Mbinu chache za kuwaweka waume zenu kiganjani.
Mpe mumeo anachohitaji :
Wanawake wengi wanashindwa kujua wao wanatofautiana na wanaume kwa hisia na hata mawazo ya mapenzi. Wanaume wana mambo wanayoyapenda kutoka kwa wake zao hasa katika masuala ya mapenzi. Kwanza wanawake wajue wanaume wengi wana hisia za haraka za kufanya mapenzi kuliko wanawake.
Mwanaume alivyoumbwa ni kwamba akiona tu mfano mwanamke umevaa kanga moja au umevaa night dress hiyo inatosha kusisimua. Wapo wanawake wanaowasisimua waume zao bila wao kujua. Mfano umevaa tu kanga moja au night dress ndani huna kitu. Kwako ni jambo la kawaida lakini kwa mwanaume sio la kawaida kwa kukuona hivyo tayari unakuwa umeamsha hisia zake. Ukimwona anakuja kutaka haki yake usidhani anakusumbua. Ujue tayari mwenzako alishafiria mbali zamani we huna habari.
Ni vyema ukawa mwangalifu kujua hisia za mwanaume huyo mumeo kama inawezekana mpe anachohitaji kwani usipofanya hivyo unamwathiri kisaikolojia na anaweza kufikiria nje. Wanawake wengi wa nje waliowaweka waume zenu kiganjani hiyo ndio mbinu wanayotumia. Akiwa na ahadi na mumeo atamkuta kanga moja au amevaa night dress na kila anachohiji atapewa haraka tena kwa madoido. Kwanini akitaka hayo hayo kwa mkewe hapewi je ana kosa gani anapofikiria nje?
NB:
Nikisema mpe mumeo Hitaji lake sina maana Umpe mpaka kinyume na maumbile Ukiona Mumeo kafikia hapo Huyo Hafai si Mume mwenye Busara huyo na wala hakutakii mema mkatalie na Umwelimishe madhara ya Tendo la ndoa kinyume na maumbile.
Mvutie mumeo kwa mwenekano wako:
Mvuto ni muhimu sana kwa mwanaume. Wanaume wanapenda wanawake wanaowavutia kihisia. Niwaambie wanawake mlioolewa jueni kumvalia mumeo mavazi yanayomvutia.
Sio vibaya kama nilivyosema hapo juu ukavaa kanga moja kama upo pamoja nae. Kama nilivyoeleza hapo juu mwanaume anasisimka kwa kuona. Kwanini avaliwe kanga moja na wanawake wa nje wakati wewe unaweza kuvaa.
Wanawake jueni hili mnapokuwa karibu na waume zenu jianchieni Kwa mfano hakuna ubaya wakati mumeo karudi kutoka kazini akiwa amechoka, wakati unampotengea chakula ukavaa kanga moja au night dress. Unaweza kuona hilo ni jambo dogo lakini kisaikolojia utakuwa umefanya jambo kubwa. Hapo hata kama atakuwa ameudhiwa kazini atasahau na kukuona wewe mpenzi wake.
Usafi panga vitu vyako vya chumbani vizuri:
Jambo hili limekuwa lizizungumzwa sana hadi wengine wanasema mwanamke usafi. Kisaikolojia mpangalio wa vitu ndani na hasa chumbani kama ni mbovu unaweza kuathiri hata tendo la ndoa. Kama chumba ni kichafu vitu havijapangwa vizuri kisaikolojia kunapunguza msisimko wa mapenzi na hata kumfanya mwenzako achukie kufanya na wewe tendo hilo ukadhani hakupendi.
Mwanamke tandika kitanda chako vizuri panga chumba chako tandika shuka nzuri. Siku hizi kuna shuka zina maneno ya mapenzi nunua hiyo uwe unatandika. Kisaikolojia utamfanya mpenzi wako avutiwe chumba chako na hata wewe mwenyewe. Mazingira mazuri yatamfanya asisimke haraka kimapenzi anapokuwa na wewe na hata kuitamana nyumba yake na kurudi mapema nyumbani.
Jinsi chumba kilivyo rafu ndiyo wanasakolojia wanasema kunafanya ubongo uwe rafu hata kuchukia. Unaweza kumwona mwenzako anachukia kumbe ni kutokana na mpangilio mbovu wa chumba ndio sababu inayomfanya achukie.
Uwe msafi wa mwili:
Sio usafi wa chumba pekee unatosha pia na usafi wa mwili wako ni muhimu. Niwakumbushe wanawake hakuna kitu kinachowachukiza wanaume kama mwanamke mchafu. Asiyejipenda. Sio lazima ujirembe sana lakini jitahidi ukawa msafi. Oga vizuri paka mafuta au lotion yako jipulizie manukato kidogo yanayomvutia mumeo. Sio lazima utumie gharama kubwa usafi wa kawaida unatosha na kupaka rotion kuna fanya ngozi ya mwanamke ikawa laini inayovutia wanaume wanapenda sana wanawake wenye ngozi laini yenye kuvutia inaleta msisimko mumeo anapokuwa anakuangalia mara kwa mara.
Wanawake wa nje hawana zaidi ya hayo ni hayo hapo juu na mengine ndiyo wanayotumia kuwaweka waume zenu kiganjani. Usijaribu kwenda kwa mganga hakuna atakachokusaidia memeo atatoka kama wewe humsisimui, hupangi vitu vyako vizuri na pia kama unaendekeza uchafu ni rahisi mumeo kufikiria nje.
Kujiamini kwako iwe ni kwa sababu unajua ‘kumhendo’ mumeo kwa kumpa mapenzi ya kiwango cha juu, kumheshimu, mjali na kumpatia mambo ya msingi ambayo anastahili kuyapata kutoka kwako. Ukifanya hivyo utaifanya roho yake imsute kila anapotaka kukusaliti.
Hiyo ndiyo iwe sababu ya wewe kujiamini na wala huna sababu ya kujinadi kwa wenzako. Tambua kuwa kuna wanaofikia hatua ya kuhatarisha maisha yao kwa kutoa ‘mtandao’ wakijua kuwa ni njia ya kuwashika waume zao kumbe wanajitafutia matatizo makubwa.
Wapo waliopoteza fedha zao nyingi kwa kwenda kwa waganga ili waume zao wasifurukute mbele zao lakini imekuwa kazi bure. Shituka leo, anza kutumia mbinu sahihi za kuishikilia ndoa yako na usijidanganye kwa kufanya mambo ambayo ni sawa na kutwanga maji kwenye kinu.
Mwanamke aliyekamilika ni yule anayeuthamini mwili wake, sasa kwa nini leo hii ukubali ‘kumrukisha ukuta’ mumeo ili kumfanya asiende nje? Kwa nini utumie fedha zako kwenye kumtafutia limbwata mumeo wakati wewe mwenyewe ni limbwata tosha?
DEAR READER LEAVE A COMMENT BELOW
SHARE THIS POSTS TO YOUR FRIENDS BELOW==>>
DONT HESITATE TO JOIN OUR FACEBOOK PAGE BELOW FOR MORE BREAKING AND HOT RESEARCHED NEWS