Friday, October 18, 2013

IMEFAHAMIKA JOKATE NA HASHEEM THABIT WALIKUWA WAPENZI KWA MIAKA MITATU KABLA YA KUACHANA

Muigizaji wa filamu, VJ wa Channel O Tanzania, mbunifu wa mavazi na mjasiriamali, Jokate Mwegelo aka Kidoti na mchezaji mrefu zaidi kwenye ligi ya mpira wa kikapu ya Marekani, NBA, Hasheem Thabeet walikuwa kwenye uhusiano wa kimapenzi uliodumu kwa miaka mitatu..

Akizungumza kwenye kipindi cha Amplifaya cha Clouds FM, Jokate alikiri kuwa mara nyingi alikuwa akijitahidi mno kukwepa maswali yanayohusu mahusiano yake hali iliyopelekea uhusiano wake na Hasheem usifahamike kwa watu wengi.

“Hashim Thabeet aka ‘Lulu’ nimedumu naye kwa miaka miwili mpaka mitatu na Diamond nimedumu naye kama siyo mwezi mmoja basi miwili,” alisema.


Jokate alisema baada ya hapo amekaa kwa kipindi cha mwaka mmoja mpaka sasa bila kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mwanaume yoyote hali iliyomfanya awe na uhuru wa kufanya mambo yake bila kusumbuliwa na mwanaume.

DEAR READER LEAVE A COMMENT BELOW

SHARE THIS POSTS TO YOUR FRIENDS BELOW==>>

DONT HESITATE TO JOIN OUR FACEBOOK PAGE BELOW FOR MORE BREAKING AND HOT RESEARCHED NEWS

0 comments em “IMEFAHAMIKA JOKATE NA HASHEEM THABIT WALIKUWA WAPENZI KWA MIAKA MITATU KABLA YA KUACHANA”

Post a Comment

 

Mambomseto Copyright © 2011 -- Template created by MAMBOMSETO TEAM -- Powered by MAMBOMSETO

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter