Kutokana na kutokea hitilafu ya umeme Alfajiri ya leo kwenye show ya Serengeti Fiesta Dar, iliyopelekea baadhi ya wasanii waliokuwa wakitarajia kupanda jukwaani kutumbuiza akiwemo Davido, Mohombi, Diamond, Nay wa Mitego na wengine kushindwa kupanda, leo kuanzia saa tisa, wasanii hao watapanda tena jukwaani kuzikonga nyoyo za mashabiki wao bila kiingilio chochote.
Ni katika uwanja ule ule, jukwaa lile lile la Serengeti Fiesta Dar es Salaam ambapo Diamond,Davido,Mohombi pamoja na Nay wa Mitego watapanda kuanzia saa 9 jioni mpaka saa 12.Show hiyo ya bure itapambwa pia na bendi ya Twanga Pepeta.
-Habari kwa hisani ya bongo5
DEAR READER LEAVE A COMMENT BELOW
SHARE THIS POSTS TO YOUR FRIENDS BELOW==>>
DONT HESITATE TO JOIN OUR FACEBOOK PAGE BELOW FOR MORE BREAKING AND HOT RESEARCHED NEWS