Tuesday, November 5, 2013

Baby Madaha akanusha kutoa rushwa ya ngono kwa bosi wake wa Candy n Candy



Msanii wa label ya Candy n Candy Baby Joseph Madaha amekanusha uvumi uliovumishwa na wanamuziki wenzake wa labe hiyo kuwa ana uhusiano wa kimapenzi na CEO, Joe Kariuki.
 
Uvumi huo ulianzishwa na baadhi ya wasanii wengine, wa label hiyo wanaodai kuwa tangu Baby Madaha asainishwe Candy n Candy maisha yake yamebadilika na kwamba amekuwa akipendelewa zaidi.
 
Akizungumza   Bongo5  jana , Baby amesema CEO wa Candy N Candy, Joe Kariuki alishauriwa na wadau kwamba amwendeleze yeye na akifanikiwa awasaidie na wenzake.
 
“Joe amesikia na hajapenda hili swala kwasababu sisi tupo kizazi zaidi kwasababu mimi najituma kufanya kazi ya muziki ambayo imenipeleka Candy n Candy na sio mambo mengine kama wanayosema wao. 

"Huu ni wivu ni kwasababu mimi ni msanii mkubwa tayari nimeshatengeneza jina kwenye muziki sema kuna kipindi nilijikita kwenye filamu sana, kwahiyo siwezi lingana nao hata kidogo,” amesema.
 
“Candy n Candy walihitaji mwanadada ambaye ataweza kuongea zaidi ya lugha mmoja kwasasababu ya kufanya muziki kimataifa na kigezo kingine walichokitaka ni huyo mwanamuziki mwanadada kuwa na mwenekano mzuri. 

" Wasanii wote wa Candy n Candy tulipelekwa studio, tukarekodi kila msanii.Wale Four – D ndio walianza kurekodi sasa kukawa na msichana mmoja anatoka kimapenzi na msanii mwezake wakawa wanatukanana na kushikanashikana pamoja na kumsema bosi wao. 

"Baada ya kurekodi bosi akapokea ushauri kutoka kwa wadau kwamba ‘hii kazi ya Four – D ni mbaya kwanini usimwendeleze Baby Madaha halafu baadaye Baby Madaha akawainua wenzake’. 

"Bosi akatuambia ‘sasa ngoja nianze na Baby Madaha nyie wengine mtafuata’ wale Four – D hawakuwa wavumilivu ndio wakaanza kusema maneno mengi,” amefafanua Baby  na  kuongeza
 
“Kiukweli mimi najituma katika kazi, Top C wanataka wafanyiwe kila kitu watafutiwe kila kitu. 

"Kwahiyo mimi naona kama wangenisikiliza mimi kama mimi kwasababu nimepitia kwenye academy ya muziki kwahiyo naulewa muziki, haikuwa na sababu ya kuongeaongea maneno mtaani.

"Mpaka leo Top C anapigiwa simu akafanye video hawajaenda wanasema ana matatizo ya kifamilia, sasa ni bosi gani aache kufanya kazi na watu ambao wako serious amfuate yule aliye bize?"
 
Hata hivyo Baby amesema kwa kuwa Joe ni mwanaume na yeye ni mwanamke endapo wakiwa wapenzi si japo la kushangaza wakikubaliana kufanya hivyo.
 
“Haya ni mafanikio yangu ndio maana wanaongea,leo nimezindua bag na perfumes wana wivu, kwani Joe si yupo single na mimi nipo hivyo hivyo!! Kwahiyo kama tukikubalina personal ni sisi,muziki ni muziki na mapenzi ni mapenzi. Kwahiyo yote yanawezekana.”

DEAR READER LEAVE A COMMENT BELOW

SHARE THIS POSTS TO YOUR FRIENDS BELOW==>>

DONT HESITATE TO JOIN OUR FACEBOOK PAGE BELOW FOR MORE BREAKING AND HOT RESEARCHED NEWS

0 comments em “Baby Madaha akanusha kutoa rushwa ya ngono kwa bosi wake wa Candy n Candy”

Post a Comment

 

Mambomseto Copyright © 2011 -- Template created by MAMBOMSETO TEAM -- Powered by MAMBOMSETO

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter