Hizi ni Chemba mbili ambazo zimesha jaa na Kupasuka na kusababisha uharibifu mkubwa wa Mazingira na kuhatarisha afya za wakazi wa eneo hili la Umoja street ambapo sasa panaitwa Kinyesi Street.
Majani Haya si kwamba yamekuwa Kijani kuna mvua katika kipindi hiki cha Kiangazi lakini ni kwamba Maji machafu yanayo Churuzika kila wakati ndiyo yamesababisha kuwepo kwa hali hii hatarishi.
Hii ni Chemba ya Maji Taka ambayo kwa msingi kabisa inamwaga maji mengi sana kwa kai ya ajabu pia , mkondo huu ambao sasa umesemwa mpaka wananchi wameamua kunawa mikono na kukubaliana na mtaa wao kuitwa Kinyesi Street.
Hili ni eneo Hatari sana Hapa Chemba imefumuka inamwaga maji utazania ni yanatoka katika chanzo cha mto, hali hii ni hatarishi sana .
Hivi ndivyo haya maji yanavyo anza safari yake ya kuelekea huko yaendako
Mbaya zaidi wakati Chemba moja inatema maji kwa wingi hii ipo Jirani kabisa ambapo ukitazama picha ya kwanza ndipo utaelewa vizuri sana . Chemba hizi ni hatari sana na mpaka sasa zimebadili sura ya Mtaa huo.
Huku Ndiko Maji haya yanapo elekea yametokea katika makazi ya watu na yanaelekea katika Makazi ya watu hasa kwenye mkusanyiko wa watu huku Katika Maghorofa ya Jeshi.
Eneo hili ni Moja ya Chemba ambayo Haijatengenezwa na hakuna mfuniko ipo nyuma ya TRA Mwenge kuna majani haya lakini chini ni Chemba mtu akifanya kosa hapa anazama . Lakini Mamlaka husika inalitambua hili na hakuna anaye fanyia kazi hata kidogo.
Hii ni Chemba ya Pili ambayo nayo inatakiwa kupeleka Maji Baharini ni shimo refu lakini hakuna usalama mfunuiko hakuna hakuna kitu chochote kile.. Miaka inapita Mamlaka husika hakuna anaye hangaika . Hii ni Chemba ya Tatu ambayo nayo ipo eneo hilo hilo nyuma ya Jengo la TRA lakini hakuna anaye hangaika kupashughulikia ikiwa ni pamoja na kuhakikisha kuwa panawekewa Mifuniko
Chemba hizo zimekuwa zikizibuka na kutiririsha maji machafu ya kinyesi na kupita katika makazi ya wananchi wa maeneo hayo jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.
Pamoja na jitihada za viongozi wa mitaa kutoa taarifa kwa wahusika hakuna chochote kilichofanyika hadi leo jambo ambalo linatishia kuwepo kwa magonjwa ya mlipuko kama kipindupindu hasa wakati. Mtdandao huu umekusanya matukio katika picha na video yakionyesha hali ilivyo...endelea kutazama chini ujionee mwenyewe..
Wakazi wa mwenge mtaa wa umoja karibu kabisa na majengo ya jeshi (JKT) wapo hatarini kupata magojwa ya mlipuko kutokana na mkondo wakupitisha maji taka kujaa na kupasuka bila mamlaka husika kushughulikia na hivyo kuwa kero kubwa kwa wananchi wanaoishi katika mazingira hayo.
Mmoja kati ya wananchi wanaoishi katika eneo hilo ambaye hakutaka jina lake kuandikwa, kwa masikitiko makubwa amesema kuwa ni zaidi ya mwezi sasa wamekuwa wakipata adhaa hii ya kujaa na kuziba kwa mikondo ya kupitisha maji taka bila ya wahusika kuzibua angali wanalipa tozo za kila mwezi.

“Hali hii ya kujaa na kuzibuka kwa mikondo ya maji taka imekuwa ikitokea mara kwa mara hasa kipindi cha masika na wakati mwingine wakati wa kiangazi jambo lililopelekea hata mtaa huu kubadilishwa jina na kugeuzwa kuwa ni mtaa wa kinyesi”
Wananchi hao wameituhumu mamlaka husika kwa kutokutambua majukumu yao na hivyo kupelekea wananchi hao kuingia gharama mara kwa mara kwa kwa kuchangishana pesa ili kuzibua wenyewe kwaajili ya kulinda afya zao.
Wananchi hao wanashindwa kuelewa kwanini mamlaka husika inashindwa kutekeleza majukumu yake na kubaki kuchangisha pesa kwa wananchi wakati mamlaka hizo zina mafungu ya fedha kwaajili ya marekebisho ya miundombinu ya maji taka maarufu kama (service charge)

Pamoja na wananchi hao kufanya jitihada za kuwapata watu wa mamlaka ya maji safi na maji taka DAWASCO lakini juhudi zao ziligonga mwamba baada ya kuambia kuwa ni lazima wachangie fedha ya mafuta kwa sababu gari la mamlaka hiyo halina mafuta.
Hofu kubwa ya wananchi wa maeneo hayo ni mvua, hasa katika wakati huu unaoelekea kwenye kipindi cha mvua za masika ambazo zimekuwa na madhara makubwa kwa upande wa magonjwa ya milipuko kama kipindupindu.
DEAR READER LEAVE A COMMENT BELOW
SHARE THIS POSTS TO YOUR FRIENDS BELOW==>>
DONT HESITATE TO JOIN OUR FACEBOOK PAGE BELOW FOR MORE BREAKING AND HOT RESEARCHED NEWS
ndio bongo ilivyo