Monday, October 21, 2013

Nimebakwa na bosi wangu....Naombeni ushauri wenu ili nijue jinsi ya kukabiliana na Aibu hii


Nime vumilia aibu hii lakini nimeshindwa  na hivyo nimeamua niwe  muwazi  ili  niweze  kusaidiwa.Sihitaji  msaada  wa  kifedha, bali  nahitaji  ushauri  tu.

Ndugu zangu mwenzenu juzi   jumamosi nilipatwa na dhahama iliyo pelekea nione aibu kwenda kazini kuendelea na majukumu yangu  baada  ya  kubakwa  na  mama  mke  wa  mtu. 

Ilikua jioni bosi aliponipigia simu nakuhitaji msaada wangu wa kumpeleka katika  sehemu moja ya starehe .

Mimi ni dereva ninaye mwendesha. Nimefanya kazi kwa muda wa miezi sita sasa lakini hakuwahi kunionyesha dalili yoyote ya kimapenzi kwa kuwa anafahamu mimi ni mume wa mtu na yeye ni mke wa mtu.

Mume  wake  siyo  mtu  wa  kushinda  sana  nyumbani.Ni  mfanyabiashara  na  mara  nyingi  huwa  nje  ya  nchi  kibiashara. Nyumba  yao  ina  geti  kubwa  na  mlinzi  mmoja.

Baada  ya  kumpeleka  huko  mapumzikoni, saa tano  usiku  alinipigia  simu  nikamchukue  ili  nimrudishe  nyumbani. Nilimkuta  akiwa  amelewa  sana, hivyo  nikamkokota  mpaka  ndani ya  gari  tukaondoka.

Nyumbani  tulikuta  mwanae  mdogo  na  house girl  wamelala  hivyo  akaniomba  nimpeleke  chumbani  kwake  kwa  madai  kwamba  alikuwa  hawezi  kutembea  kwa  sababu  alizidisha  pombe.

Nilimvuta  mpaka  chumbani  kwake  maana  sikuwa  na  jinsi  ya  kukataa.Cha  ajabu  nilipomfikisha  chumbani yule  mama  alipata  nguvu akafunga  mlango.

Alisimama  pale  mlangoni  na  kuanza  kuvua  nguo  zake.Nilipojaribu  kumvuta  ili  nitoke, yule  mama  alitishia  kupiga  kelele.Akanambia  nitulie  tulale, vinginevyo  atapiga  kelele  kwamba  nataka  kumbaka.

Nikifikiria  getini  kuna  mlinzi  na  nipo  ndani  ya  chumba  cha  bosi wangu  kiasi  kwamba  mlinzi  akija  ni  lazima  aamini  kwamba  nilikuwa  nataka  kumbaka..

Akili  ya  haraka  haraka  ilinituma  nimkubalie  tu, lakini  nikakumbuka  pia  sina  hata  kipande  cha kondom.

Mpekuzi  naomba  niishe  hapo  maana  nashindwa  kuendelea  kuelezea.Kwa  kifupi  ni  kwamba  nilifanya  mapenzi na  yule  mama  bila  kinga  yoyote. 

Mlinzi  alijua  kila  kitu  tulichokifanya  maana  niliondoka  asubuhi.Siwezi  kuendelea  na  kazi  tena  maana  mumewe  akirudi  ni  lazima  aambiwe  kila  kitu..

Kinachoniuma  ni  kwamba  kazi  nimeipoteza  na  huenda  afya yangu nayo  ikawa  imeingia  dosari.Tangu  juzi  sijafanya  mapenzi  na  mke  wangu.Nasubiri  miezi  mitatu  ipite  ili  nikapime. 

Lakini  namwelezaje mke  wangu  kwa  kipindi  chote  hicho  ili  anielewe.Na  mimi  kama  mumewe  naanzaje  kumweleza  kwamba  nimebakwa?  Ndoa  yangu  itakuwaje?

Naomba  msaada  wa  ushauri  toka  kwenu  na  kwa  wasomaji  wenu.

Ni  mimi 
Jose. 

DEAR READER LEAVE A COMMENT BELOW

SHARE THIS POSTS TO YOUR FRIENDS BELOW==>>

DONT HESITATE TO JOIN OUR FACEBOOK PAGE BELOW FOR MORE BREAKING AND HOT RESEARCHED NEWS

0 comments em “Nimebakwa na bosi wangu....Naombeni ushauri wenu ili nijue jinsi ya kukabiliana na Aibu hii”

Post a Comment

 

Mambomseto Copyright © 2011 -- Template created by MAMBOMSETO TEAM -- Powered by MAMBOMSETO

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter