Mastaa wengi wa dunia wamewahi kuonekana kwenye matukio ya kuwa karibu na stripper ambapo miongoni mwao ni Ne-yo ambae hiki kitendo kiliwahi kumpa lawama nyingi na sio pongezi, hii ni kutokana na picha waliyokua nayo mashabiki juu yake kwamba ni miongoni mwa mastaa wastaarabu wasiotaka sifa ambao huwezi kuwaona wakichezea hela na kuzirusha kwenye mwili wa stripper.
Udogo wake ulifanya mapokezi ya kipaji chake yawe makubwa zaidi… Justine Bieber staa ambae taswira yake kwa watu wengi ilibaki kwamba ni mtoto ambapo fans wake wengi wanatajwa kuwa wa kike na kwa asilimia kubwa ni mabinti wadogo kiumri.
Toka kipindi ameanza kuwa staa, Mcanada huyu mwenye umri wa miaka 19 matukio yake hayakua yenye utofauti sana na picha ambayo wengi walikua nayo kichwani kuhusu yeye akiwa ni staa mdogo anaejua kuvaa kisasa lakini bila kuvuka mipaka na kutoonekana kama mastaa wengine waliolewa sifa.. ila kwa sasa baadhi ya vyombo vya habari vimekua vikimuonyesha na hata kuripoti stori zake za misukosuko ikiwemo kutukana waandishi wa habari na kutaka kuwapiga.
Kwenye tukio ambalo limefanya hii post iwepo hapa ni kuhusu yeye kuonekana kwenye moja kati ya club za usiku ambazo sehemu kubwa ya vinavyopatikana ndani ni pamoja na kina dada maalum kucheza wakiwa na nguo chache au wakati mwingine kutoaa kabisa. (Texas strip club)
Kilichofanya mpaka Bieber aandikwe na TMZ ni pale picha yake ilipopatikana akiwa Texas Strip Club kifua wazi na pia suruali ikiwa chini kabisa na kufanya boxer yake kuonekana kwa sehemu kubwa, aina ya mavazi ambayo hakuwahi kuonekana nayo kipindi hicho.
Mmoja wa hao warembo wanaocheza bila nguo aliandika kwenye page yake ya twitter kwamba ‘Bieber aliyagusa makalio yangu, nimewahi kuwachezea mastaa wengi lakini hakuna hata mmoja amewahi kunigusa makalio kama alivyofanya Bieber, alinishtua sana’
DEAR READER LEAVE A COMMENT BELOW
SHARE THIS POSTS TO YOUR FRIENDS BELOW==>>
DONT HESITATE TO JOIN OUR FACEBOOK PAGE BELOW FOR MORE BREAKING AND HOT RESEARCHED NEWS