Masogange na mwenzake, Melisa Edward walikamatwa nchini Afrika Kusini Julai 5, mwaka huu wakidhaniwa kuwa na madawa haramu ya kulevya na baadaye mahakama kuu ya nchini humo ikawaachia kwa dhamana ikidai unga waliokutwa nao si madawa ya kulevya bali ni mali ghafi zijulikanazo kama Methamphetamine.
Pamoja na wadau wengi kuonesha kukerwa na picha hizo, Masogange hakujali, aliwajibu kuwa kama hawataki kuziona picha hizo wamuondoe kwenye listi ya marafiki mtandaoni humo kwani siyo lazima.
“Hii ni akaunti yangu, nina uhuru wa kuweka picha za aina yoyote. Kama mtu anaona nimemkera basi ‘aniblok’ maana hapa nimevaa mavazi ya kuogelea sasa mlitaka nivae pensi niogelee nayo? Simuogopi mtu…,” aliandika Masogange.
DEAR READER LEAVE A COMMENT BELOW
SHARE THIS POSTS TO YOUR FRIENDS BELOW==>>
DONT HESITATE TO JOIN OUR FACEBOOK PAGE BELOW FOR MORE BREAKING AND HOT RESEARCHED NEWS