Showing posts with label BONGO FLAVOUR. Show all posts
Showing posts with label BONGO FLAVOUR. Show all posts
Friday, November 8, 2013
HII NDIO VIDEO ILIYOMPONZA SHILOLE KWENYE MITANDAO YA KIJAMII...!! BOFYA HAPA KUITAZAMA..
Posted by
Teacher Hawa
at
10:54 PM
Wednesday, November 6, 2013
Tuesday, November 5, 2013
Baby Madaha akanusha kutoa rushwa ya ngono kwa bosi wake wa Candy n Candy
Posted by
Teacher Hawa
at
11:26 PM
Msanii wa label ya Candy n Candy Baby Joseph Madaha amekanusha uvumi uliovumishwa na wanamuziki wenzake wa labe hiyo kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na CEO, Joe Kariuki.
Uvumi huo ulianzishwa na baadhi ya wasanii wengine, wa label hiyo wanaodai kuwa tangu Baby Madaha asainishwe Candy n Candy maisha yake yamebadilika na kwamba amekuwa akipendelewa zaidi.
Akizungumza Bongo5 jana , Baby amesema CEO wa Candy N Candy, Joe Kariuki alishauriwa na wadau kwamba amwendeleze yeye na akifanikiwa awasaidie na wenzake.
“Joe amesikia na hajapenda hili swala kwasababu sisi tupo kizazi zaidi kwasababu mimi najituma kufanya kazi ya muziki ambayo imenipeleka Candy n Candy na sio mambo mengine kama wanayosema wao.
"Huu ni wivu ni kwasababu mimi ni msanii mkubwa tayari nimeshatengeneza jina kwenye muziki sema kuna kipindi nilijikita kwenye filamu sana, kwahiyo siwezi lingana nao hata kidogo,” amesema.
“Candy n Candy walihitaji mwanadada ambaye ataweza kuongea zaidi ya lugha mmoja kwasasababu ya kufanya muziki kimataifa na kigezo kingine walichokitaka ni huyo mwanamuziki mwanadada kuwa na mwenekano mzuri.
" Wasanii wote wa Candy n Candy tulipelekwa studio, tukarekodi kila msanii.Wale Four – D ndio walianza kurekodi sasa kukawa na msichana mmoja anatoka kimapenzi na msanii mwezake wakawa wanatukanana na kushikanashikana pamoja na kumsema bosi wao.
"Baada ya kurekodi bosi akapokea ushauri kutoka kwa wadau kwamba ‘hii kazi ya Four – D ni mbaya kwanini usimwendeleze Baby Madaha halafu baadaye Baby Madaha akawainua wenzake’.
"Bosi akatuambia ‘sasa ngoja nianze na Baby Madaha nyie wengine mtafuata’ wale Four – D hawakuwa wavumilivu ndio wakaanza kusema maneno mengi,” amefafanua Baby na kuongeza
“Kiukweli mimi najituma katika kazi, Top C wanataka wafanyiwe kila kitu watafutiwe kila kitu.
"Kwahiyo mimi naona kama wangenisikiliza mimi kama mimi kwasababu nimepitia kwenye academy ya muziki kwahiyo naulewa muziki, haikuwa na sababu ya kuongeaongea maneno mtaani.
"Mpaka leo Top C anapigiwa simu akafanye video hawajaenda wanasema ana matatizo ya kifamilia, sasa ni bosi gani aache kufanya kazi na watu ambao wako serious amfuate yule aliye bize?"
Hata hivyo Baby amesema kwa kuwa Joe ni mwanaume na yeye ni mwanamke endapo wakiwa wapenzi si japo la kushangaza wakikubaliana kufanya hivyo.
“Haya ni mafanikio yangu ndio maana wanaongea,leo nimezindua bag na perfumes wana wivu, kwani Joe si yupo single na mimi nipo hivyo hivyo!! Kwahiyo kama tukikubalina personal ni sisi,muziki ni muziki na mapenzi ni mapenzi. Kwahiyo yote yanawezekana.”
Monday, November 4, 2013
WEMA NA DIAMOND WAMFANYA HUDDAH MONROE KUWA GUMZO MTANDAONI BONGO
Posted by
Teacher Hawa
at
11:32 PM
Hivi majuzi mwanadada Huddah MonroeUchunguzi uliofanya na bongomovies umebaini kuwa mashabiki wengi wa muziki na filamu hapa nchini wanapenda sana mahusiano baina ya wawil hawa (Wema na Diamond
Katika pitapita zetu kwenye mtandao tuliweza kupata kauli hizi za watu mbalimbali wakimsifia Huddah kwa kauli yake hiyo huku wengine wakimuona kama ni shujaa….
“Umenifurahisha sana leo yaan had nime comment!!@huddahmonroe”
mmoja wapo aliandika…
“Kuanzia leo nakupenda bureee....na nakufollow@huddahmonroe”
mwingine aliongezea…
“Nakupenda bureee Huddah we ni shujaa”… mwingine naye aliongezea huku wakidiriki kusema kuwa wawili hawa wakioana basi itakuwa kama siku ya mapumziko ya kitaifa kwao.
Sunday, November 3, 2013
Wednesday, October 30, 2013
Rushwa ya ngono kwa boss wake yamponza Baby Madaha baada ya wanakundi kuanza kumtenga
Posted by
Teacher Hawa
at
11:03 PM
Mwanamuziki na mwigizaji Bongo, Baby Joseph Madaha ‘Baby Madaha’, amemshukia mwanamuziki memba mwenzake wa Candy n’ Candy, Top C na kumtaka asimuingilie katika maisha yake.
Kupitia kipindi cha redio hivi karibuni, Top C alisema tangu Baby Madaha asajiliwe katika kampuni hiyo ya muziki iliyopo nchini Kenya, memba wengine wamekuwa wakipuuzwa na bosi wao, Joe Kairuki kiasi kwamba hawasikiki kabisa na kuainisha kuwa Baby anatamba kwa sababu amekuwa ‘kiburudisho’ cha bosi huyo.
Alipoulizwa kuhusiana na tuhuma hizo, Baby alikanusha:
“Top C na wenzake ni wazushi, sina uhusiano na Joe. Mimi nina kipaji kikubwa na nina nidhamu ya kazi kuliko wao ndiyo maana ninapewa nafasi. Wanaendekeza uzushi kwa nini wasipigwe chini?”
MWIGIZAJI ASHELY TOTO KUTOKA KENYA INASEMEKANA NDIO SABABU MOJA WAPO YA NDOA YA BOB JUNIOR KUVUNJIKA....
Posted by
Teacher Hawa
at
10:55 PM

Ashely Toto in German
![]() |
| Hapa Bob Junior Akiwa Mombasa na Ashley Toto hivi Karibuni |
![]() |
| Hapa Bob Junior Akiwa Ujerumani na Dada Ashley Toto |
![]() |
| Wakila Raha Ujerumani Frankfurt |
![]() |
| Wakiwa Ujerumani Mall Wakifanya Shopping |
Ashley Toto Ni Msanii wa movies kutoka Kenya ambae makazi yake ni Ujerumani ila kwa sasa yupo Mombasa kwa mapumziko ..Mnyetishaji wa habari ametuhabarisha kuwa wawili hawa wapo mapenzini kwa muda mrefu sana hata alipokuwa Ujerumani Bob Junior huwa anaenda huko kama baadhi ya picha zinavyoosha ..Pia inasemekana kuwa baada ya Mwana Dada huyu kuja Mombasa kwa mapumziko Bob Junior alienda Matembezi huko na Kukaa kwa muda wa week moja akiwa nae na baadae Mwana dada huyo Mrembo alimtafutia Show mbili Huko Mombasa ...Inasemekana ndio Sababu mojawapo ya mke wake kuona wivu wa mapenzi na kuamua kuachana na Bob junior..
DIAMOND LUPANGO MIEZI MIWILI BAADA YA KUGOMBEA DEMU....
Posted by
Teacher Hawa
at
10:49 PM
![]() |
| Nasibu Abdul ‘Diamond’. |
STAA wa muziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ amewahi kusota lupango ya Keko, Temeke jijini Dar es Salaam kwa miezi miwili kisa kikiwa ni kugombea demu wa mtu.
Akizungumza na Amani juzi jijini Dar, Diamond alisema tukio hilo lilimtokea mwaka 2007 akiwa ‘andagraundi’ wa muziki wa kizazi kipya.
Diamond aliyasema hayo kufuatia kuulizwa swali na paparazi wetu kwamba, amerudiana na Miss Tanzania 2006 ambaye pi ni staa wa filamu za Bongo, Wema Sepetu. Je, haogopi kufanyiwa kitu mbaya na jamaa wake ambaye ndiye anayemuweka mjini?
Msikie Diamond: Mimi simwogopi mtu eti kwa sababu natembea na demu wake. Hakuna anayeweza kunifanya lolote lile, najiamini.
“Mwaka elfu mbili na saba niligombea demu na jamaa mmoja pale Tandale (Dar). Matokeo yake jamaa akanikamata na kuniweka Gereza la Keko kwa miezi miwili, nikaachiwa baadaye, kwa hiyo sitishiki,” alisema Diamond.
Hata hivyo, Diamond hakuweka wazi kwamba baada ya kukamatwa alipelekwa kituo gani cha polisi na mahakama gani alipandishwa kabla ya kupelekwa mahabusu ya Keko.
"BASATA KUNA KITU WANATAFUTA KUTOKA KWANGU"......NEY WA MITEGO
Posted by
Teacher Hawa
at
3:20 AM
Siku chache zilizopita mwana Hip Hop kutoka pande za Manzese Nay Wa Mitego alipokea barua kutoka BASATA inayomtaka kubadili aina ya mavazi anayovaa katika show zake (mlegezo/mtepesho) ambayo hayaendani na Tamaduni za kitanzania.

Akizungumza na Bongo5 leo kwa njia ya simu Nay amesema amekuwa akivaa mlegezo kwa kipindi cha miaka ishirini hali ambayo itamwia vigumu kubadilika kutokana ni mtindo ambao ata mashabiki wake wengi wameuzoea.
“Nahisi kuna kitu kingine wanakitaka toka kwangu kuhusu muziki wangu ndiyo maana wananitishia kunifungia wakati mimi nafanya muziki kama ndiyo maisha yangu, kwahiyo kubadilika kwa haraka kuvaa mlegezo siwezi labda baada ya miaka 3 ila inategemea” Alisema Nay.
Aidha katika mahojiano mengine na kipindi cha Showtime kupitia kituo cha RFA ya Mwanza Nay amesema kuwa Baraza hilo lina majukumu mengi ya kufanya kwaajili ya kuboresha maslahi ya wasanii badala ya kuhangaika na kumzuia kuvaa mlege ili hali wanaovaa hivyo ni wengi.
“Sasa hata baraza la sanaa Tanzania wana shughuli nyingi sana za kufanya nyingi sana ili sanaa yetu isonge mbele mambo yetu yaani wasanii tuishi maisha mazuri lakini si swala la kufuatilia mlege wa Nay, hapana kuna kitu behind ambacho kinaendelea sijui ni nini maybe wameamua waanzie hapo ili wastopishe kile ambacho nakifanya.”
Akizungumza na Bongo5 leo kwa njia ya simu Nay amesema amekuwa akivaa mlegezo kwa kipindi cha miaka ishirini hali ambayo itamwia vigumu kubadilika kutokana ni mtindo ambao ata mashabiki wake wengi wameuzoea.
“Nahisi kuna kitu kingine wanakitaka toka kwangu kuhusu muziki wangu ndiyo maana wananitishia kunifungia wakati mimi nafanya muziki kama ndiyo maisha yangu, kwahiyo kubadilika kwa haraka kuvaa mlegezo siwezi labda baada ya miaka 3 ila inategemea” Alisema Nay.
Aidha katika mahojiano mengine na kipindi cha Showtime kupitia kituo cha RFA ya Mwanza Nay amesema kuwa Baraza hilo lina majukumu mengi ya kufanya kwaajili ya kuboresha maslahi ya wasanii badala ya kuhangaika na kumzuia kuvaa mlege ili hali wanaovaa hivyo ni wengi.
“Sasa hata baraza la sanaa Tanzania wana shughuli nyingi sana za kufanya nyingi sana ili sanaa yetu isonge mbele mambo yetu yaani wasanii tuishi maisha mazuri lakini si swala la kufuatilia mlege wa Nay, hapana kuna kitu behind ambacho kinaendelea sijui ni nini maybe wameamua waanzie hapo ili wastopishe kile ambacho nakifanya.”
JENEZA LA DIAMOND LAIBUA MAZITO.... !!
Posted by
Teacher Hawa
at
12:53 AM
Diamond akipozi na madansa wake siku alipoingia na jeneza katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar.
Diamond ambaye wimbo wake mpya wa ‘Number One’ upo katika chati ya juu katika muziki huo, usiku wa kuamkia Jumapili iliyopita aliingia na jeneza hilo katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar na kusababisha maswali mengi tata kutoka kwa mashabiki waliojazana kwenye onesho la Serengeti Fiesta 2013. ILIKUWA SAPRAIZI
Mapaparazi waliokuwa wamejaa katika viwanja hivyo wakihakikisha wananasa matukio muhimu hasa yale ‘exclusive’, walipenyezewa mapema kuhusu Diamond kuingia na jeneza.
Mtoa habari alisema Diamond aliingiza jeneza viwanjani humo kwa lengo la kupanda nalo jukwaani wakati akiimba wimbo wake uitwao Nikifa Kesho ambao mashabiki wake wengi wanasema amejichulia kifo.
Kwa sharti la kutoandikwa jina lake , mtoa habari huyo ambaye ni mtu wa karibu na Diamond alisema:
“Diamond amekuja na jeneza, limefichwa kule nyuma wanakobadilishia nguo wasanii, atapanda nalo jukwaani. Anataka kuwafanyia sapraizi mashabiki wake.”
SAPRAIZI YAKWAMA
Hata hivyo, baada ya matatizo ya kiufundi yaliyojitokeza, Diamond hakuweza kupanda jukwaani Jumamosi usiku huo na badala yake akatakiwa kupanda kesho yake Jumapili ambapo pia hakulitumia jeneza hilo kama mawazo yake ya awali yalivyokuwa.
Mapaparazi wetu walisaka sehemu lilipohifadhiwa jeneza hilo na kufanikiwa ambapo pia walikuta baadhi ya watu wakilishangaa na kuulizana maswali.
MASWALI TATA
Nurdin Ali, mkazi wa Mbagala, Dar aliyeliona jeneza la Diamond alisema:
“Mimi namkubali sana huyu bwana mdogo lakini sasa mambo ya majeneza jukwaani ya nini tena?
“Sikubaliani na hili suala. Hata wimbo wake wa Nikifa Kesho sioni kama una mantiki. Ni kama tu anajitabiria kifo. Anapita mlemle alimopita marehemu Kanumba, maana naye aliimba wimbo akielezea itakavyokuwa siku akifa, ikawa kweli.
“Lakini Diamond amekwenda mbele zaidi kwa kuamua kuja na jeneza kabisa stejini. Sijui amenunua au amekodisha, ila sikubaliani naye hata kidogo.”
MATUMIZI YA JENEZA
Mwingine aliyekataa kuandikwa jina lake alisema:
“Halafu kama lengo lake lilikuwa kuonesha uhalisia wa kifo katika wimbo wake, kwa nini asingekuja na jeneza la imani yake? Angalia, jeneza lina msalaba ambao unakubalika katika imani ya Kikristo, kwa nini asije na jeneza la Kiislamu au sanduku ambalo halina msalaba?”
Akaongeza: Au inawezekana huyu jamaa anataka kubadili dini ili aoane na Penny (Penniel Mungilwa) ambaye ni Mkristo kwa sababu huku ni kukana imani yake kimyakimya.”
ALIWAHI KUTANGAZA KUJENGA MSIKITI
Shabiki mwingine alikwenda mbali zaidi na kusema kama Diamond ni muumini mzuri wa Kiislamu tena mwenye lengo la kujenga msikiti kama alivyowahi kutangaza siku za nyuma, anatakiwa kutofungamana kabisa na ishara zinazoonesha anaunga mkono imani nyingine.
“Anapaswa kuwa makini na mambo yake na awe na washauri wazuri, vinginevyo atakuwa anafanya mambo yanayoibua maswali mengi kwa jamii inayomwamini,” alisema shabiki huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Jennifer.
HUYU YUPO TOFAUTI
Shabiki aliyejitambulisha kwa jina la Hamadi Hajj (34) mkazi wa Kijitonyama, Dar alisema:
“Hakuna uhusiano wowote kati ya hili jeneza na mambo ya kubadilisha dini au kuiunga mkono. Kikubwa ni lengo alilotaka litimie.
“Ukiachana na hilo, mambo mengine yako wazi jamani. Upatikanaji wa majeneza ya Kikristo ni rahisi zaidi tofauti na ya Kiislamu. Wabongo wanapenda sana kukuza mambo,” alisema Hajj.
Siku hiyohiyo, usiku huohuo, mapaparazi wetu walimbana Diamond kuhusu kutinga Leaders na jeneza ambapo alijitetea hivi:
“Ni swaga tu zile.”
Alipobanwa zaidi na kuulizwa ni swaga gani zinazochanganywa na vitu vinavyoashiria huzuni na imani ambayo si yake, alisema:
“Nilitaka kuwafurahisha mashabiki wangu na kuwapa uhalisia wa ule wimbo wangu wa Nikifa Kesho, sikuwa na nia ya kukashifu imani ya mtu.”
FIESTA PART II
Baada ya shoo yake kushindikana na kuhamishiwa siku iliyofuata (Jumapili), timu yetu ilitinga viwanjani hapo ili kujua kama Diamond angepanda na jeneza hilo kama alivyotarajia lakini jeneza halikuwepo eneo lilipohifadhiwa awali.
Diamond alipofuatwa na kuulizwa kama mpango wake bado uko palepale, alijibu:
“Lile jeneza nilipanga kupanda nalo jukwaani wakati nikiwa naimba wimbo wangu wa Nikifa Kesho lakini kwa bahati mbaya sikuweza kupanda kuimba kutokana na matatizo ya kiufundi, leo (Jumapili) nisingeweza kupanda nalo kwa kuwa muda tuliopewa ni mfupi sana,” alisema Diamond.
Alipobanwa kuhusu kutumia jeneza la Kikristo na kuhusishwa na fununu za kubadili dini, alisema hana mpango huo kabisa.
“Naomba nieleweke, mimi sikuwa na nia tofauti zaidi ya kuwakilisha kilichopo katika wimbo wangu. Lengo lilikuwa kuonesha uhalisia tu wa kibao changu cha Nikifa Kesho, siyo zaidi ya hivyo,” alisema.
Inasemekana kwamba Diamond aliamua kubadilisha uamuzi wake wa kupanda na jeneza jukwaani siku hiyo baada ya kunyetishwa na watu wanaomtakia mema kuwa asingeonesha picha nzuri kwa jamii, hasa kwa vile jeneza hilo lilikuwa na msalaba juu ya mfuniko.
katika Viwanja vya Leaders Club, Kinondoni, Dar
Monday, October 28, 2013
LULU NA ALIKIBA KWENYE PENZI JIPYAA...!!
Posted by
Teacher Hawa
at
5:23 AM
Katika hali isiyokuwa ya kawaida na yakushangaza kwa watu wengi inasemekana baada ya lulu alimpigia sim Ali kiba wakutane hoteli moja hivi wapate dina mambo ndo yakawa hivi kama mnavyojionea wenyewe kwenye picha , ila baada ya kupata msosi yaliyoendelea haikujulikana walitoka saa ngapi.
-uswazi blog
-uswazi blog
ANGALIA HAPA REMIX YA 'MY NUMBER 1' YA DIAMOND NA DAVIDO ILIVYONOGA HAPO JANA PALE LEADERZ CLUB...!!
Posted by
Teacher Hawa
at
4:26 AM
Sunday, October 27, 2013
DIAMOND, DAVIDO, MOHOMBI NA NAY WA MITEGO KUFANYA SHOW YA BURE LEADERS CLUB LEO SAA TISA MCHANA..
Posted by
Teacher Hawa
at
5:06 AM
Kutokana na kutokea hitilafu ya umeme Alfajiri ya leo kwenye show ya Serengeti Fiesta Dar, iliyopelekea baadhi ya wasanii waliokuwa wakitarajia kupanda jukwaani kutumbuiza akiwemo Davido, Mohombi, Diamond, Nay wa Mitego na wengine kushindwa kupanda, leo kuanzia saa tisa, wasanii hao watapanda tena jukwaani kuzikonga nyoyo za mashabiki wao bila kiingilio chochote.
Ni katika uwanja ule ule, jukwaa lile lile la Serengeti Fiesta Dar es Salaam ambapo Diamond,Davido,Mohombi pamoja na Nay wa Mitego watapanda kuanzia saa 9 jioni mpaka saa 12.Show hiyo ya bure itapambwa pia na bendi ya Twanga Pepeta.
-Habari kwa hisani ya bongo5
Friday, October 25, 2013
Picha za maandalizi ya jukwaa la Serengeti Fiesta itakayofanyika kesho ndani ya viwanja vya Leaders Club
Posted by
Teacher Hawa
at
4:30 AM



Pichani ni sehemu ya maandalizi ya jukwaa la kisasa kabisa la Serengeti Fiesta 2013 ndani ya viwanja vya Leaders Club,Kinondoni jijini Dar,tamasha hilo ambalo litawajumuisha wasanii wa muziki wa kizazi kipya zaidi ya 50 wakiwemo na wageni kutoka nchini Nigeria linatarajiwa kufanyika kesho jumamosi ndani ya viwanja vya liders club,ambapo kiiingilio kimepangwa kuwa ni shilingi 10,000 na 15,000 kwa mtu mmoja.
Thursday, October 24, 2013
PICHA NA VIDEO YA MAPOKEZI YA MSANII DAVINO KUTOKA NIGERIA KWA AJIRI YA FIESTA
Posted by
Teacher Hawa
at
10:23 PM
Muimbaji wa Skelewu, Mnaigeria Davido ametua jijini Dar es Salaam akiwa na ulinzi mkali wa mabaunsa takriban wanne walioshiba. Akiwa na kofia, miwani nyeusi na kibegi mgongoni kama mtoto wa shule, Davido alitua kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Julius Nyerere saa tano usiku.
Davido akihojiwa na Clouds TV
Muda mfupi baada ya kufika Dar es Salaam, Davido alitweet:
Hitmaker huyo ni mmoja wa wasanii wa kimataifa watakaotumbuiza Jumamosi hii kwenye Serengeti Fiesta ya Dar es Salaam itakayofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club.
Davido akihojiwa na Clouds TV
Muda mfupi baada ya kufika Dar es Salaam, Davido alitweet:
Hitmaker huyo ni mmoja wa wasanii wa kimataifa watakaotumbuiza Jumamosi hii kwenye Serengeti Fiesta ya Dar es Salaam itakayofanyika kwenye viwanja vya Leaders Club.
Wednesday, October 23, 2013
EXCLUSIVE: DOGO JANJA AFUKUZWA RASMI MTANASHATI ENTERTINMENT...!!
Posted by
Teacher Hawa
at
4:23 AM
Msanii mdogo aliyewahi kutamba katika tasnia ya muziki wa bongo fleva Dogo Janja amefukuzwa rasmi Mtanashati Entertinment, Taarifa zilizofikia dawati letu la habari zinasema Dogo Janja amefukuzwa na Ostazi Juma Na Musoma baada ya kushindwana kitabia, Hapo awali Dogo Janja aliwahi kuwa mwanakundi la Tip Top Connection lililo chini ya uongozi wa Madee hata hivyo alifukuzwa na kurudi kwao Arusha ambapo Ustazi Juma Na Musoma alimfuata na na kumuweka kundini huku akimuhudumia katika kila jambo ambalo alitakiwa kupata kama mtoto na mwanamuziki pia. Lakini Leo imefika tamati ya Ostazi Juma na kuamua kumuacha Dogo Janja aende zake.
Vile vile kutoka katika kundi hilo la Mtanashati Kuna nyimbo mpya ya msanii PNC inayokuja hivi karibuni, ni Bonge moja la track linakwenda kwa jina la HABARI YA MJINI, nyimbo hii itayoachiwa hvi karibuni itakuja pamoja na video kali. Jiandae kwa nyimbo kali kutoka kwa PNC
Tuesday, October 22, 2013
PICHA!!, Diamond Kaomba Mashabiki Watume Picha Wakiwa Kwenye Pozi Kama Lake, TAZAMA VITUKO Hapa.
Posted by
Teacher Hawa
at
3:07 PM
JE WAJUA KWA NINI DIAMOND NI TAJIRI NA MZEE GURUMO NI MASIKINI...?? SOMA HII MAKALA HAPA...
Posted by
Teacher Hawa
at
4:23 AM
MWAKA 2005 nilikuwa nikipanda daladala na Naseeb Abdul (Diamond) katika kituo cha Shule Tandale Magharibi jijini Dar es Salaam. Wakati huo, sikuwa hata na wazo kwamba atakuja kuwa mtu maarufu katika muziki hata kushughulisha watu kutaka kujua zaidi kuhusu maisha yake.
Baada ya hapo nikaanza kuona wimbo wake wa kwanza kwenye video, ‘Nenda Kamwambie’ kilikuwa kibao kizuri kilichompa umaarufu, ndipo alipoanza kunivutia kusikiliza nyimbo zake. Baada ya video ile sikumuona tena kituoni kama ada yetu, nikaanza kusikia anaendesha gari aina ya Toyota Celica.
Kutoka mwaka 2006 mpaka sasa ni mfululizo wa mafanikio aliyoendelea kuyapata kijana huyu aliyezaliwa Septemba 28, 1988 mpaka kuwa mwanamuziki wa kwanza Tanzania kulipwa pesa nyingi kutokana na shughuli hiyo.
Baada ya hapo nikaanza kuona wimbo wake wa kwanza kwenye video, ‘Nenda Kamwambie’ kilikuwa kibao kizuri kilichompa umaarufu, ndipo alipoanza kunivutia kusikiliza nyimbo zake. Baada ya video ile sikumuona tena kituoni kama ada yetu, nikaanza kusikia anaendesha gari aina ya Toyota Celica.
Kutoka mwaka 2006 mpaka sasa ni mfululizo wa mafanikio aliyoendelea kuyapata kijana huyu aliyezaliwa Septemba 28, 1988 mpaka kuwa mwanamuziki wa kwanza Tanzania kulipwa pesa nyingi kutokana na shughuli hiyo.
Kutokana na utafiti uliofanywa na tovuti inayozungumzia masuala ya vijana inasemekena ‘Diamond Platnamz’ anapata kiasi cha Sh Mil 16 kwa matamasha mawili anayofanya katika mwezi.
Mbali ya mikataba minono aliyoingia na makampuni mbalimbali yanayonufaika kwa taswira ama sauti ya mwanamuziki huyo kijana, Diamond anaingiza fedha nyingi kila anaposafiri nje ya Tanzania na bara la Afrika kufanya matamasha ya muziki.
Mbali ya mikataba minono aliyoingia na makampuni mbalimbali yanayonufaika kwa taswira ama sauti ya mwanamuziki huyo kijana, Diamond anaingiza fedha nyingi kila anaposafiri nje ya Tanzania na bara la Afrika kufanya matamasha ya muziki.
Wakati Diamond, ambaye hajatimiza hata miaka kumi kwenye tasnia ya muziki kuna mtu mmoja anaitwa Muhidini Gurumo, amejishughulisha na muziki kwa takriban miaka 45 lakini kila alipokutana na swali hili kutoka kwa wanahabari kuwa kwa kipindi chote hicho muziki umemsaidia nini, jibu lake ni: “Bado hakuna ninachoweza kujivunia kupitia muziki, hali ya maisha ni ngumu.”
Gurumo ambaye alizaliwa 1940 alianza muziki mwaka 1959 akiwa na bendi ya Kilimanjaro Chacha Band. Sasa ni takriban miaka 45, umri wa baba mwenye wajukuu lakini alichofanikiwa ni kujenga nyumba mbili na kupata shamba moja. Gari lenyewe alizawadiwa na Diamond mwaka huu baada ya kulalamika sana kwenye vyombo vya habari.
Nini Tatizo
Maalim Gurumo (Kamanda), analalamika kuwa wanamuziki wa kizazi kipya wanasifiwa sana na vyombo vya habari. Akisisitiza kuwa hawana ubunifu, nyimbo zao hazina athari katika jamii na hudumu chini ya mwaka mmoja zinapoteza taswira.
Lakini amesahau kuwa wanamuziki wa sasa wengi wamejiajiri, kipindi hicho bendi nyingi zilimilikiwa na kampuni, taasisi ama mtu ambaye anapenda sanaa hiyo ya muziki.
Lakini sasa wanamuziki wameamka, wanajimiliki wenyewe pesa wanazopata zinaingia mifukoni mwao.
Mathalan tangu Diamond aanze kuimba ameshaingia zaidi ya mikataba kumi tofauti ambayo ilimnufaisha yeye kama Diamond, matamasha yake yanamnufaisha yeye, kikundi anachomiliki anakilipa kiasi wanachokubaliana kutokana na uwezo wa mwanakikundi.
Mwaka jana, 2012, Diamond aliingia mkataba na kampuni ya I-View Studios wa kusimamia kazi zake zote kwa miaka miwili. Huu ni mkataba ambao umemjengea heshima kubwa sana. Ingawa kiasi cha malipo kilifanywa siri lakini inaonekana ni mkataba mnono.
Kampuni nyingine ya One Touch, ilifunga naye mkataba wa kuwa wasemaji wake. Yaani kila anachotaka kufanya ama kuzungumza kwenye jamii, ikiwa kuna kampuni inataka kufanya naye mazungumzo ya kibiashara, One Touch Company ndio watakaofanya kazi hiyo.
Hilo tu linamfanya Diamond awe na uwezo mkubwa wa kupata fedha kutokana na muziki. Mara nyingine msanii anashindwa kujua thamani yake, anaweza kutaja kiasi kidogo cha fedha katika ‘dili’ kubwa. Lakini kwa kupata mtu wa kukusimamia kwenye mazungumzo ya kifedha lazima uwe tajiri.
Aidha, bendi ambazo Maalim Gurumo amehama kutokana na sababu za kimaslahi hazipungui kumi, alianza na Kilimanjaro Chacha Band, Kilwa Jazz Band, NUTA Jazz Band, Mlimani Park, Safari Sound Ochestra, Rufiji Jazz, na nyingine nyingi kabla ya kumalizia muziki kwenye bendi kongwe ya Msondo Ngoma Music Band.
Kote huko alizunguka kwa kutumia kichwa kitupu kujadili thamani ya sauti yake, hakuwa na mshauri wa masuala ya muziki ambaye atamwambia kutokana na thamani yako usikubali kuhama bendi hii ili kuenda bendi nyingine bila kupewa kiasi fulani cha fedha.
Aliweza kuitwa baa akawa anakunywa bia na nyama choma huku anajadili mustakabali wa maisha yake na mkurugenzi wa bendi pinzani na anayofanyia kazi.
Katika mazungumzo yake na wanahabari Maalim Gurumo aliwahi kutamka kuwa anatamani siku zirudi nyuma ili anufaike na muziki wake. Lakini nakataa, hata awe vipi kutokana na mfumo anaoutumia hawezi kuwa tajiri kama Diamond.
Leo hii, Maalim Gurumo akiandaa tamasha na kuingiza Sh Mil 50, basi atakachoambulia ni asilimia 10 ya mapato ambayo ni Sh Mil 5, ambacho kitakuwa ni kiasi kikubwa kuwahi kukipata kwa tamasha moja tangu aanze kuimba.
Lakini siku hiyohiyo Diamond akialikwa katika tamasha hilo la Gurumo ataondoka na Sh Mil 8 taslimu bila kupungua senti. Bado tofauti ipo kubwa.
Aidha, mbali ya mapato ya stejini lakini Diamond ana mikataba minono na makampuni ya simu ambayo yanatumia nyimbo zake kama miito ya simu, ana mkataba mwingine mnono na kampuni ya Vodacom, ana mkataba na kampuni ya vinywaji baridi ya Coca Cola hata kufikia kujiita Coke Boy.
Tukiwakusanya wanamuziki wa zamani kuanzia Mbaraka Mwinshehe mpaka kufikia Maalim Gurumo, bado hawawezi kufikia mafanikio ya muda mfupi aliyoyapata kijana mdogo Naseeb Abdul ‘Diamond’ ambaye hata ladha ya ndoa hajaionja kutokana na umri wake kuwa mdogo.
Wakati Gurumo akijisifia nyumba mbili alizojenga kwa tamu, Diamond ana nyumba zaidi ya mbili ambapo moja amemjengea mama yake yenye thamani inayofikia zaidi ya Sh Mil 50.
Pengine Gurumo ni mwanamuziki bora zaidi kuliko Diamond lakini mwenziye amemzidi kwenye ujanja wa kutafuta fedha
source: Raia Mwema
Sunday, October 20, 2013
NISHA: MUZIKI NILIFUATA MKUMBO, NAJUTA
Posted by
Teacher Hawa
at
1:52 PM
STAA wa filamu Bongo, Salma Jabu ‘Nisha’ amesema kuwa katika maisha yake hakuwahi kufikiria kujihusisha na masuala ya muziki, isipokuwa aliingia katika fani hiyo kwa kufuata mkumbo.
Akipiga stori na paparazi wetu, Nisha alisema imekuwa ni aibu kubwa kujikita kwenye fani hiyo na kukaa kimya kwa kipindi kirefu kwa kuwa hana mapenzi ya dhati na fani hiyo kama ilivyo kwenye filamu.
“Niliona waigizaji wanaingia kuimba na mimi nikaingia, nilivamia fani tu ndiyo maana najuta, nimeamua nikae chonjo kwanza na mambo hayo nijikite zangu kwenye filamu,” alisema Nisha.
Akipiga stori na paparazi wetu, Nisha alisema imekuwa ni aibu kubwa kujikita kwenye fani hiyo na kukaa kimya kwa kipindi kirefu kwa kuwa hana mapenzi ya dhati na fani hiyo kama ilivyo kwenye filamu.
“Niliona waigizaji wanaingia kuimba na mimi nikaingia, nilivamia fani tu ndiyo maana najuta, nimeamua nikae chonjo kwanza na mambo hayo nijikite zangu kwenye filamu,” alisema Nisha.
Subscribe to:
Posts (Atom)
































