Wednesday, October 30, 2013

Mtuhumiwa sugu akamata mkoani Simiyu...Silaha 45 za kivita , 17 za kienyeji na risasi 892 zanaswa



OPERESHENI Maalumu ya Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu kukabiliana na vitendo vya Ujambazi, Ujangiri wa uwindaji haramu pamoja na wahamiaji haramu umefanikisha kukamatwa kwa silaha 45, zikiwemo za Kivita na 17 za kienyeji na risasi 892 na magazine 24 huku watuhumiwa sugu wa ujambazi na ujangiri wakitiwa mbaroni.
Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu Salum Msangi.
 
Akizungumza jana na mbele ya waandishi wa Habari ofisini kwake, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Simiyu Salum Msangi alisema kuwa opresheni hiyo ilitokana na kuwepo vitendo vya uhalifu katika Wilaya tano za Mkoa huo na kwenye maeneo ya mbalimbai ya Mapori Tengefu ya Uwindaji kwa kipindi cha mwaka moja tangu kuanzishwa kwake Desemba 2012.
Silaha zilizokamatwa za kisasa na za kienyeji.
 
Kamanda Msangi alieleza kuwa miongoni mwa silaha hizo 45 na magazine 28 zilikamatwa ni pamoja na SMG 7 risasi 763 na G3 moja ikiwa na risasi zake 35 iliyokuwa ikitumiwa na mwanamke mmoja aliyekamatwa Hollo Mabuga (28) mkazi wa Wilayani Bariadi, silaha nyingine 13 zilisalimishwa kwa hiali na baadhi ya watu waliokuwa wakizimiliki kinyume na sharia,Short-Gun saba, Gobole 17 na SAR moja.
Shehena ya risasi zilizo kamatwa.
  
“Tumeweza pia kumkamata mtuhumiwa hatari wa matukio ya uhalifu ambaye hivi karibuni aliachiwa kutoka Gerezani lakini tukapata taarifa za raia wema kuwa amekuwa akijihusisha na ujangiri na ujambazi ambaye ni Masanja Sumuni, tukaweka mtego na kufanikiwa kumkamata akiwa na SMG moja na risasi 96 huku mke wake Hollo Mabuga akikutwa pia na silaha” alisema.
Silaha za zilizotengenezwa kienyeji.
  
Kufatia operesheni hiyo Jeshi hilo pia limefanikiwa kuwakamata wahamiaji haramu wane katika maeneo ya Wilaya ya meatu huku zaidi ya watu kumi waliokuwa wakijihusisha na ujangiri wakikutwa na nyara za serikali ikiwa ni za wanyama waliopo kwenye Hifadhi ya Taifa ya Serengeti na Mapori ya Akiba katika Wilaya za Meatu, Maswa na Itilima.
 
“Tumeunda kikosi kazi ambacho pia kinaendelea na operesheni ya kuwakamata wafugaji na mifugo yao ambao wamekuwa wakichungia mifugo ndani ya eneo la Hifadhi ya Serengeti ambapo zaidi ya ng’ombe wengi walikamatwa na kutozwa faini ambapo zaidi ya shilingi milioni 180 zilipatikana huku watu wanaoendesha vitendo vya ujangiri wakiuwa tembo na wamyama na kuuza kwa wananchi wa maeneo ya jirani” alisema Kamanda.
 
Kamanda Msangi amewataka wananchi kushirikiana na Jeshi la Polisi kutoa taarifa za siri zitakazowawezesha kuwakamata wahalifu na wahamiaji haramu katika maeneo yote ya Wilaya za Meatu, Maswa, Bariadi, Itilima na Busega huku makakati wa kuanzisha vikosi kazi kila tarafa ukiwa mbioni kukamilika ili kuimalisha ulinzi kwa wananchi na mali zao.

source: GSENGO

Kiongozi wa waasi wa M23 ajisalimisha



Kiongozi wa waasi wa M23 Bertrand Bisiimwa ameripotiwa kusalimu amri kwa jeshi la Uganda.
 
Kiongozi huyo wa waasi alivuka na kuingia nchini Uganda kwenye masururu wa magari mawili huku wanajeshi wa Umoja wa Mataifa na wale wa DRC walipofika kilomita tano kuelekea katika kambi yake ya kijeshi
Mwandishi wa BBC Ignatius Bahizi amesema baada ya kuongea na afisaa mmoja wa usalama eneo la Bunagana alimthibitisha kujisalimisha kwa Bisiimwa akisema kuwa anahojiwa na maafisa wa usalama katika eneo la Bunagana katika mpaka wa Uganda na Congo DRC.
 
Waasi wa M23 mnamo siku ya Jumatatu walitoroka maeneo yao ya vita ikiwemo eneo la Rumangabo baada ya kukabiliwa na mashambulizi kutoka kwa jeshi la UN na sasa inaarifiwa wametorokea msituni.
 
Majeshi yanayopambana na waasi hao yamefanikiwa kuwashinda waasi hao katika miji waliyokuwa wameiteka na sasa kuna matumaini kuwa jeshi la DRC linaweza sasa kusitisha harakati za kundi hilo ambazo zilianza miezi 20 iliyopita na ambazo zimewasababisha maelfu ya watu kutoroka makwao wakikimbilia usalama wao.
 
Kundi hilo limekuwa kikiendeshea harakati zao katika mkoa wa Kivu Kaskazini.
 
Mjumbe maalum wa Umoja wa Mataifa aliambia baraza la usalama la umoja wa mataifa siku ya jumanne kuwa waasi wa M23 sio tisho tena na kuwa wameshindwa kijeshi baadhi wakikimbilia msituni kutokana na mashambulizi makali kutoka kwa wanajeshi wa muungano wanaokabiliana na waasi hao.
 
Naye msemaji wa UN nchini Uganda amesema kuwa zaidi ya watu 5,000 wametoroka maeneo ya Bunagana kufutaia mapambano makali kati ya waasi na wanajeshi wa DRC.
 
Lucy Beck wa shirika la kuwahudumia wakimbizi alisema Jumatano kuwa idadi hiyo huenda ikaongezeka hadi 10,000 ifikapo siku ya Alhamisi huku mapambano yakichacha katika mpaka wa Uganda na Congo.

-BBC

"BASATA KUNA KITU WANATAFUTA KUTOKA KWANGU"......NEY WA MITEGO

Siku chache zilizopita mwana Hip Hop kutoka pande za Manzese Nay Wa Mitego alipokea barua kutoka BASATA inayomtaka kubadili aina ya mavazi anayovaa katika show zake (mlegezo/mtepesho) ambayo hayaendani na Tamaduni za kitanzania.
0051
Akizungumza na Bongo5 leo kwa njia ya simu Nay amesema amekuwa akivaa mlegezo kwa kipindi cha miaka ishirini hali ambayo itamwia vigumu kubadilika kutokana ni mtindo ambao ata mashabiki wake wengi wameuzoea.
Nahisi kuna kitu kingine wanakitaka toka kwangu kuhusu muziki wangu ndiyo maana wananitishia kunifungia wakati mimi nafanya muziki kama ndiyo maisha yangu, kwahiyo kubadilika kwa haraka kuvaa mlegezo siwezi labda baada ya miaka 3 ila inategemea”  Alisema Nay.
Aidha  katika mahojiano mengine na kipindi cha Showtime kupitia kituo cha RFA ya Mwanza Nay amesema kuwa Baraza hilo lina majukumu mengi ya kufanya kwaajili ya kuboresha  maslahi ya wasanii badala ya kuhangaika na kumzuia kuvaa mlege ili hali wanaovaa hivyo ni wengi.

Sasa hata baraza la sanaa Tanzania wana shughuli nyingi  sana za kufanya nyingi sana ili sanaa yetu isonge mbele mambo yetu yaani wasanii tuishi maisha mazuri lakini si swala la kufuatilia mlege wa Nay, hapana kuna kitu behind ambacho kinaendelea sijui ni nini  maybe wameamua waanzie hapo ili wastopishe kile ambacho nakifanya.

PICHA 6 ZA FUJO ZILIZOFANYWA NA MASHABIKI WA MBEYA CITY MARA BAADA KUPATA USHINDI WA 2-0 DHIDI YA PRISONS HAPO JANA..!!


Taarifa kutoka 87.8 Mbeya zinaamplfy kwamba mashabiki wa Mbeya City wamelishambulia gari la wachezaji wa Prisons na kumuumiza mchezaji mmoja ambapo pia walivunja vioo vya  gari aina Toyota Coaster na magari mengine yaliyokuwa kwenye msafara wa timu hiyo ikitoka uwanjani baada ya kufungwa na Mbeya City kwa mabao 2-0.

mbeyayetu.blogspot.com wameripoti kwamba Mashabiki hao walilishambulia magari hayo na kuyavunja vioo na baada ya hapo wakakimbilia kusikojulikana.

Mmoja wa maofisa wa Prisons alisema ana uhakika kuwa waliofanya hivyo ni mashabiki wa Mbeya City kwa kuwa walikuwa wamevaa jezi za rangi ya zambarau ambayo huvaliwa na timu hiyo.






Hapa chini ni baadhi ya fans Mbeya City wakiwa wamebeba jenela la timu ya Prisons, chini ya hii picha ni baadhi ya picha wakishangilia magoli uwanjani

Baada ya Kanye West na Kim K, sasa hivi ni zamu ya Ciara na Future

future-ciaraRapper Future na muimbaji Ciara ni wapenzi ambao mapenzi yao ni motomoto hivi sasa na 

wamefungua ukurasa mpya wa mapenzi yao. Baada ya siku chache ambapo wapenzi wa burudani kushuhudia Kanye West akimvalisha pete ya uchumba mama wa mtoto wake Kim Kardashian. Future na Ciara nao wamepitia hatua hiyohiyo.


Baada ya kutoka kwa habari kwamba wawili hawa ni wachumba baada ya Future kumvalisha pete Ciara,bila kusita Cici alijitokeza na pete hiyo in public kwa mara ya kwanza kwenye birthday party yake akitimiza miaka 28. Pete hiyo ya almasi 15 carant ilionekana kwenye kidole cha Ciara akiwa ameshikilia chupa ya Moet kwenye bday part hiyo.


moet

UKATILI! MTOTO WA MIAKA 8 ALAZIMISHWA KUWA HAUSIGELI,MWAJIRI WAKE AMCHANJA NA KISU....


UKATILI! Katika hali ya kusikitisha, mtoto mwenye umri wa miaka 8 aliyejitambulisha kwa jina la Loveness na mwenzake aitwaye Anna, wanadaiwa kulazimishwa kufanya kazi za ndani huku wakipata vipigo vikali kutoka kwa waajiri wao.

Loveness alikuwa akifanyishwa kazi Ubungo-Maziwa na Anna alikuwa Kimara jijini Dar.
Watoto hao wameeleza kazi nzito wanazofanyishwa katika mazingira magumu wakiwa na umri mdogo, wanaohitaji kwenda shule.
“Mama (mwajiri wake) alikuwa akinipiga na wakati mwingine kunichanja na kisu,” alisema Loveness.


Majirani ambao hawakupendezwa na matukio hayo, waliitonya Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers ili kufuatilia suala hilo.
Jirani mmoja ambaye hakutaka kutajwa gazetini, alidai kwamba alikuwa akiumizwa na mwajiri wa Anna ambaye alikuwa akimpa vipigo vikali mtoto huyo ambaye alikuwa akimlea mtoto wa mama huyo kila siku.

“Hakuna kitu kilichokuwa kikituumiza majirani kama mtoto Anna ambaye alikuwa akipata vipigo vikali kila siku iendayo kwa Mungu kutoka kwa mwajiri wake, heri arudi kwao,” alisema.


Mtangazaji wa kipindi cha Wanawake Live kinachotetea haki za watoto na wanawake kupitia EATV, Joyce Kiria alitinga nyumbani kwa waajiri hao na kumkamata mmoja wao kisha  kumpeleka katika Kituo cha Polisi cha Kimara, Dar kwa ajili ya kujibu mashitaka ya kukaa na mtoto mdogo kama mfanyakazi.

Hata hivyo, mtangazaji huyo aliamua kuwachukua watoto hao na kwenda kuishi nao nyumbani kwake Changanyikeni, Dar, kwa ajili ya kufanya utaratibu wa kuwasafirisha vijijini kwao ambapo Loveness anatokea Morogoro na Anna ametokea Singida.
Joyce amekuwa akifanya mawasiliano na familia za watoto hao ili kuwarejesha kwao huku Waziri wa Maendeleo ya Jamii Jinsia na Watoto, Sophia Simba na Waziri wa Kazi na Ajira, Gaudensia Kabaka wakiombwa kuangalia suala hilo la unyanyasaji kwa watoto kwa umakini mkubwa.

SUALA LA WEMA KUTOSHIRIKI MISIBA YA WENZAKE,BONGO MOVIE WAAMUA KUMTENGA KWENYE MSIBA WA BABA YAKE...


KATIKA hali isiyotarajiwa katika wasanii wanaounda kundi la Bongo movie wamejikuta wakijitenga kushiriki msiba wa Baba mzazi wa msanii mwenzao Wema Isack Sepetu, baada ya kuundwa zengwe na mmoja wa watu wenye ushawishi katika kundi hilo, Wema akiongea kwa uzuni amesema kuwa hata wale waliofika jana katika msiba huo hawakufika kwa ajili ya kumfariji bali walifika kwa ajili ya kumsanifu.

FC ilifanya utafiti ili kubaini hilo kwa kuwapigia simu baadhi ya wasanii wanaotoka katika kundi hilo nao bila kusita kwa masharti ya kutotajwa majina walitiririka kwa kusema kuwa ni kweli uongozi wa kundi hilo umetoa agizo watu wasishiriki kutokana na tabia ya msanii huyo kutoshiriki katika misiba ya wasanii wenzake.


“Ni kweli hilo lipo na lina ukweli kwa njia moja au nyingine Wema bwana huwa hashiriki katika misiba ya wasanii wenzake, kuna mtu muhimu sana na ana sauti katika kundi la Bongo Movie amesema kuwa katika misiba iliyotokea ameshiriki misiba miwili tu, wa marehemu Sharo na Kanumba kwa sababu alikuwa mtu wake,”anasema kijana huyo.


Hili si jambo la kulifurahia kwa wasanii kwani halijengi bali linaleta mgawanyiko wa moja kwa moja, msanii mwingine alikiri kuwa Wema anabagua kushiriki misiba kwani wakati amefariki marehemu John Maganga alipigiwa simu ili ashiriki katika msiba lakini alisema yupo Location, hivyo wasanii wenzake wanamtenga ili aone umuhimu wa kushiriki misiba ya wenzake.

Jana jioni nyumbani hakukuwa na wasanii zaidi ya mtangazaji wa kipindi cha Take One Zamaradi Mketema akiwa na Rais wa shirikisho la wasanii Simon Mwakifwamba na waombolezaji wengine, huku baadhi ya wasanii wakifika pale na kuondoka jambo ambalo Wema alilitafsiri kama walifika pale kutoa lawama ili asiwaone kama hawajafika lakini hawakuwa na dhamira ya kweli mioyoni mwao.
 

Mambomseto Copyright © 2011 -- Template created by MAMBOMSETO TEAM -- Powered by MAMBOMSETO

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter