MWIGIZAJI wa filamu Bongo, Mayasa Mrisho ‘Maya’ amefunguka kuwa wale waliozusha kuwa amechumbiwa, watasubiri sana kwani suala la ndoa kwake bado halipo leo wala kesho.
Mayasa Mrisho ‘Maya’.
Akipiga stori na paparazi wetu, Maya alisema uvumi ulionenezwa miezi kadhaa iliyopita kuwa amechumbiwa ulikuwa una lengo la kumchafua kwani yeye siku yake ya kuolewa ikifika ataweka hadharani.“Watasubiri sana hao waliozusha suala la mimi kuolewa, sijui hizo taarifa walizitoa wapi. Mimi muda ukifika tu nitawaambia maana wanaonekana wana hamu sana na ndoa yangu,” alisema Maya.
DEAR READER LEAVE A COMMENT BELOW
SHARE THIS POSTS TO YOUR FRIENDS BELOW==>>
DONT HESITATE TO JOIN OUR FACEBOOK PAGE BELOW FOR MORE BREAKING AND HOT RESEARCHED NEWS