Mingine na asilimia za maambukizi katika mabano ni Ruvuma (7.2), Shinyanga (7.4), Dar es Salaam (6.9) Rukwa (6.2), Katavi (5.9), Pwani (5.9),Tabora (5.1), Kagera (4.8) na Geita (4.7).
Mikoa mingine aliyoitaja ni Mara (4.5), Mwanza (4.2), Mtwara (4.1), Kilimanjaro (3.8), Kigoma (3.4), Simiyu (3.6), Morogoro (3.8), Singida (3.3), Dodoma (2.9), Manyara (1.5), Lindi (2.9), Tanga (2.4), Unguja (1.9) na Pemba (0.3).
Mziray alisema takwimu hizo zinatokana na utafiti uliofanyika mwaka juzi hadi mwaka jana. Kutokana na matokeo hayo, alisema maambukizi ya Ukimwi yamepungua kwa kasi ndogo.
Alisema Watanzania walioonesha kuwa na ufahamu sahihi wa elimu kuhusu Virusi vya Ukimwi (VVU) na Ukimwi wanafikia asilimia 60 jambo linalosababisha kuwepo mwamko mdogo wa kubadili tabia.
Kuhusu tohara kwa wanaume, alisema inapunguza maambukizi ya Ukimwi kwa asilimia 60 na kusisitiza kuwa ipo haja ya kutoa elimu zaidi juu ya uelewa wa ugonjwa huo.
DEAR READER LEAVE A COMMENT BELOW
SHARE THIS POSTS TO YOUR FRIENDS BELOW==>>
DONT HESITATE TO JOIN OUR FACEBOOK PAGE BELOW FOR MORE BREAKING AND HOT RESEARCHED NEWS