu wavunje nyumba waingie ndani pengine kamfungia ndani maana ilikuwa kawaida yake kufanya hivyo kumfungia Hamida ndani.Basi mjumbe akaruhusu mlango uvunjwe walipoingia ndani palikuwa patupu hawakuona kitu wala dalili za mauaji.Kuna chumba ambacho ni stoo hicho walishindwa kufungua na mjumbe akawaambia hiyo ni stoo wanawekaga mavitu yamejazana humo basi wakakiacha wakaondoka.


Hawakuishia hapo bado waliendelea kumsaka Hamida bila mafanikio.


Hamida alipotea toka jumapili iliyopita,jumanne juzi kila mtu wakapanga kila mtu akamtafute popote pale anapoona anaweza kumpata.Mama akaenda kwenye maombi kanisani wakati muislam,dada akaenda blue pearl kazini kwa Yahaya na huku majirani Mbagala wakaanza kuona inzi na harufu kali ikitoka nyumbani kwa Yahaya.Ikabidi mjumbe apige simu kwa mama Hamida kumueleza kinachoendelea polisi wakaitwa,nyumba ikavunjwa ili kutafuta harufu inatokea wapi.Wakavunja kile chumba cha stoo na kukuta mwili wa Hamida umeshaanza kuharibika.Kanyongwa na kamba ya katani na kitenge kafungwa puani na mdomoni.Mwili wake ukawekwa kwenye mfuko akajaziwa mito na manguo nguo na tendegu la kitanda kawekewa shingoni.


Ndugu, polisi wakachukuwa mwili kwa ajili ya msiba na mazishi wakati huo Yahaya alishakimbia siku nyingi hajulikani alipo.


Hamida alizikwa jana kule kwa babu yake Mzenga uzaramuni walipokuwa waende  kwenye mashamba waliyopewa. Msiba upo nyumbani kwao Tabata. Mrehemu ameacha mtoto wa kike wa miaka mitatu anaitwa Tayana.


Habari hii inaendelea tena kesho katika heka heka za leo ndani ya leo tena ya clouds fm.

Na kwa sasa kama nilivyo report hapo mapema leo kwamba mthumia Yahaya anatafutwa na police kwa kosa la mauwaji ya mkewe Hamida.

R.I.P Hamida na tunatoa pole kwa familia nzima ya Urembo kwa msiba

Wednesday, November 6, 2013

PICHA: AZIKWA AKIWA HAI KWA TUHUMA ZA KUMUUA MWANAE WA KUMZAA KISHIRIKINA MBEYA....

HILI NI KABURI LA MZEE ALIYEZIKWA AKIWA HAI KABURI HILI LITAFUKULIWA KESHO NA POLISI
MOJA YA NDUGU WA MZEE ALIYEZIKWA AKIWA HAI AKIELEZEA KWA KIFUPI JINSI NDUGU YAKE ALIVYOZIKWA AKIWA HAI HABARI KAMILI TUTAWALETEA KESHO MARA BAADA YA KUFUKULIWA MWILI HUO
HILI NI KABURI LA MTOTO WA MZEE ALIYEZIKWA HAI AMBAYE INASEMEKANA BABA YAKE ALIMUUA KIUCHAWI

PICHA: MWIZI WA PIKIPIKI AFUNGIWA KWENYE BODABODA NA KUBURUZWA UMBALI WA KILOMITA MOJA KISHA KUCHOMWA MOTO...

Wananchi wakishuhudia  mwili wa mtu aliyetuhumiwa kuiba pikipiki ukiteketea kwa moto

Polisi wakiondoka na mwili wa marehemu
MTU mmoja asiyefahamika jina wala makazi yake, amepoteza maisha baada ya kupigwa na kuchomwa moto na wananchi ambao wameamua kujichukulia sheria mkononi.
Wananchi hao ambao ni wakazi wa eneo la Mtakuja Mbalizi, walifanya tukio hilo jana majira ya saa mbili asubuhi.
Mwenyekiti wa Kijiji cha Mtakuja Mbalizi Mbeya vijijini, Ambonisye Masinga, alisema kuwa  marehemu huyo alidaiwa kuiba pikipiki  eneo la Utengule.
 
Alisema, baadhi ya madereva wa bodaboda(pikipiki) walianzisha msako na kufanikiwa kumtia nguvuni marehemu huyo na kuanza kumshushia kipigo huku mwili wake ukiwa umefungwa kwenye pikipiki na kuuburuza barabarani umbali wa kilomita moja.
Alisema, mwili huo uliburuzwa na kufikishwa kwenye eneo la mlima reli maarufu kwa jina la eneo la adhabu kwa wahalifu  na kuchoma moto mwili wake.
 
Aidha, katika tukio hilo fundi ujenzi aliyekuwa katika eneo hilo Asangalwisye Mayasu(50) mkazi wa kivukoni, alijikuta akiambulia kipigo baada ya kujaribu kuwazuia wananchi ambao waliamua kujichukulia sheria mkononi.
 
“Baada ya msamalia huyu kupigwa na kuumizwa vibaya serikali ya kijiji ilimkimbiza hospitali Teule ya ifisi na kwamba hali ya afya yake si nzuri hali iliyopelekea mke wake aitwaye Kristina Kyando (45) Kuzirai,”alisema
Hata hivyo Kamanda wa Polisi mkoa wa Mbeya, Diwani Athumani, alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba jeshi la polisi litahakikisha linawatia mbaroni watu wote waliohusika na mauaji hayo.
 
Kumeibuka kwa vitendo vya madereva  pikipiki kujichukulia sheria mkononi ambapo hivi karibuni walifunga barabara ya Iwambi Jijini Mbeya kwa kulishinikiza jeshi la polisi kuwaachia watuhumiwa wawili ambao  walituhumiwa kuiba pikipiki ili wawaue.

UKATILI! MFANYAKAZI WA TBC APIGWA RISASI MAENEO YA UBUNGO NA KUFARIKI HAPO HAPO JANA JIONI....


Ni simanzi kubwa tena na mfululizo wa matukio ya ujambazi nchini. Jana jioni Ramadhani Gize mfanyakazi wa TBC alipigwa risasi na watu wanaosadikika ni majambazi akiwa kazini na kukutwa na mauti hapo hapo. Majambazi hao wanasadikika walikuwa wanne walipovamia katika maeneo ya Ubungo Maziwa.
Poleni wafanyakazi wa TBC kwa msiba huu na familia ya marehemu.

Chanzo Tbc News

Monday, November 4, 2013

Mwanamke amwagiwa maji ya moto mwili mzima....Kosa lake ni kumlilia mama yake ambaye ni mgonjwa



Msichana mmoja, Mariam Chacha, mkazi wa Mtaa wa Nyasho A, mjini Musoma  amemwagiwa maji ya moto na kuunguzwa mwili, hali iliyofanywa alazwe katika hospitali ya mkoa. 
 
Tukio hilo la kusikitisha lilitokea Oktoba 22 mwaka huu saa mbili usiku ambapo inadaiwa aliyefanya kitendo hicho ni Pendo Wambura ambaye amekamatwa na polisi.
 
Habari kutoka ndani ya kituo cha polisi mjini hapa zinadai kuwa mara baada ya Mariam kumwagiwa maji ya moto na mwenzake na kuungua sehemu za kitovu mpaka usoni, matiti na mikono na akiwa hajitambui mpaka sasa,wasamaria wema walimpeleka polisi ili kupata hati ya matibabu (PF 3) na akaenda kutibiwa katika Hospitali ya Serikali ya Musoma alikolazwa wodi namba nne.
 
“Polisi tulikwenda kumkamata mtuhumiwa na tunamshikilia kwa kuwa majeruhi hali yake ni mbaya, kalazwa, na tayari amefunguliwa jalada namba MUS/IR/5009/013,” alisema afisa mmoja wa polisi kwa sharti la kutoandikwa jina lake  kwa kuwa siyo msemaji.
 
Shuhuda mmoja alimwambia  mwandishi  wetu kwamba Mariam alikwenda kuwasalimia ndugu zake pamoja na mama yake ambaye ni mgonjwa wanaokaa nyumba moja na mtuhumiwa.
 
“Mariam alipoona hali ya mama yake alianza kulia ndipo Pendo alipokwenda kuchukua maji yaliyokuwa yakichemka ili yapikiwe ugali wa mama mwenye nyumba na akamwagia mwenzake akidai eti anachukizwa na kitendo chake cha kumlilia mgonjwa wake,” kilisema chanzo.
-GPL

Sunday, November 3, 2013

HURUMA!!Mwanafunzi ajinyonga kukwepa mtihani wa kidato cha nne huko Iringa


Mwanafunzi aliyekuwa akisoma  shule  ya  sekondari  Sabasaba  mjini  Iringa akijiandaa kurudia  kufanya  mtihani  wa  taifa  wa kidato  cha nne kupitia  kituo  cha Krelluu mjini  Iringa Khamis Mkundo  mkazi  wa Mwangata  C katika manispaa ya  Iringa amejiua kwa kujinyonga  kwa kamba kwa kile  alichodai  kuchoshwa na kufeli  mara kwa mara mtihani wa kidato cha nne.

Katika  barua  yake  ndefu aliyoiandika  kijana  huyo amesema  kuwa amefanya  hivyo si kwa kujipendea  ila amechukizwa na hatua yake ya  kufeli mara kwa mara  hivyo  kuamua  kujiua ili  kuepuka aibu katika mtihani ujao ambao anaamini angefeli.

Shemeji  wa  kijana  huyo Aden Tagalile ameueleza mtandao  matukiodaima.com  kuwa  tukio  hilo limetokea mida ya saa 12 na saa 1  usiku wa  leo baada ya kuwepo kwa mazungumzo ya muda  mrefu  kwa kijana  huyo kuonyesha kuchukia hatua yake ya kuendelea kuristi  mtihani  wa kidato cha nne  bila mafanikio.

Kijana huyo  alisema hajapenda  kuona anaendelea  kufeli na kuwa  yupo tayari kwa lolote  kukwepa aibu ambayo ipo mbele  yake.
 
Hata  hivyo kufuatia mazungumzo hayo, kijana huyo aliagana na ndugu zake akiwemo kaka  yake anayeishi nae kwa kila mmoja kuondoka nyumbani  hapo kabla  ya kijana  huyo kukutwa amejinyonga.

Mwenyekiti  wa serikali  ya mtaa huo Sarehe Mgimwa amethibitisha  kutokea kwa kifo  hicho na kuonyesha ujumbe ambao kijana  huyo ameuacha .

 
 
 
-Matukiodaima .com

Friday, November 1, 2013

MWANAMKE ANUSURIKA KUUAWA BAADA YA KUKUTWA UCHI HUKU AKIWA AMESHIKA KOPO LENYE MAVI NA DAWA HUKO BUNDA...

(Picha  ya  Maktaba.)

JESHI la Polisi wilayani Bunda, jana lililazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi wenye hasira kali waliotaka kumuua mwanamke mmoja mkazi wa mtaa wa Cha Nyerere katika mamalaka ya mji mdogo wa Bunda.
 
Mwenyekiti wa mtaa huo, Maxmilian Bwire, alisema kuwa tukio hilo lilitokea saa 10 usiku nyumbani kwa mwanamke huyo, Sarafina Nyamboko, maarufu kama mama Nyamboko.

Alisema kuwa siku ya tukio mama huyo alikutwa na mpangaji wake, Robert Msilimu, akiwa uchi wa mnyama na kopo tupu la amboni lita tano, lililodaiwa kuwa na dawa ambayo alikuwa ameimwaga katika kila mlango wa wapangaji wake.
 
“Baada ya kumhoji alisema alikuwa anawamwagia dawa ya baraka wapangaji wake kwani kila tarehe moja huwa anafanya hivyo ili waweze kupata baraka kwa Mwenyezi Mungu.
 
“Dawa hiyo inaonekana ilikuwa imechanganyikana na kinyesi maana mji mzima ulikuwa unanuka kinyesi,” alisema mpangaji huyo ambaye alimkuta mwenyenyumba wake akifanya mchezo huo.
 
Alifafanua kuwa kitendo hicho kilimshtua sana ndipo alipowaamsha wapangaji wenzake ambao waliamua kupiga yowe na majirani walifika na silaha mbalimbali za jadi na kuanza kumshambulia.
 
Alisema kwa kushirikiana na mwenyekiti wa mtaa huo, walipiga simu polisi ambao walikuja na baada ya kukuta hali ni mbaya, waliamua kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi hao na kumchukua mama huyo kwenda naye kituo cha polisi.
 
Hata hivyo, baadhi ya majirani walidai kuwa hii ni mara ya tatu sasa kwa mama huyo kukutwa anafanya mchezo huo na kwamba hata kwenye mikutano ya hadhara ya mtaa huo, ameshaonywa mara kwa mara lakini alikuwa hajaacha.
 
Polisi walisema kuwa wanaendelea kumhoji kwa kina kuhusu kitendo hicho cha kukutwa uchi na pia kufahamu ukweli wa dawa hiyo aliyokutwa nayo.
 
Kama ikithibitika kuwa kuna kosa ndani yake watamfikisha kwenye mkondo wa sheria.

Wednesday, October 30, 2013

INASIKITISHA: MTOTO WA MIAKA MINNE AKUTWA AMEFARIKI NDANI YA SHIMO LA CHOO CHA JIRANI MKOANI MBEYA....

Mwili wa Marehemu Joshua Isaac, 4,  mara baada ya kutolewa kwenye shimo la choo cha jirani alikotumbukia  na kufikwa umati.
 Habari zinasema kwamba juzi marehemu alikuwa anacheza na wenzake kisha akatoweka. 
Wadau mbali mbali wakishuhudia jana hilo

PICHA 6 ZA FUJO ZILIZOFANYWA NA MASHABIKI WA MBEYA CITY MARA BAADA KUPATA USHINDI WA 2-0 DHIDI YA PRISONS HAPO JANA..!!


Taarifa kutoka 87.8 Mbeya zinaamplfy kwamba mashabiki wa Mbeya City wamelishambulia gari la wachezaji wa Prisons na kumuumiza mchezaji mmoja ambapo pia walivunja vioo vya  gari aina Toyota Coaster na magari mengine yaliyokuwa kwenye msafara wa timu hiyo ikitoka uwanjani baada ya kufungwa na Mbeya City kwa mabao 2-0.

mbeyayetu.blogspot.com wameripoti kwamba Mashabiki hao walilishambulia magari hayo na kuyavunja vioo na baada ya hapo wakakimbilia kusikojulikana.

Mmoja wa maofisa wa Prisons alisema ana uhakika kuwa waliofanya hivyo ni mashabiki wa Mbeya City kwa kuwa walikuwa wamevaa jezi za rangi ya zambarau ambayo huvaliwa na timu hiyo.






Hapa chini ni baadhi ya fans Mbeya City wakiwa wamebeba jenela la timu ya Prisons, chini ya hii picha ni baadhi ya picha wakishangilia magoli uwanjani

UKATILI! MTOTO WA MIAKA 8 ALAZIMISHWA KUWA HAUSIGELI,MWAJIRI WAKE AMCHANJA NA KISU....


UKATILI! Katika hali ya kusikitisha, mtoto mwenye umri wa miaka 8 aliyejitambulisha kwa jina la Loveness na mwenzake aitwaye Anna, wanadaiwa kulazimishwa kufanya kazi za ndani huku wakipata vipigo vikali kutoka kwa waajiri wao.

Loveness alikuwa akifanyishwa kazi Ubungo-Maziwa na Anna alikuwa Kimara jijini Dar.
Watoto hao wameeleza kazi nzito wanazofanyishwa katika mazingira magumu wakiwa na umri mdogo, wanaohitaji kwenda shule.
“Mama (mwajiri wake) alikuwa akinipiga na wakati mwingine kunichanja na kisu,” alisema Loveness.


Majirani ambao hawakupendezwa na matukio hayo, waliitonya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ili kufuatilia suala hilo.
Jirani mmoja ambaye hakutaka kutajwa gazetini, alidai kwamba alikuwa akiumizwa na mwajiri wa Anna ambaye alikuwa akimpa vipigo vikali mtoto huyo ambaye alikuwa akimlea mtoto wa mama huyo kila siku.

“Hakuna kitu kilichokuwa kikituumiza majirani kama mtoto Anna ambaye alikuwa akipata vipigo vikali kila siku iendayo kwa Mungu kutoka kwa mwajiri wake, heri arudi kwao,” alisema.


Mtangazaji wa kipindi cha Wanawake Live kinachotetea haki za watoto na wanawake kupitia EATV, Joyce Kiria alitinga nyumbani kwa waajiri hao na kumkamata mmoja wao kisha  kumpeleka katika Kituo cha Polisi cha Kimara, Dar kwa ajili ya kujibu mashitaka ya kukaa na mtoto mdogo kama mfanyakazi.

Hata hivyo, mtangazaji huyo aliamua kuwachukua watoto hao na kwenda kuishi nao nyumbani kwake Changanyikeni, Dar, kwa ajili ya kufanya utaratibu wa kuwasafirisha vijijini kwao ambapo Loveness anatokea Morogoro na Anna ametokea Singida.
Joyce amekuwa akifanya mawasiliano na familia za watoto hao ili kuwarejesha kwao huku Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka wakiombwa kuangalia suala hilo la unyanyasaji kwa watoto kwa umakini mkubwa.

Hii ni video ya yule mganga aliyekamatwa na kiganja cha binadamu kikivuja damu huko Mwanza..!!


Watu watatu wakiwemo waganga wawili wa jadi wamekamatwa na polisi katika eneo la Igombe Tx, jijini Mwanza wakiwa na kiganja cha mkono wa kulia unaoaminika kuwa wa 

 binadamu.
 




Kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Mwanza, kamishna msaidizi wa polisi Joseph Konyo amesema tukio hilo limetokea eneo la kati ya ziwani na nyuma ya uwanja wa ndege wa Mwanza baada ya raia wema kuwapa taarifa za siri.

Tuesday, October 29, 2013

Mganga akutwa na kiganja cha binadamu akimuuzia mteja wake kwa milioni 100 huko Mwanza..


Mtu mmoja jijini Mwanza anadaiwa kukamatwa na kiganja cha mtu akiwa anajiandaa kumuuzia mteja kwa sh million 100.

Washukiwa walikamatwa  jana  karibia na uwanja wa ndege wa Mwanza  wakifanya  biashara  hiyo  haramu....
 Baada  ya  upekuzi  wa  kina, mteja  alikuwa  ana  milioni  100  na mganga alikutwa  na   kiganja cha  binadamu  ambacho kilikuwa  kibichi kikitoa damu.
Kiganja  hicho  kilikuwa  kimevishwa  tunguri  na nywele za binadamu.

Sunday, October 27, 2013

UKIATILI! BABA NA MAMA WAGOMBEA MTOTO,BAADA YA BABA KUZIDIWA NGUVU NA MKEWE ALIPUA WATOTO KWA PETROLI...


 Mtoto aliyefariki

Mtoto Matrida Michael mwenye umri wa miaka 9, mkazi wa Mtoni kwa Azizi Ally, wilayani Temeke jijini  Dar es Salaam, amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili Oktoba 23, mwaka huu kufuatia majeraha ya moto aliyoyapata.Marehemu Matrida na watoto wenzake wawili, Tatu Mapunda (9) na Flora Mapunda (7), waliungua moto Oktoba 16, mwaka huu saa tano usiku wakiwa wamelala baada ya chumba chao kulipuliwa kwa petroli na mtu anayedaiwa kwa ni Brighton Mnamwa.
Inadaiwa kwamba chanzo cha Mnamwa kuamua kulipua watoto hao ni ugomvi baina yake na mkewe Janeth Lwena, waliyekuwa katika mzozo wa kumgombea mtoto wao wa miaka mitatu aitwaye Tulizo.


Watoto ambao wako hoi

Mama mdogo wa marehemu Mary Ivo ambaye alikuwepo msibani hapo, alisema kwamba dada yake yupo Muhimbili anawauguza majeruhi wawili waliobakia na kwamba wakati wa ugomvi wao, mke alimzidia nguvu mumewe.
Aidha aliendelea kueleza kwamba baada ya mke kumzidi nguvu, mume alizusha ugomvi mkubwa huku akitishia kumuua kwa panga, hata hivyo mke alimdhibiti.
‘Baadaye mume huyo inadaiwa kwa aliondoka hapo nyumbani na haikujulikana alikoenda, ndipo mke alienda chumba cha jirani na kumuomba Matrida abakie na watoto pale chumbani akatoe taarifa polisi lakini mtoto aliyekua akigombewa alienda naye kituoni,’ alisema mama mdogo.
Habari zinasema kwamba yule mume alienda kituo cha mafuta kununua petroli ili aweze kuwatekezeza wote, lakini hakujua kama mkewe pamoja na mtoto aliyekua akigombewa hawakuwepo.
Taarifa zaidi zinaeleza kwamba baada ya mume huyo kurudi, alimimina mafuta hayo katika chumba hicho kisha kukilipua wakati watoto hao watatu wakiwa katika usingizi na wananchi walipojitokeza walikuta chumba kikiteketea huku sauti ya watoto ikisikika wakiomba msaada.

Wananchi waliokuwepo kwenye eneo la tukio walisema kwamba walipatwa na uchungu hivyo walijitosa kuuzima moto ule na kuwaokoa watoto hao watatu huku wakiwa wameungua vibaya, waliwakimbiza Hospitali ya Temeke na kutokana na hali yao kuwa mbaya walipelekwa Muhimbili ambapo Matrida alifariki dunia.
Naye Michael Melkiori Kess, baba wa marehemu alisema kwamba amesikitishwa na kitendo hicho na amedai ni cha kinyama hivyo ameiomba dola kumsaka mtu huyo hatari kwani huko aliko kwa sasa bado anaweza kusababisha majanga megine.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mtoni Sabasaba, Mwita Mang’ana alisema kwa kitendo hicho ni cha kinyama kwani amesababisha kujeruhi watoto wasiokua na hatia na amewataka wananchi kushirikiana na jeshi la polisi kuhakikisha kuwa mtuhumiwa anapatikana .

Naye Kamanda wa Polisi mkoa wa Temeke, Engelbert Kiondo alithibitisha kutokea kwa tukio hilo na kusema kwamba msako wa kumtafuta mtuhumiwa unaendelea sambamba na uchunguzi wa tukio.

MAZISHI YA NYAISANGAH YATUMIA MAJENEZA MAWILI...




NI vigumu kutokea! Lakini safari hii imetokea, mwili wa aliyekuwa mtangazaji wa Abood TV, Julius Nyaisangah ‘Anko J’ ambaye alifariki dunia Jumapili iliyopita mjini Morogoro, ulisafirishwa kwa majeneza mawili.
Usiku wa Jumatatu iliyopita kamera za Risasi Jumamosi, zilishuhudia jeneza lenye rangi nyeupe likiwa limetumika kuusafirisha mwili wa marehemu huyo kutoka Morogoro hadi Hospitali ya Taifa, Muhimbili jijini Dar.
Jumanne iliyopita, saa tatu asubuhi kamera zetu zilishuhudia jeneza lenye rangi ya kahawia (brown) likitumika kuusafirisha mwili huo kutoka Muhimbili hadi Viwanja vya Leaders, Kinondoni, Dar ambako marehemu aliagwa.
Baadhi ya watu walipoulizwa na Risasi Jumamosi wana mawazo gani kuhusu mwili wa marehemu kusafirishwa na majeneza mawili walionekana kushangazwa na tukio hilo.
Mwili wa marehemu ulisafirishwa siku hiyohiyo kwenda Bunda, mkoani Mara alikozaliwa kwa mazishi yaliyofanyika Alhamisi iliyopita.

Risasi Jumamosi lilimtafuta mjumbe mmoja wa kamati ya mazishi ya Anko J aliyeomba kusitiriwa jina lake na kumuuliza kulikoni majeneza mawili yatumike kusafirisha mwili mmoja ambapo alijibu:
“Lile lililotoka na mwili Morogoro lilionekana kukosa ubora halafu lilitengenezwa ‘chapchap’ ndiyo ikaamriwa linunuliwe jingine zuri zaidi.”
Risasi Jumamosi: Sasa lile jeupe lililotoka Morogoro limepelekwa wapi?
Mjumbe: Mh! lile tuliliacha muhimbili ,ndugu watajua cha kufanya.
Kwa Waislam, jeneza linalotumika kubebea mwili wa marehemu ni la wazi na hurudishwa msikitini baada ya mwili kuzikwa kaburini.
Kama mwili utasafirishwa hutumika jeneza la sanduku lakini haliendi kuingia kaburini na huvunjwavunjwa punde mwili unapofika.
Kwa Wakristo, jeneza linalotumika kubebea mwili wa marehemu hutengenezwa kama sanduku na huingizwa kaburini na marehemu akiwemo ndani.
Awali ilidaiwa kuwa, mwili wa marehemu ungesafirishwa kwa ndege kwenda tarime na gharama za usafirishaji zingesimamiwa na wizara ya habari vijana utamaduni na michezo, lakini juzi naibu waziri wa wizara hiyo, Amos makalla alikanusha wizara yake kutoa tamko hilo.

“Wizara haikutoa tamko hilo, wala hatukuwa kwenye kamati ya mazishi  ila tulituma mwakilishi,” alisema Waziri  makalla.


GPL

Thursday, October 24, 2013

SAKATA LA MTOTO ALIYEBAKWA NA BABA YAKE KWA MIEZI 9... MAMA MZAZI ASIMULIA MAZITO..!!

WIKI kadhaa zimepita tangu binti wa miaka 15 (jina tunalihifadhi) mkazi wa Kimara jijini Dar kupasua jipu la kubakwa na baba yake mzazi aliyefahamika kwa jina laMOHAMEDkwa miezi tisa, mama mzazi wa mtoto huyo amejitokeza na kusimulia mambo mazito zaidi.
Akizungumza na Ijumaa, mama huyo aitwaye Nusura amesema alipata habari za mwanaye kutendewa unyama wa kuingiliwa na mwanaume aliyezaa naye kupitia vyombo vya habari na kufunga safari kutoka Kigamboni jijini Dar hadi Kimara kwa viongozi wa serikali ya mtaa anakoishi mtoto wake huyo.
MSIKIE MAMA HUYO
Mwanamke huyo alisema alikutana na Mohamed (baba wa mtoto huyo) na kupendana naye hadi kufikia mwanaume huyo kwenda kujitambulisha nyumbani kwa wazazi wake.
“Lakini siku chache kabla hajatimiza lengo hilo la kuleta barua ya posa nilijigundua kuwa na ujauzito wa mwezi mmoja,” alisema.
Mama huyo anasema wakati wa ujauzito huo, mwanaume huyo alianza kumbadilikia na kutaka kumtumia kinyume na maumbile jambo ambalo alilikataa na kwenda kumweleza mama yake ambaye alimshauri kuachana naye.
Baada ya kukubaliana na ushauri aliopewa na mama yake mzazi, uhusiano wa wawili hao ukavunjika na miezi tisa baadaye akazaliwa binti aliyefanyiwa unyama.
Mtoto huyo alipozaliwa alikuwa chini ya uangalizi wa mama yake na bibi yake bila mzazi wa kiume kutoa matumizi yoyote kwa ajili ya mtoto.
KUMBE ALIMUIBA?
Kwa mujibu wa mama huyo, baba alimwiba mtoto huyo alipokuwa na umri wa miaka mitano na kumpeleka Manzese, Dar ambapo mama yake huyo alimfuatilia lakini baba huyo alikataa katakata kumwachia kwa madai kwamba alikuwa akitaka kumpeleka shule.
Tangu hapo mama huyo anadai kwamba hawakuonana  na mwanaye mpaka alipopata habari zake kupitia kwenye vyombo vya habari.
ALIAHIDI KUMBAKA TANGU AKIWA TUMBONI!
Akieleza kwa uchungu, mama huyo alisema kwamba mwanaume huyo aliwahi kutoa ahadi ya kumbaka mwanaye huyo tangu alipokuwa hajazaliwa, wakati mama huyo alipokuwa na mimba ya mwezi mmoja.
“Baada ya kukorofishana naye kutokana na kitendo alichotaka kunifanyia, nikiwa na mimba ya mwezi mmoja,  mwanaume huyo aliniahidi kwamba kama nikizaa mtoto wa kike lazima alale naye ,” alifafanua mama huyo.
Mama huyo alisema kwamba Mohamed ametimiza lengo lake ambalo yeye hakutarajia kama angeweza kulifanya kwani alichukulia ni vigumu kwa mzazi kufanywa jambo kama hilo.
“Nilidhani maneno yale aliyatamka kwa hasira tu, kumbe alikuwa ameweka dhamira ya kweli moyoni na sasa ameitimiza,” aliongeza mama huyo kwa huzuni.
AOMBA MSAADA WA KISHERIA
Baada ya kufikwa na mambo hayo, mama huyo ameomba msaada wa kisheria ili mzazi mwenziwe huyo achukuliwe hatua kwani amekuwa akiwatishia maisha.

Wednesday, October 23, 2013

NEWZ ALERT: MSITU WA SAO HILL ULIOPO MUFINDI HUKO IRINGA WATEKETEA KWA MOTO JIONI HII...!!


 Msafara  wa rais Jakaya  Kikwete ukiwa  umesimama kwa muda eneo la  msitu wa  taifa  wa Sao Hill Mufindi  katika barabara kuu ya Iringa- Mbeya  kufuatia  moto mkubwa kuwaka katika msitu huo mchana wa leo
 Askari polisi akisimamisha  msafara  wa rais Kikwete kutokana na moto  mkubwa  kutanda  eneo hilo la Changalawe katika  msitu wa Taifa  wa Sao Hill umbali wa mita  mbili kuelekea  barabara  ya Ikulu ndogo mjini Mafinga
 Askari  wa FFU  wakishuka katika gari lao kwenda  kuangalia  usalama  wa rais Kikwete na  kulia gari la kwanza ni naibu waziri wa ujenzi gari la pili la la tatu ni magari ya Ikulu yakiwa  yamesimama
 hapa  askari  wakishuka  kuingia katika moshi mzito  kuangalia  usalama  wa rais katika eneo hilo ambalo moshi mzito  ulitanda barabarani


 Msafara  ukipita  eneo hilo salama huku kulia ni askari wa JKT mafinga wakizima moto  huo


YAKIWA  ni masaa takribani mawili  kupita  kutoka Rais Jakaya  Kikwete kufanya  kikao chake  cha majumuisho   ya ziara  yake   na  viongozi wa mkoa wa Njombe na  kuwataka  kuchukua hatua  katika kuthibiti moto  ili  kuepusha ukame ,moto  mkubwa umezuka katika msitu wa Taifa  wa Sao Hill Mufindi na kupelekea  msafara  wa  Rais kusimama kwa  muda  kiusalama kutoka na moshi mzito  uliotanda  barabara  kuu ya Iringa Mbeya .

Moto  ulio ulioanza  kuwaka  mida ya saa nane  mchana    ulizuia kwa  muda  kama dakika tatu hivi msafara  wa Rais Kikwete  kufimama katika eneo la Changalawe mjini  Mafinga umbali  wa mita 2  kufika  njiapanda  ya   kuingia ofisi ya mkuu  wa wilaya ya  Mufindi na Ikulu ndogo  ya  wilaya ya Mufindi.

Kutokana na tukio hilo la moto msafara  wa rais  Kikwete  ulisimama na baada ya maofisa  usalama  kushuka na kutazama usalama  zaidi wa msafara  huo ndipo  walioruhusu msafara  huo  kuendelea .

Hata  hivyo  jitihada  kubwa  zilionekana kufanywa na  kikosi  cha askari  wa  JKT Mafinga  pamoja na  wananchi ambao  walikuwa  wakizima  moto  huo .

Huku   vyombo  vya  usafiri  yakiwemo mabasi ya abiri yanayosafiri  kutoka Dar es Salaam kuwenda  mikoa ya  kusini na nchi  za kusini mwa Tanzania yakikwama  kuendelea na  safari  kutoka na moto  huo kushikakasi na  moshi  mzito  kutanda  barabara 

Mkuu  wa  mkoa  wa  Iringa Dr  Christine Ishengoma  alisema kuwa  uongozi  wa  mkoa  tayari  umeagiza  mkuu wa wilaya ya Mufindi kuwasaka   waliohusika na  uchomaji  moto huo ili  kuchukulia  hatua  kali.


Mkuu  huyo  wa  mkoa alisema  kuwa mkoa  wa Iringa umekuwa  ukichukua hatua  kali  kwa wale wote wanaoanzisha  moto  kichaa kama  huo hivyo  kupitia  ofisi ya mkuu wa wilaya ya Mufindi wahusika  watasakwa  popote  walipo .

Mbali na  hilo mkuu  huyo amelipongeza  jeshi la JTK Mafinga kwa  kuchukua hatua  za haraka katika kukabiliana na moto  huo huku akisema madhara  zaidi  yatokanayo na moto  huo yatatolewa baada ya  moto  huo kuthibitiwa
 

Mambomseto Copyright © 2011 -- Template created by MAMBOMSETO TEAM -- Powered by MAMBOMSETO

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter