Sunday, October 20, 2013

KIOJA...!! WAZAZI WATOA KALI YA MWAKA KWA KUMUUZA MTOTO WA ILI WAPATE PESA YA KUNUNULIA SIMU..


Kwa mujibu wa ripoti za polisi wa Shanghai, wazazi hao waliotambulika kwa majina ya Mr. Teng na Miss Zhang, walichapisha tangazo kwenye gazeti wakiwa na nia ya kumuuza mtoto wao mwenye umri wa chini ya mwezi mmoja, na muda mfupi baada ya kumuuza mtoto huyo walienda kununua simu aina ya iphone, na kukaa kwenye mtandao (internet).
 Wakiongea na gazeti la Jiefang Daily muda mfupi baada ya kukamatwa, wazazi hao walisema kuwa walikuwa na nia nzuri tu ya kumuuza mtoto wao kwa kuwa wao walikuwa hawawezi kumtunza vizuri kwa hiyo walitaka achukuliwe na familia bora yenye uwezo wa kumpa elimu bora.  
Hata hivyo majirani zao walidai kuwa watu hao walianza kuwachanganya watu kuhusu hali ya ujauzito wa mwanamke huyo kwa kutaka watu waamini kuwa haukuwa ujauzito bali ni uvimbe tu usio na kitu (tumour).
Tukio kama hili la kuipata lilitokea mwaka jana nchini humo ambapo watu saba walifungwa jela katika jimbo la Hunan baada ya kujihusisha na ununuzi wa figo ya kijana mdogo ambae alitumia pesa hizo kununua iPhone na iPad.

DEAR READER LEAVE A COMMENT BELOW

SHARE THIS POSTS TO YOUR FRIENDS BELOW==>>

DONT HESITATE TO JOIN OUR FACEBOOK PAGE BELOW FOR MORE BREAKING AND HOT RESEARCHED NEWS

0 comments em “KIOJA...!! WAZAZI WATOA KALI YA MWAKA KWA KUMUUZA MTOTO WA ILI WAPATE PESA YA KUNUNULIA SIMU..”

Post a Comment

 

Mambomseto Copyright © 2011 -- Template created by MAMBOMSETO TEAM -- Powered by MAMBOMSETO

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter