Thursday, November 7, 2013

BONGO DA ES SALAAM YA DUDE ILIPIGWA MARUFUKU NA POLISI KWA MADAI KUWA UNAFUNDISHA UTAPELI

Kipindi cha TV cha Bongo Dar es Salaam ambapo ndani yake huigiza Dude, kilizuiliwa kuoneshwa kwenye TV na polisi waliodai kuwa kinafundisha watu kuwa matapeli, imebainika.
  

Taarifa hiyo imetolewa na mwanzilishi na mmiliki wa kipindi hicho kilichokuwa kikioneshwa TBC1, Mrisho Mpoto.
“Ilifika wakati polisi walitutumia barua na wakisema kuwa ‘kwanini Dude Hakamatwi? Kila siku tunamuona anawatoka polisi,tunataka hkamatwekwasababu mnalidhalilisha jeshi la polisi kama limeshindwa kufanya kazi’.

Huku wengine wakisema tunafundisha watu mbinu za utapeli,wengine wakisema kipindi kizuri na kinaelimIsha watu ambao wanaingia Dar es Salaam. Basi kwasababu walitupiga stop tukaona ngoja tutafute mbinu nyingine,” Mrisho alisema.
Katika hatua nyingine, Mpoto amesema kwasasa hawezi kukiendesha tena kipindi hicho na hivyo atamuachia mikoba Dude, ambaye ni muigizaji mkuu. Amesema sasa hivi anajishughulisha na mambo ya muziki na pamoja na kuendesha makampuni yake yanayomwingizia fedha nyingi zaidi.
“Kipindi cha Bongo Dar es salaam ni cha kwangu. Mimi ndio producer na Dude alikuwa kama partner, kwasababu alikuwa ni mhusika mkuu. Kwahiyo hata kama nikaamua kukirudisha naweza nikaenda kurenew kibali nikaendelea kuproduce kwasababu mimi ndio nimekisajili,” amesema Mpoto.
Mpoto amesema alisikia taarIfa kuwa Dude alitaka kwenda kukiuza kipindi hicho M-Net bila kumtaarifu lakini aligonga mwamba kwakuwa hati za umiliki walizozihitaji anazo yeye.
“Namwachia Dude kiwe cha kwake kwasababu yeye ni mwigizaji na mimi nafanya shughuli tofauti na hizo. 

Ingawa makaratasi ya usajili yote ninayo kama akiyahitaji nitampatia kwasababu nimesikia kwamba anashindwa kufanya mambo ya kukiendeleza kipindi kwasababu hana hati ya umiliki wa kipindi. Ili ni tatizo la Watanzania wengi kushindwa kusema ukweli wa mambo. Nasikia Dude alienda, M-Net kwenda kuuza vipindi,ila ikashindika kwasababu walihitaji document za umiliki na document zote ninazo mimi.”

Imeandikwa na: BONGO5.com

DEAR READER LEAVE A COMMENT BELOW

SHARE THIS POSTS TO YOUR FRIENDS BELOW==>>

DONT HESITATE TO JOIN OUR FACEBOOK PAGE BELOW FOR MORE BREAKING AND HOT RESEARCHED NEWS

0 comments em “BONGO DA ES SALAAM YA DUDE ILIPIGWA MARUFUKU NA POLISI KWA MADAI KUWA UNAFUNDISHA UTAPELI”

Post a Comment

 

Mambomseto Copyright © 2011 -- Template created by MAMBOMSETO TEAM -- Powered by MAMBOMSETO

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter