Saturday, October 19, 2013

WEMA, DIAMOND, PENNY SINEMA YAENDELEA

Lile sinema la kuzungukana kimalavidavi kati ya malkia wa drama Bongo, Wema Isaac Sepetu ‘Madam’, mfalme wake, Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ na Mtangazaji wa DTV, Penniel Mungilwa ‘Penny’ linaendelea.
Pamoja na kwamba Wema na Diamond wamekuwa wakikataa kuwa hawajarudiana, wakisisitiza kuwa wanarekodi filamu iitwayo Temptation, timu ya Penny imekuwa ikihaha kumsaidia mwanadada huyo kurejesha ‘ushwari’ kwenye penzi la mwanamuziki huyo linalodaiwa kuingiliwa na Wema.
“Unajua washkaji wa Penny wanachokifanya ni kuhakikisha wanatuma maoni mengi mitandaoni kuonesha kuwa Penny ndiye anayefaa zaidi kuwa na Diamond. Yaani ni mwendo wa kumkandia Wema kwa kumpachika majina ya …(tusi),” kilisema chanzo chetu.
Baada ya mbinu hiyo kushindwa kwa kuwa timu ya Wema nayo ipo kazini, Penny alitundika picha mtandaoni ikimuonesha akiwa kwenye pozi la kimahaba na jamaa aliyetajwa kwa jina moja la Raheem.
Miezi kadhaa iliyopita, jamaa huyo alipiga picha ya aina hiyo akiwa kimahaba na Wema hivyo kinachoonekana, Penny naye anajibu mapigo.
Ukifuatilia picha na posti zao katika mtandao wa kijamii wa Instagram, inaaminika kuwa kila anachoposti Wema au Penny ni mwendelezo wa vijembe vinavyorushwa na kila upande kisha kutoa nafasi kwa kundi la mashabiki wa upande mmoja kutukana mwingine.

Hata hivyo, imeelezwa kwamba Wema na Diamond wangeweka mambo hadharani ili kumaliza mzozo unaoendelea wakituhumiwa kumpa mwenzao (Penny) mateso ya moyo huku wakiombwa kutafuta ushawishi kwa umma kwani endapo filamu wanayodai kuwaweka karibu haitatoka, basi watakuwa wamewadanganya mashabiki wao na kupoteza heshima na mvuto.
-GPL

DEAR READER LEAVE A COMMENT BELOW

SHARE THIS POSTS TO YOUR FRIENDS BELOW==>>

DONT HESITATE TO JOIN OUR FACEBOOK PAGE BELOW FOR MORE BREAKING AND HOT RESEARCHED NEWS

2 comments em “WEMA, DIAMOND, PENNY SINEMA YAENDELEA”

  • October 19, 2013 at 1:31 PM

    hawa nao wametuchosha

    delete
  • October 19, 2013 at 1:35 PM
    Anonymous Disse:

    ni kweli kabisa kilacku wao tu cjui hawana kazi za kufanya!!!

    delete

Post a Comment

 

Mambomseto Copyright © 2011 -- Template created by MAMBOMSETO TEAM -- Powered by MAMBOMSETO

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter