Thursday, October 24, 2013

SAKATA LA MTOTO ALIYEBAKWA NA BABA YAKE KWA MIEZI 9... MAMA MZAZI ASIMULIA MAZITO..!!

WIKI kadhaa zimepita tangu binti wa miaka 15 (jina tunalihifadhi) mkazi wa Kimara jijini Dar kupasua jipu la kubakwa na baba yake mzazi aliyefahamika kwa jina laMOHAMEDkwa miezi tisa, mama mzazi wa mtoto huyo amejitokeza na kusimulia mambo mazito zaidi.
Akizungumza na Ijumaa, mama huyo aitwaye Nusura amesema alipata habari za mwanaye kutendewa unyama wa kuingiliwa na mwanaume aliyezaa naye kupitia vyombo vya habari na kufunga safari kutoka Kigamboni jijini Dar hadi Kimara kwa viongozi wa serikali ya mtaa anakoishi mtoto wake huyo.
MSIKIE MAMA HUYO
Mwanamke huyo alisema alikutana na Mohamed (baba wa mtoto huyo) na kupendana naye hadi kufikia mwanaume huyo kwenda kujitambulisha nyumbani kwa wazazi wake.
“Lakini siku chache kabla hajatimiza lengo hilo la kuleta barua ya posa nilijigundua kuwa na ujauzito wa mwezi mmoja,” alisema.
Mama huyo anasema wakati wa ujauzito huo, mwanaume huyo alianza kumbadilikia na kutaka kumtumia kinyume na maumbile jambo ambalo alilikataa na kwenda kumweleza mama yake ambaye alimshauri kuachana naye.
Baada ya kukubaliana na ushauri aliopewa na mama yake mzazi, uhusiano wa wawili hao ukavunjika na miezi tisa baadaye akazaliwa binti aliyefanyiwa unyama.
Mtoto huyo alipozaliwa alikuwa chini ya uangalizi wa mama yake na bibi yake bila mzazi wa kiume kutoa matumizi yoyote kwa ajili ya mtoto.
KUMBE ALIMUIBA?
Kwa mujibu wa mama huyo, baba alimwiba mtoto huyo alipokuwa na umri wa miaka mitano na kumpeleka Manzese, Dar ambapo mama yake huyo alimfuatilia lakini baba huyo alikataa katakata kumwachia kwa madai kwamba alikuwa akitaka kumpeleka shule.
Tangu hapo mama huyo anadai kwamba hawakuonana  na mwanaye mpaka alipopata habari zake kupitia kwenye vyombo vya habari.
ALIAHIDI KUMBAKA TANGU AKIWA TUMBONI!
Akieleza kwa uchungu, mama huyo alisema kwamba mwanaume huyo aliwahi kutoa ahadi ya kumbaka mwanaye huyo tangu alipokuwa hajazaliwa, wakati mama huyo alipokuwa na mimba ya mwezi mmoja.
“Baada ya kukorofishana naye kutokana na kitendo alichotaka kunifanyia, nikiwa na mimba ya mwezi mmoja,  mwanaume huyo aliniahidi kwamba kama nikizaa mtoto wa kike lazima alale naye ,” alifafanua mama huyo.
Mama huyo alisema kwamba Mohamed ametimiza lengo lake ambalo yeye hakutarajia kama angeweza kulifanya kwani alichukulia ni vigumu kwa mzazi kufanywa jambo kama hilo.
“Nilidhani maneno yale aliyatamka kwa hasira tu, kumbe alikuwa ameweka dhamira ya kweli moyoni na sasa ameitimiza,” aliongeza mama huyo kwa huzuni.
AOMBA MSAADA WA KISHERIA
Baada ya kufikwa na mambo hayo, mama huyo ameomba msaada wa kisheria ili mzazi mwenziwe huyo achukuliwe hatua kwani amekuwa akiwatishia maisha.

DEAR READER LEAVE A COMMENT BELOW

SHARE THIS POSTS TO YOUR FRIENDS BELOW==>>

DONT HESITATE TO JOIN OUR FACEBOOK PAGE BELOW FOR MORE BREAKING AND HOT RESEARCHED NEWS

0 comments em “SAKATA LA MTOTO ALIYEBAKWA NA BABA YAKE KWA MIEZI 9... MAMA MZAZI ASIMULIA MAZITO..!!”

Post a Comment

 

Mambomseto Copyright © 2011 -- Template created by MAMBOMSETO TEAM -- Powered by MAMBOMSETO

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter