Tuesday, March 25, 2014

Aibu! Njemba anaswa Akila Uroda na Shemeji yake huko Sinza..!!

AMA kweli mchepuko ni balaa!Jamaa aliyefahamika kwa jina moja la Peter amekiona cha moto baada ya kufanya mchepuko na mke wa rafiki yake bila kufahamu kuwa kufanya hivyo ni hatari kwa maisha yake,Risasi Jumamosi lina kisa na mkasa.
Bwana Peter akijiandaa kuvaa nguo zake kwa aibu mara baada ya kufumaniwa na mke wa mtu.
Kama kawaida, hivi karibuni, Mkuu wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers, akiwa chumba cha habari, alipokea simu kutoka kwa ‘kaka mkubwa’ mmoja aliyeomba hifadhi ya jina na kueleza kuwa alimtilia shaka mke wa kaka yake na yupo njiani na bodaboda akimfuatilia.
Shemeji mtu alidadavua kuwa amekuwa akimtilia shaka shemeji yake huyo kutokana na kawaida yake kutoka nyumbani pale mumewe anapokwenda kazini.
Mke wa mtu akijaribu kujificha baada ya soo hilo.
“Mkuu kaka akitoka tu kwenda kazini naye amekuwa na kawaida ya kuchomoka ‘homu’, nahisi kuna harufu ya usaliti. Nimejaribu kumweleza kaka akaniambia nimfanyie uchunguzi, sasa leo nilibana sehemu nikamsikia akizungumza kwenye simu masuala ya mapenzi hivyo namfuatilia,” alisema jamaa huyo.
Bwana Peter akivaa viwalo vyake kwa aibu mara baada ya kufumaniwa na mke wa mtu.
OFM, baada ya kunyaka taarifa hizo na kuelekezwa kule anakoelekea mwanamke huyo, walikusanya vifaa vyao na kuungana na shemeji mtu huyo katika kumfuatilia dada huyo.
Safari ya dada huyo iliishiia katika gesti moja iliyopo Sinza-Mori, Dar, maeneo ya Meeda Club.
Kwa mujibu wa taarifa za mapokezi, mwanadada huyo alipofika alipitiliza hadi chumbani bila kujua kuwa shemeji yake pamoja na OFM wanamfuatilia hatua kwa hatua.
Aliyeng’amua chumba alichozama ni dereva wa bodaboda ambaye alitumwa atangulie ndani ya gesti hiyo.
Ndani ya dakika sifuri, dereva bodaboda alirudisha majibu kuwa alimuona akizama chumba namba tano.
Dakika kumi baadaye, OFM ilishauri kuripoti polisi na serikali za mtaa ambapo watu hao walifika na kuongozana kisha kuingia kwenye gesti hiyo.
Mtuhumiwa akichukuliwa na afande baada ya fumanizi hilo.
Baada ya kujitambulisha mapokezi na kuonesha vielelezo, waliruhusiwa kwenda kugonga chumba namba tano ambapo jamaa huyo alinaswa laivu akijiandaa kuvunja amri ya sita na mke huyo wa mtu, kumbe yeye alishatangulia chumbani muda mrefu.
Baada ya jamaa kukutwa utupu na mke wa mtu, nusura adondoke kwa presha kwani aliangua kilio kama vile ametangaziwa adhabu ya kifo hasa alipomuona shemeji mtu ambaye kumbe walikuwa wakifahamiana.
Ndani ya chumba hicho kulitokea sekeseke la aina yake ambapo sakata hilo lilitinga katika Kituo cha Polisi cha Kijitonyama, Dar (maarufu Mabatini) kwani shemeji mtu aligoma kulimaliza kiutu uzima kama mfumaniwaji alivyotaka.
Mpaka OFM wanaondoka kituoni hapo usiku mnene, waliwaacha wahusika wakiwa katika kikao kizito cha kuwekeana mambo sawa ili sakata hilo maarufu kama mchepuko liishie hapohapo.

DEAR READER LEAVE A COMMENT BELOW

SHARE THIS POSTS TO YOUR FRIENDS BELOW==>>

DONT HESITATE TO JOIN OUR FACEBOOK PAGE BELOW FOR MORE BREAKING AND HOT RESEARCHED NEWS

0 comments em “Aibu! Njemba anaswa Akila Uroda na Shemeji yake huko Sinza..!!”

Post a Comment

 

Mambomseto Copyright © 2011 -- Template created by MAMBOMSETO TEAM -- Powered by MAMBOMSETO

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter