Showing posts with label BONGO MOVIE. Show all posts
Showing posts with label BONGO MOVIE. Show all posts
Friday, November 8, 2013
HII NDIO VIDEO ILIYOMPONZA SHILOLE KWENYE MITANDAO YA KIJAMII...!! BOFYA HAPA KUITAZAMA..
Posted by
Teacher Hawa
at
10:54 PM
SHILOLE AAMBULIA MATUSI MARA MAADA YA KUANDIKA KIINGEREZA CHA UGOKO MTANDAONI......!!!
Posted by
Teacher Hawa
at
9:03 AM
Shilole aliamua kutandika yai kwenye Instagram, ili kuzipa uzito shukrani zake za dhati kwa muongozaji wa video yake ya ‘Nakomaa na Jiji’ itakayotoka Jumamosi hii, Nisher.
Bahati mbaya, yai lake lilivunjika mapema wakati lilipokuwa likiufikisha ujumbe huo na kuwafanya watu waligeuzie mjadala.
Kama tumekuacha kwa lugha hiyo, ni kwamba Shilole aliandika Kiingereza kilichokosewa sarufi aka Broken English.
Shilole aliandika: I did ever think I would do a nice video like this thank you alot to my director @nisherbybee.
Baada ya hapo, haya ndio yaliyosemwa:
[ @ ] nicrac1914 Lugha za majahazi!! Ongea Kiswahili tu utaeleweka vzr
[ @ ] lisammbando Speaking English is not a joke Hahahahah
[ @ ] clararobinso Me cjaelewa hiyo lugha mpz, kwan ulitaka kuandika nn hapo?
[ @ ] pinnadelicious Jmn mbona mnapenda kumcritisize hvo mwenzenu sa amekosea nn nyie mnaojua, duh dis is too much
[ @ ] teddybebe Jaman all in all si mmemuelewa.hata mbuyu ulianza kama mchicha kila kitu kinaitaji mazoezi na usione aibu hata wakikucheka mpenz jitahid tu utaelewa. @shilolekiuno
[ @ ] teddybebe Kumbukeni hata nyie mlitoka huko hata kama mlisoma za kishuaa. Vizur kumsahihisha na sio kumbeza 4h
[ @ ] m_bongo her message sent, delivered, read and understood hicks. By the way english isn't her first language.
[ @ ] tutupahamidu Did or didnt?!!thank you or thanks to my director?!
[ @ ] raqey_unique Yeah her English is not gud but a bet u all understood wat she meant so stop hating
[ @ ] pinnadelicious Kiswahili every one anajua so mdada wawatu anajitahidi awe internationally so km tumeelewa wat she mean mbona hakuna tatizo, sema bongo tumemeza!!!!
[ @ ] eshyleta bora washushuliwe tu, coz baadae wanaleta nyodo za kiswanglish, et kiswahili hawezi baadhi ya maneno, km huwezi kithungu tumia lugha yako ya taifa
[ @ ] makavlive @shilolekiuno mwisho wa ujuaji ni aibu...ona sasa, ungeandika kiswahili isingekua shida, kutaka ung'eng'ee shule yenye hujaenda...acha kuiga paka la baa wee ongea kinyamwezi unachokijua!
[ @ ] auma_bebe we al knw dat english iz not our mothertongue n tz nxma mnaijua histry yke shilole ss y mnamponda hvyo bdala hta ya kumrekebisha? sio fair bna...
Thursday, November 7, 2013
KIINGEREZA CHAMPONZA SHILOLE..HAYA NDIYO YALIOMKUTA...SOMA ZAIDI
Posted by
Teacher Hawa
at
11:43 PM

HIZI NI Screenshot Baadhi..
DAH,KINGEREZA HAPANA CHEZE WEWE....
SCENES ZA KIMAPENZI ZAMUWEKA RAYUU KATIKA WAKATI MGUMU....SOMA ZAIDI HAPA
Posted by
Teacher Hawa
at
9:07 AM
Rayuu ambaye ni actress wa Swahiliwood amesema kuwa moja ya mambo ambayo huwa yanamuweka katika wakati mgumu anapokuwa katika kazi zake za filamu ni kuigiza scene za
mapenzi na wakati mwingine humlazimu kuonja ulabu kidogo ili aende sawa. Akizungumza na
Swahiliworldplanet Rayuu alisema "dah scenes za mapenzi me zinaniweka kwenye wakati mgumu, kama jana nimeshikwa tako yaani limeminywa dah ilibidi ninywe kwa maana Cyril Kamikaze alifanya yake"
Filamu hiyo mpya ambayo yupo na Cyril Kamikaze ambaye ni mwanamuziki wa Bongofleva inaitwa Kivuli Cha Binadamu. Rayuu pia anakuja na filamu ya Chicken Head akiwa na Vicent Kigosi(Ray), Skyner Ally na Walter De Ngonde.

Wednesday, November 6, 2013
HIVI NDIVYO JACKLINE WOLPER ALIVYODHALILISHWA FACEBOOK...!! AOMBA MASHABIKI WAWE NA HURUMA...
Posted by
Teacher Hawa
at
11:44 PM
Akionyesha kusikitishwa na kile kinachoendelea facebook, leo hii muigizaji bongo movie,Jackline Walper ameanika maongezi yaliyokuwa yakiendelea katika akaunti ya Walper fake kupitia facebook ikionyesha chati iliyoonekana Walper akiomba sh 20,000 kwa ajili ya kununua umeme mara baada ya kukatiwa na umeme huku akifanya kazi zake kwenye computer.Tazama hapa chini..

Walper aliweka maongezi hayo yakiambatana na maneno haya kwa chini
wolpergambemashabiki zangu haya ndo mambo ya fc bk dah hvii kweli ndo wanavyonidhalilisha plz nisaidien ata kuamdika huko kwa fc bk zenu situmii jina lolote zaidi ta wolper gambe real .siyoo vzuri jamani muwe na roho ya huruma kdogo dah
djfetty.blogspot.com
JE UNAJUA KWANINI WAIGIZAJI WA BONGO HUIGIZA MUVI MAPENZI SANA....!!SOMA HAPA REY AKUJUZE..
Posted by
Teacher Hawa
at
8:48 PM
STAA wa filamu za Kibongo, Vincent Kigosi ‘Ray’ ameeleza chanzo cha wasanii Bongo kuigiza mapenzi kwenye filamu ni kwa sababu Tanzania hakuna uhuru wa kuigiza.
Akizungumza hivi karibuni jijini Dar, Ray alisema msanii anapoonesha kipaji chake kwa kuigiza kitu kwa ajili ya kuelimisha jamii anarudishwa nyuma kwani wakati mwingine inafikia hatua ya filamu husika kufungiwa.
“Hapa Tanzania hakuna uhuru wa kuigiza kama zilivyo nchi nyingine ndiyo maana kila siku tunaigiza mapenzi tu. Niliwahi kutoa filamu ya Second Wife (Mke wa Pili), Waislam hawakunielewa mpaka baadaye. Juzikati nilitaka kutoa filamu ya Sista Maria, Wakatoliki wameipinga isitoke, sasa nini kimebaki, ni kuigiza filamu za mapenzi tu,” aliema Ray.
PICHA: MASOGANGE APIGA PICHA ZA NUSU UTUPU....
Posted by
Teacher Hawa
at
8:16 PM
Masogange na mwenzake, Melisa Edward walikamatwa nchini Afrika Kusini Julai 5, mwaka huu wakidhaniwa kuwa na madawa haramu ya kulevya na baadaye mahakama kuu ya nchini humo ikawaachia kwa dhamana ikidai unga waliokutwa nao si madawa ya kulevya bali ni mali ghafi zijulikanazo kama Methamphetamine.
Pamoja na wadau wengi kuonesha kukerwa na picha hizo, Masogange hakujali, aliwajibu kuwa kama hawataki kuziona picha hizo wamuondoe kwenye listi ya marafiki mtandaoni humo kwani siyo lazima.
“Hii ni akaunti yangu, nina uhuru wa kuweka picha za aina yoyote. Kama mtu anaona nimemkera basi ‘aniblok’ maana hapa nimevaa mavazi ya kuogelea sasa mlitaka nivae pensi niogelee nayo? Simuogopi mtu…,” aliandika Masogange.
JINI KABULA ANYWA SUMU KISA PENZI LA CHUZ....
Posted by
Teacher Hawa
at
8:14 PM
![]() |
| Miriam Nyafulwa Jolwa ‘Jini Kabula’. |
Akizungumza na mwandishi wetu mwanzoni mwa wiki hii, Chuz alisema tukio hilo lilijiri mwaka 2011 nyumbani kwake, Makongo jijini Dar na kwamba siku hiyo hataisahau kutokana na jinsi alivyochanganyikiwa na hali ilivyokuwa.
Aidha, Chuz alisema walikuwa na ugomvi mdogo tu wa kimapenzi jambo ambalo alitarajia kuwa lingeisha kwa amani. Lakini tofauti na matarajio yake, kila dakika iliyokuwa ikiondoka Kabula alizidi kupandisha mori kama si maruhani.
Alisema muda mfupi baadaye, Jini Kabula alivunja vioo vya gari lake kwa kutumia mawe kitendo kilichompa sababu Chuz kumpeleka polisi (hakutaja jina la kituo).
Hata hivyo, Chuz aliendelea kushusha ‘vesi’ kuwa baada ya siku mbili, Jini Kabula alitolewa kwa dhamana huku yeye akidhani kuwa yameisha lakini Kabula aliendeleza ‘libeneke’ ambapo alifika nyumbani kwake na kujifungia ndani kisha akanywa dawa ambazo zilidaiwa kuwa ni sumu kali.
“Nilipokuta mlango umefungwa nilianza kubisha hodi bila mafanikio. Niliamua kwenda polisi, wakaja na kuvunja mlango na kumkuta akiwa amelala chali huku akiwa anatokwa na povu jingi kinywani,” alisema Chuz.
Baadaye walimpa huduma ya kwanza kabla ya kumkimbiza hospitali (jina tunalo) kwa matibabu zaidi. Hata hivyo, baada ya kutibiwa, Chuz aliomba yaishe kwa amani.
“Kaka sitaisahau siku hiyo, ilikuwa mbaya sana kwangu. Jini Kabula alikuwa kabadilika kabisa, alidhamiria kujiua kweli.
“Nashukuru hamkupata habari hiyo lakini ilinichanganya sana,” alisema Chuz.
Mwandishi alimtafuta Jini Kabula kwa njia ya simu ili kuthibitisha juu ya habari hizo ambapo baada ya kusomewa madai hayo alianza kwa kucheka na kujibu:
“Duh! Wewe ni kiboko, umezipata wapi hizo habari? Lakini sipendi kuzungumzia mambo ya zamani, muulize vizuri aliyekwambia.”
Tuesday, November 5, 2013
Lulu akanusha kuchumbiwa, asema kuolewa kupo tu, lakini yeye bado mdogo sana
Posted by
Teacher Hawa
at
11:25 PM
Muigizaji wa filamu nchini Elizabeth Michael aka Lulu amekanusha fununu zilizoandikwa kwenye gazeti la udaku liitwalo ‘Filamu’ kwamba amechumbiwa na muda mchache ataolewa.
Akizunguza jana kwennye kipindi cha XXL cha Clouds FM, muigizaji huyo wa Foolish Age, alisema hajachumbiwa na mtu yeyote ila ni magazeti ya udaku tu ndio yamekuwa yakiandika kile yanachojisikia.
“Mimi sijachumbiwa na hakuna mtu yeyote aliyenichumbia na kama itatokea siku nikachumbiwa kila mtu atajua, na ni mimi mwenyewe ndiye nitakaesema,” alisema mrembo huyo.
“Lakini sasa sijajua wao wamepata hiyo habari kutoka kwenye chanzo gani, by the way kwaajili kumekuwa na habari kila kukicha kila mtu anayejisikia kuandika anaandika ,anaamka anaandika, anaamka anandika.
"Kwa hiyo leo wameandika nimechumbiwa, kesho wataandika nimeolewa, kwa hiyo inategemea na mood ambayo wao waliamka nayo, kwamba ‘leo Lulu tumchumbie, tumuozeshe, tumuachishe’, I don’t know.
“Kuchumbiwa, kuolewa,kuwa mke ni vitu ambavyo tumeumbiwa binadamu, vipo kama ukiwa mpango wa mwenyezi Mungu nitachumbiwa na nitaolewa.” Lulu
Monday, November 4, 2013
WEMA NA DIAMOND WAMFANYA HUDDAH MONROE KUWA GUMZO MTANDAONI BONGO
Posted by
Teacher Hawa
at
11:32 PM
Hivi majuzi mwanadada Huddah MonroeUchunguzi uliofanya na bongomovies umebaini kuwa mashabiki wengi wa muziki na filamu hapa nchini wanapenda sana mahusiano baina ya wawil hawa (Wema na Diamond
Katika pitapita zetu kwenye mtandao tuliweza kupata kauli hizi za watu mbalimbali wakimsifia Huddah kwa kauli yake hiyo huku wengine wakimuona kama ni shujaa….
“Umenifurahisha sana leo yaan had nime comment!!@huddahmonroe”
mmoja wapo aliandika…
“Kuanzia leo nakupenda bureee....na nakufollow@huddahmonroe”
mwingine aliongezea…
“Nakupenda bureee Huddah we ni shujaa”… mwingine naye aliongezea huku wakidiriki kusema kuwa wawili hawa wakioana basi itakuwa kama siku ya mapumziko ya kitaifa kwao.
Sunday, November 3, 2013
"MNAOSEMA NAMLEA MTOTO WANGU VIBAYA NA KUMFUNDISHA UMALAYA, ZAENI WA KWENU MUWALEE VIZURI..." KAJALA
Posted by
Teacher Hawa
at
1:52 PM
“…nawashangaa sana watu wengine mnajifanya mnajua sana kuongea kuhusu mambo yasiyo wahusu kuna mzazi yoyote anataka mwanae apotee ache mambo ya kishamba unataka mtoto avae dira kwani yeye mtu mzima kama unaona namlea mtoto wangu vibaya niachie mwenyewe zaa wa kwako mlee vizuri…”
Hayo ni maneno ya mwanadada Kajala aliyoyasema leo baada ya fans wake mbalimbali kuanza “kumponda” kuwa anamlea mtoto wake “ndivyo sivyo” hususani suala kumvalisha mtoto wake vinguo vya “wadada wa mjini”
Kajala ambaye mara nyingi anaonekana akiweka picha mbalimbali za mwanaye huyo aitwaye Paula akiwa kwenye mapozi tofauti alizidi kusisitiza kuwa mtoto huyo ni wake na ambaye hapendi anachofanya basi atafute wake.
Kauli yake hiyo ilipokewa kwa hisia tofauti na mashabiki wake ambao baadhi yao walisema yafuatayo kumsapoti….
“…tena wakukome ma sis wanajua uchungu wako ulioubeba au au wanajua umemkuzaje mpaka kufika ... nyamafu hao wakosa akili wana low life yamaisha they av got nothing better to do Wa africa uwa tunamatatizo dunia nzima mtoto wa mwenzio anakuhusu nini ukse umuongelee kweli Education kitu kuzuri ukisoma unafikilia utaongelea kiumbe we kazi. Acheni ujinga na utumwa business za wenzenu zinakuwa zenu.. thats ma bby paullet right there and am proud she is a grown gal hun.. kay ma mdogo never give a Fuck life is unbilivable!!!! Family first...”
“Umeambiwa kistaarabu tu hako nguo ckazur kwa umri wake ukizingatia unamtoto mrembo hebu uwe unamvalisha vzr sio nguo zakumfanya wanaume waanze kumtaman…”
Friday, November 1, 2013
HUKUMU YA MASOGANGE YAPINGWA KWASABABU NI NDOGO NA HAIENDANI NA KOSA ALILOLIFANYA....
Posted by
Teacher Hawa
at
11:09 PM
MAKAMANDA wa vitengo vya kudhibiti madawa ya kulevya kwa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wamemaliza kikao chao jana kujadili mustakabali wa uhalifu ikiwemo hukumu iliyotolewa kwa Mtanzania Agness Gerald ‘Masogange’ aliyekamatwa na malighafi haramu aina ya Ephedrine, Julai 5, 2013 nchini Afrika Kusini kwamba ni ndogo.
Taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi Tanzania zimeeleza kuwa makamanda wa nchi hizo 15 walikutana jijini Arusha kuanzia Jumatatu iliyopita lengo kubwa likiwa kutokubaliana na adhabu zinazotolewa na baadhi ya nchi wanachama kwa wanaokutwa na hatia ya kukamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’.
WALICHOJADILI
Kwa mujibu wa chanzo kilicho ndani ambacho kiliomba hifadhi ya jina kwa kuwa si msemaji, makamanda wa nchi hizo walikuwa na kibarua kizito cha kujadili mbinu mbalimbali za kukabiliana na uhalifu pamoja na hukumu inayotolewa kwa watu wanaokutwa na hatia ya kukamatwa na unga.
“Walijadili matukio mengi ya uhalifu likiwemo suala la madawa ya kulevya, wakajadili mbinu za kukomesha biashara hiyo haramu ili waweze kupata suluhisho la kudumu,” kilisema chanzo hicho.
![]() |
| NZOWA |
Ilidaiwa kuwa, malighafi aliyokamatwa nayo Masogange na mwenzake kwa nchi nyingine kifungo chake kinafanana na kile cha mtu aliyekamawa na madawa ya kulevya, lakini kwa Afrika Kusini ni cha chini sana.
Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, miongoni mwa masuala yaliyokuwepo kwenye ajenda ni pamoja na umoja katika suala zima la hukumu hususan kwa watuhumiwa wa madawa ya kulevya kwani kumekuwa hakuna uwiano baina ya nchi moja na nyingine ndani ya Jumuiya hiyo.
“Tumeona ilivyokuwa kwa Masogange, nchi nyingi zimepinga kabisa ile hukumu kwani ilikuwa haifanani na kosa husika. Mtu anatozwa faini ya shilingi milioni nne na laki nane (Sh. milioni 4.8) kitu ambacho hakiingii akilini kabisa, makamanda wengi wameonesha kupinga hukumu ile,” kilisema chanzo hicho.
MASOGANGE AJIFICHA
Wakati makamanda wa nchi hizo wakimaliza kikao chao, habari zenye utata zimesambaa kwamba, Masogange alitua Bongo katikati ya mwezi uliopita lakini anaishi Dar au Mbeya kwao kwa kujificha.

Agness Gerald ‘Masogange’. |
Baadhi ya watu, wakiwemo marafiki zake wamekuwa wakisema kwa mkato staa huyo yupo Dar huku wengine wakisema baada ya kutua Dar alikwenda kwao Mbeya kwa sababu hataki kujulikana kuwa amesharudi Bongo.
Mwenyewe anapopatikana kwenye simu na kuulizwa amekuwa akijibu bado yupo Afrika Kusini lakini siku yoyote atatua Dar.
NZOWA ATOA UFAFANUZI
Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa alipoulizwa kwa njia ya simu juzi kuhusu mkutano huo alijibu kuwa yupo safarini kikazi akiwa katika mazingira mazuri atatoa ufafanuzi.
“Nipo safarini kikazi, naomba unitafute siku nyingine nitakupa ufafanuzi mzuri sana,” alisema Kamanda Nzowa ambaye naye ilidaiwa alikuwepo kwenye kikao hicho.
KUMBUKUMBU
Masogange na Mellisa Edward walikamatwa Julai 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo uliopo Kempton Park jijini Johannesburg nchini humo wakidaiwa kuingiza madawa ya kulevya aina ya Crystal Methamphetamine yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.
Hata hivyo, mahakama kuu nchini humo ilidai madawa hayo si ya kulevya bali ni malighafi haramu iitwayo Ephedrine ambapo kwa sheria za Afrika Kusini mtu akipatikana na hatia ya kuyaingiza nchini humo ni kifungo cha miezi 32 jela au faini ya shilingi milioni 4.8 kama alivyohukumiwa Masogange ambayo ni ndogo.

DIAMOND NUSURA AWEKWE CHINI YA USALAMA WA TAIFA KWA KUVURUGA MSAFARA WA RAIS...
Posted by
Teacher Hawa
at
10:42 PM
STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Alhamisi iliyopita alijikuta akiutibua msafara wa Rais wa Zanzibar, Dk. Mohamed Shein kufuatia kuondoka kwenye msiba wakati ilitangazwa kiongozi huyo ndiye aliyetakiwa kuanza kuondoka.
Ishu hiyo iliyotafsiriwa kama jeuri ya staa huyo ilitokea Mbuzini Mjini Magharibi, Zanzibar baada ya kumalizika kwa mazishi ya baba wa Wema Sepetu, aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania Urusi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Waziri wa Elimu wa zamani katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, marehemu Isaac Abraham Sepetu.
DIAMOND AINGIA
Awali, wakati waombolezaji wamekaa wakiusubiri mwili wa marehemu ufike, ghafla Diamond aliibuka akisindikizwa na kundi la wapambe mpaka alipokaa.
AWEKWA MSTARI WA MBELE
Diamond alipofika aliwekwa mstari wa mbele ambako walikaa ndugu wa karibu na watoto wote wa marehemu.
MC ATANGAZA ITIFAKI YA SERIKALI
Mwili ulipowasili, ratiba ya mazishi ikatangazwa na MC ambapo alitaja utaratibu wa mazishi mpaka watu watakaotakiwa kuweka mashada ya maua kaburini, akiwemo Rais Shein.
Baada ya mazishi, Mwongoza Shughuli ambaye jina halikujulikana aliwaomba watu wote wazingatie itifaki ya usalama wa taifa kwamba ni lazima viongozi wote wa serikali waondoke ndipo waombolezaji wengine watawanyike.
“Jamani naomba sana itifaki izingatiwe, asiondoke mtu yeyote kabla ya viongozi wetu wa serikali, akiwemo Rais Shein hawajaondoka,” alisema MC huyo.
DIAMOND APUUZA, ANYANYUKA
Baada ya MC huyo kutoa mwongozo, watu wote walitulia wakisubiri kiongozi wa kwanza kuondoka ambaye alikuwa ni Rais Shein kama itifaki ilivyotaka.
Lakini kabla Rais Shein hajaanza kusimama, Diamond alinyanyuka na kuzua kasheshe kwa sababu baadhi ya watu, hasa wa umri wake walianza kumkimbilia huku wakikanyagana na kusababisha hali ya taharuki.
MC AWATULIZA WATU
Baada ya watu kuanza kukimbizana hovyo muongozaji wa msiba huo aliwaomba watulie na kusema kuwa wasiogope ila kuna staa ambaye anapita ndiyo maana watu wamemkimbilia.
“Naomba utulivu huyo ni staa f’lani kapita huko ndiyo maana watu wanamkimbilia hivyo tulieni kwanza viongozi wetu waondoke,” alisema.
USALAMA WA TAIFA NUSURA WAMKAMATE
Baada ya kuona watu wakikimbia hovyo baadhi ya maofisa wa usalama wa taifa walitaka kumkamata msanii huyo wakisema alisimama kwa makusudi licha ya kusikia tangazo la kiitifaki.
WATU WAMSHANGAA DIAMOMD
Baadhi ya watu waliohudhuria msiba huo walionekana kushangazwa na kitendo cha Diamond na kusema kuwa ni vyema angesubiri viongozi wote waondoke ndipo na yeye atimke lakini kufanya vile si sahihi.
“Huyu Diamond kwani ana nini? Nakumbuka kwenye msiba wa Kanumba kule Dar pia aliingia kipindi ambacho ilitangazwa kuna kiongozi anakwenda, utaratibu ukatibuka, watu wakawa wanamshangilia yeye,” alisema mtu mmoja aliyetoka Dar kwenda Zanzibar kumzika mzee Sepetu.

UFUSKA NDANI YA BONGO MOVIE....WASANII HULIPWA NA KUHONGWA MAGARI ILI KUTOA "PENZI" BILA KINGA...
Posted by
Teacher Hawa
at
11:34 AM
KINACHOONEKANA kwa sasa Bongo ni ugumu wa serikali kupambana na vita dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi baada ya jamii kushindwa kubadilika na kuona ugonjwa huo ni wa kawaida kama ilivyo kukohoa au kichwa kugonga.Hilo limedhihirika baada ya juzi chanzo chetu cha habari kupasha kwamba, baadhi ya wafanyabiashara na wabunge wameingia ‘kazi’ ya kuwanasa mastaa wa kike Bongo, hasa waigizaji wa filamu. Kwa mujibu wa chanzo hicho, wafanyabiashara maarufu wa jijini Dar na baadhi ya waheshimiwa wabunge wamekuwa wakiwaibukia mastaa wanapokuwa kambini wakirekodi filamu na kuwahonga fedha nyingi sanjari na kuwanunulia magari ya kifahari ya kutembelea.

Chanzo kilisema: “Zamani mapedeshee ndiyo walikuwa wanaongoza kwa kuwachukua mastaa wa kike kwa kutumia picha za mitandaoni na kwenye magazeti, siku hizi mastaa wenyewe wamewashtukia, hawawataki mapedeshee, wanasema fedha zao ni za msimu.
“Siku hizi mastaa wakiwa kambini hupiga picha za hasarahasara na kuzitupia BBM, wafanyabiashara na wabunge wakiziona wanakimbilia kupanga foleni kwenye mahoteli ambayo mastaa hao wamepiga kambi.”
Aidha, chanzo kikasema kuwa baadhi ya wafanyabiashara huhonga kuanzia shilingi 1,000,000 hadi 5,000,000 kama staa ana jina kubwa.
“Kama staa ana jina kubwa, anaweza kuhongwa kuanzia milioni moja hadi tano, kama ni supastaa kama Wema, Wolper, Odama, Rose Ndauka hawa wanaweza kuhongwa hata magari ya kifahari,”kilisema chanzo hicho.

Chanzo kikasema kuwa, mbaya zaidi wanaume hao wamekuwa wakigoma kufanya mapenzi kwa kutumia kinga (kondom) kwa madai kwamba, hawawezi kuhonga pesa nyingi halafu kitandani wakatumia kondom kwani wanakosa raha.
“Kinachouma zaidi ni kwamba, hao wanaume wakiwachukua mastaa hadi chumbani wanakataa kutumia kondom, madai yao pesa wanazohonga ni ndefu (nyingi) kwa hiyo ni afadhali wafaidi, wanasahau kwamba Ukimwi upo.
“Kwa sababu ya tamaa ya pesa, dada zetu (mastaa) wanashindwa kuwa na msimamo wa kutumia kondom. Anaweza kukataa sana, lakini mheshimiwa anaahidi kumnunulia gari, hapo ndipo masharti yanalegezwa,”kilisema chanzo.
Chanzo kikasema kumekuwa na vilio na kusaga meno kwa baadhi ya mastaa kwani wanaponunuliwa magari, kadi zinakaa kwa wanaume hao, baadaye wanawanyang’anya.
“Mbaya zaidi, wapo mastaa waliwahi kushawishika na kutoa penzi bila kinga kwa ahadi ya kununuliwa gari, waliponunuliwa hawakupewa kadi ya kumiliki, baadaye wakanyang’anywa,” chanzo kilitoboa.
Baadhi ya mastaa waliozungumza na paparazi wetu walikiri kuwepo kwa wanaume wenye tabia hiyo, lakini kila mmoja akasema yeye haijamtokea.
Wolper: “Ni kweli, wapo wanaume wanabembeleza sana kutotumia kondom na kuahidi fedha au gari, lakini kama staa anakubaliana na ombi hilo ni kujiangamiza, Ukimwi unaua. Ila mimi sijawahi kukutana na mwanume wa hivyo, kwanza nilishasema ndani ya gari natembea na kondom.”
Jack wa Chuz: “Wewee, uamuzi wa kufanya hivyo ni wa mtu mwenyewe na umri wangu huu nikubali kufanya mapenzi bila kinga kwa sababu ya gari? Kwani gari kitu gani bwana.”
Nisha: “Mh! Nimewahi kusikia kuna wasanii waliingia kwenye mtego huo na sasa wanajuta maana hawana uhakika na afya zao, kwenda kupima wanaogopa, magari walishanyang’anywa, mimi aku!”
Flora Mvungi: “Mimi siwezi kusema kitu maana nina wangu, kama ni gari au pesa ananipa yeye, pole yao ambao hawajajipanga hadi leo.”
Aidha, chanzo kilisema kuwa, maeneo hatari ya kufanyika kwa michezo hiyo ni hoteli kubwa ambazo wasanii hupiga kambi kwa ajili ya kurekodi filamu.
src utamu specially
Thursday, October 31, 2013
AUNT EZEKIEL APOST PICHA MTANDAONI AKIWA CHUMBANI NA MUMEWE....!!TAZAMA PICHA HAPA
Posted by
Teacher Hawa
at
3:12 PM
STAA kunako tasnia ya filamu Aunt Ezekiel amepost picha za chumbani mtandaoni akiwa amelala kitandani na mumewe Sunday Demonte huku picha moja ikiwa imeandikwa happy birthday 2u my lvly wife,the lv ov ma life! ours is an everlasting.
Aunt amepost picha hizo kupitia mtandao wa instagram akiwa na mumewe huyo huku akiandika Thanx ma lv… Ma Mume akeee.. huku watu wakitoa coment wakimsifia kwa kumtunza mume wake hadi amenenepa tofauti na alivyokuwa mwanzo.
• saphyipsah Wawaaaache mlaleeeeeeeeeeee 2d
• lin_libra Shemeji ananenepa.. Hongera kwa matunzo 2d
• fettybihaki Hatareeeee 2d
• 23eclat mnapwndeza 2d
• amandaposhy Hapana chezea..miaka 1000000000 @auntezekiel 2d
• gorgeoucminer Aunty na auncle ake.... 1d
• coplosalum Mpo juu 16h
LULU MICHAEL AMWAGA MATUSI YA NGUONI KATIKA MSIBA WA BABA YAKE WEMA SEPETU..!! SOMA HAPA ALICHOKISEMA..
Posted by
Teacher Hawa
at
6:09 AM
Elizabeth Michael ‘Lulu’.
Tukio hilo lililotawaliwa na hasira lilijiri Oktoba 28, 2013 kwenye msiba huo uliokuwa ukiombolezwa nyumbani kwa marehemu, Sinza-Mori jijini Dar es Salaam.
KISA NA MKASA
Ilikuwa wakati Lulu akitinga msibani hapo, ghafla alimfuata mmoja wa waandishi wa habari hii na kuanza kumporomoshea matusi hayo kwa kile alichodai kukerwa na habari iliyowahi kuandikwa juu ya kitendo chake cha kula chakula sahani tatu katika hafla moja iliyofanyika hivi karibuni huko Kunduchi Beach Hotel, Dar.
TUJIKUMBUSHE KIDOGO
Katika tukio hilo la awali, Lulu alikuwa mmoja wa waalikwa wa harambee ya kuchangia kansa ya matiti kwa akina mama iliyofanyika kwenye hoteli hiyo.
Wakati wa chakula cha mchana kilichoandaliwa kwa ajili ya wachangiaji wote, Lulu alionekana akirudia kuchukua msosi kwa zaidi ya mara tatu (alikula sahani tatu).
TURUDI MSIBANI
Baadhi ya watu waliokuwa msibani hapo walimshangaa Lulu kwa kuporomosha matusi hayo ya nguoni wakati akijua kuwa yeye ni kioo cha jamii na baadhi ya maneno machafu aliyoyatamka hadharani hayaandikiki gazetini.
MSIKILIZE LULU
“Siwapendi nyinyi waandishi hasa wewe (akamtaja jina). ‘I don’t want your f**** story dude, go to hell with you’re f**** shit,” alisikika Lulu akitamka matusi hayo. (hatuwezi kuyatafsiri kwa sababu za kimaadili).
WAOMBOLEZAJI SASA
Mamia ya waombolezaji waliokuwepo eneo la msiba huo walionesha kushangazwa na kitendo cha binti huyo aliyejipatia umaarufu kutokana na kuigiza kwake.
Baadhi yao walidai hali hiyo haikuwa ya kawaida na huenda alikuwa ‘amepata kiburudisho’ (alikunywa pombe).
“Sasa binti si uende ndani ukakae? Hapa ni msibani halafu wewe unasema maneno kama hayo, huoni kama unasumbua akili za wenzako?” mzee mmoja alisikika akisema wakati Lulu anaondoka.

“Unajua hawa mastaa wa Bongo mimi nimeshawajua kwani nawafuatilia sana, wakiandikwa kwa mazuri meno thelathini na mbili nje, wakiandikwa kwa mabaya timbwili kama hili.
“Hiyo habari anayoilalamikia mimi niliiona kwenye gazeti tena ilikuwa na picha sasa alichokereka ni nini, si kweli au?” alisikika mwombolezaji mwingine.
Mwombolezaji mwingine alisema Lulu anaweza kuwa na hoja lakini inakufa kwa vile kama habari ilimkera alipaswa kumtafuta paparazi huyo kwa wakati wake au afike Ofisi za Global badala ya kujianika hadharani huku akidai siku hizi amebadilika.
KWA NINI ALIKEREKA?
Habari zilizopatikana baadaye zilisema kuwa, Lulu alihamaki kumwona mwandishi huyo aliyeandika habari zake hizo za kula sahani tatu, kwani tangu kutoka kwa stori hiyo amekuwa akitaniwa na mastaa wenzake wakimwambia ‘yeye ni mbaya sana kwenye mechi za ugenini’.
Tafsiri hiyo ni kwamba, Lulu amekuwa akila kupitia kiasi kwenye ‘minuso’ (minuso ni vyakula vya bure kwenye shughuli).
AJITENGA NA
BONGO MOVIE
Wakati huohuo, Imelda Mtema anaripoti kuwa, baada ya kufika ndani ya nyumba ya akina Wema, Lulu alionekana kutotaka kujihusisha na baadhi ya wasanii wenzake wa Klabu ya Bongo Movie Unity ambapo alijitenga.
Lulu alijitenga kwa kukaa na mama yake mzazi, Lucresia Karugila na mama mzazi wa marehemu Steven Kanumba, Flora Mtegoa.
Wasanii wa Bongo Movie waliokuwepo ambao hawakupata nafasi ya kupiga stori na Lulu kama zamani ni Jacqueline Wolper, Yobnesh Yusuf ‘Batuli’, Jennifer Kyaka ‘Odama’, Rachel Haule, Kajala Masanja na Eshe Buheti.

Baadhi ya waombolezaji waliokuwemo walinong’ona kuhusu kitendo cha staa huyo kujitenga wakidai kweli sasa amekua.
“Mh! Lulu sasa amekua jamani, naona hataki kabisa ushoga na watu, alipofika akasalimia na kwenda kukaa na wazazi wake, ni maajabu,” alisikika akisema mmoja wa waombolezaji ambaye jina lake halikufahamika.
Mwombolezaji mwingine alisikika akisema kuwa mabadiliko yote yanayoonekana kwa Lulu kwa sasa ni kazi ya mama Kanumba.
TUJIKUMBUSHE
Mzee Isaac Sepetu alifariki dunia Oktoba 28, 2013 katika Hospitali ya TMJ, Dar alikokuwa amelazwa kwa matatizo ya kisukari.
MAZISHI YA MZEE SEPETU
Mwili wa marehemu ulitarajiwa kuzikwa jana saa kumi jioni Mjini Zanzibar baada ya kusafirishwa kutoka jijini Dar es Salaam alikofia.
Mungu ailaze pema peponi roho ya marehemu. Amina.
Imeandikwa na Jelard Lucas na Brighton Masalu na Imelda Mtema.

Source: GPL
Subscribe to:
Posts (Atom)