Mwanafunzi aliyekuwa akisoma shule ya sekondari Sabasaba mjini Iringa akijiandaa kurudia kufanya mtihani wa taifa wa kidato cha nne kupitia kituo cha Krelluu mjini Iringa Khamis Mkundo mkazi wa Mwangata C katika manispaa ya Iringa amejiua kwa kujinyonga kwa kamba kwa kile alichodai kuchoshwa na kufeli mara kwa mara mtihani wa kidato cha nne.
Katika barua yake ndefu aliyoiandika kijana huyo amesema kuwa amefanya hivyo si kwa kujipendea ila amechukizwa na hatua yake ya kufeli mara kwa mara hivyo kuamua kujiua ili kuepuka aibu katika mtihani ujao ambao anaamini angefeli.
Shemeji wa kijana huyo Aden Tagalile ameueleza mtandao matukiodaima.com kuwa tukio hilo limetokea mida ya saa 12 na saa 1 usiku wa leo baada ya kuwepo kwa mazungumzo ya muda mrefu kwa kijana huyo kuonyesha kuchukia hatua yake ya kuendelea kuristi mtihani wa kidato cha nne bila mafanikio.
Kijana huyo alisema hajapenda kuona anaendelea kufeli na kuwa yupo tayari kwa lolote kukwepa aibu ambayo ipo mbele yake.
Hata hivyo kufuatia mazungumzo hayo, kijana huyo aliagana na ndugu zake akiwemo kaka yake anayeishi nae kwa kila mmoja kuondoka nyumbani hapo kabla ya kijana huyo kukutwa amejinyonga.
Mwenyekiti wa serikali ya mtaa huo Sarehe Mgimwa amethibitisha kutokea kwa kifo hicho na kuonyesha ujumbe ambao kijana huyo ameuacha .
-Matukiodaima .com
DEAR READER LEAVE A COMMENT BELOW
SHARE THIS POSTS TO YOUR FRIENDS BELOW==>>
DONT HESITATE TO JOIN OUR FACEBOOK PAGE BELOW FOR MORE BREAKING AND HOT RESEARCHED NEWS