Tuesday, March 25, 2014

Bunge la Kenya lapitisha ndoa ya wake wengi….Mwanaume sasa kuoa hadi wanawake 10..!

Bunge nchini  Kenya limepitisha sheria inayomruhusu mwanaume kuoa wake wengi atakavyo, na halazimiki kumshauri mke wake juu ya uamuzi huo.
Katika marekebisho ya Sheria ya Ndoa ya Kenya yaliyopitishwa Alhamisi iliyopita,ndoa zote zitatakiwa kusajiliwa na umri wa chini  wa mwanamke kuweza kuolewa umewekwa ili kuzuia ndoa za mapema  za watoto, hasa wasichana.
Siku hiyo ya Alhamisi Wabunge wote wanaume, ambao ni wengi, waliunga mkono kuondolewa kwa kipengele katika Sheria hiyo ya Ndoa kilichomtaka mwanaume afanye mashauriano na mkewe kwanza kabla ya kuoa mwanamke mwingine.

Wabunge wanawake walilaani hatua hiyo,  walikuja juu na kususia kikao kwa kutoka nje wakidai Sheria hiyo haiwatendei haki wanawake

DEAR READER LEAVE A COMMENT BELOW

SHARE THIS POSTS TO YOUR FRIENDS BELOW==>>

DONT HESITATE TO JOIN OUR FACEBOOK PAGE BELOW FOR MORE BREAKING AND HOT RESEARCHED NEWS

0 comments em “Bunge la Kenya lapitisha ndoa ya wake wengi….Mwanaume sasa kuoa hadi wanawake 10..!”

Post a Comment

 

Mambomseto Copyright © 2011 -- Template created by MAMBOMSETO TEAM -- Powered by MAMBOMSETO

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter