IMEELEZWA asilimia 25 ya wanawake wanafanya mapenzi kinyume cha maumbile ama na waume zao au na wanaume wengine kama njia ya kukimbia kupata ujauzito na mambo mengine.Takwimu hizo zimetolewa na Katibu wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar kutoka wilaya ya magharibi, Sheikh Nassor Hamad Omar, wakati akiwasilisha ripoti ya awali ya utafiti wa kamati ya kupambana na vitendo vya liwati katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Kusini Unguja Tunguu, kwenye kongamano la vijana kuhusu udhalilishaji wa kijinsia na mimba za mapema.Alisema takwimu hizo zimekusanywa kutokana na utafiti uliofanywa na Jumuiya ya Maimamu (JUMAZA) katika maeneo mbali mbali ya Zanzibar.Alisema sababu ya kufanya hivyo, ama wanawake hao wanaogopa kupata ujauzito hasa wale ambao bado hawajaolewa lakini wako kwenye mahusiano na hata wale walioko kwenye ndoa.Aidha alisema utafiti huo umegundua watoto wengi wenye umri wa kuanzia miaka tisa hadi 20, wanaingizwa katika vitendo viovu ikiwemo liwati na usagaji.Alizitaja sababu kubwa zinazopelekea kuenea kwa uovu huo kuwa ni
pamoja na tamaa, matumizi mabaya ya utandawazi, imani za kishirikina kwa kupiga ngoma kama vile vibuki, kupenda kuiga tabia mbaya na watalii wakorofi.Alisema kutokana na tatizo hilo, kamati yake imefanya utafiti wa tatizo hilo na kutoa elimu kwa taasisi mbalimbali ambapo nyengine zimekubali kushirikiana nao bega kwa bega ili kuondoa tatizo hilo.Alisema Jumuiya imeandaa kitabu ambacho kimeandikwa kwa kuzingatia zaidi misingi ya dini mbili za Kiislamu na Ukiristo.Aidha, alisema wamefanikiwa kuvitembelea vyuo vya Quran na taasisi nyengine na kukutana na walimu, wanafunzi, wazazi na walezi ili kufikisha ujumbe na taarifa za utafiti huo.Akizungumza kwa huzuni kubwa Shekhe huyo alisema inasikitisha kuona vijana wa kizanzibari wanafanya liwati huku wengine wakishangiria na kuchukua picha.Nao vijana walioshiriki kongamano hilo, wakichangia ripoti hiyo, wamekiri kuwa vitendo vya liwati vipo na ni maarufu na vinafanywa kwa wingi hata maeneo ya vijijini. “Vyombo vya habari vinapaswa kutumiwa kikamilifu kutambulisha na kutangaza uchafu huu unaotia doa jamii ya Kizanzibari na taifa letu” alisikika mmoja wa vijana hao akizungumza kwa masikitiko.Washiriki hao walisema kuwa sheria zilizopo sasa zinatoa mwanya kwa wahusika kutotiwa hatiani na kutoa nafasi ya kuendelea kufanya makosa.Walisema serikali kwa asilimia kubwa inapaswa kuwajibika na ni lazima iweke mikakati imara ya kutunga sheria ya kudhibiti suala hilo.Aidha, waliahidi kuvitumia vikundi vyao kuelimisha juu ya mapambano hayo na kwamba watazitumia maskani zao kulizungumzia tatizo hilokwa uwazi.Kongamano kama hilolinatarajiwa kuendelea katika mkoa wa mjini magharibi.
ZanziNews
DEAR READER LEAVE A COMMENT BELOW
SHARE THIS POSTS TO YOUR FRIENDS BELOW==>>
DONT HESITATE TO JOIN OUR FACEBOOK PAGE BELOW FOR MORE BREAKING AND HOT RESEARCHED NEWS