Showing posts with label KITAIFA. Show all posts
Showing posts with label KITAIFA. Show all posts

Monday, March 24, 2014

“Mzigo hapa unaendelea kama kawaida,mimba sio kigezo cha kusubirisha mambo yangu…” Odama

MTOTO mzuri Bongo Movies, Jennifer Kyaka ‘Odama’ amesema japokuwa ni mjamzito lakini bado ana kasi zaidi katika kufanya kazi zake za filamu.

Akipiga stori na paparazi wetu, Odama alisema watu wengi wanaamini unapokuwa mjamzito unaacha shughuli zako lakini kwake mambo ni tofauti, kazi kama kawaida.
odamaJennifer Kyaka ‘Odama’.

“Mimi mzigo hapa naendelea kama kawaida wala mimba siyo kigezo cha kusubirisha  mambo yangu, kwanza naona ndiyo imenipa nguvu ya kufanya kazi zangu, nimekamilisha tayari kazi mpya, naiachia March 28 inaitwa Jicho Langu,” alisema Odama.


Read more: http://mnyetishaji.blogspot.com/2014/03/mzigo-hapa-unaendelea-kama-kawaidamimba_24.html#ixzz2wvacZCML

Sunday, December 22, 2013

PICHA YA KWANZA YA SABABU ILIYOFANYA MAWAZIRI 4 KUONDOLEWA JUZI BUNGENI DODOMA..!! NI UNYAMA WA KUTISHA WALIOFANYIWA WATANZANIA..



Hii ndio moja ya unyama uliofanyika kwenye Operation Tokomeza Ujangili iliyosimamiwa na washiriki toka Wizara 4 za mawaziri waliondolewa juzi bungeni. 


Thursday, November 7, 2013

DAKTARI MBARONI KWA KUMTOA MIMBA BINTI WA MIAKA 17....

Polisi mkoani Kilimanjaro, imemtia mbaroni daktari mstaafu wa Hospitali ya Serikali ya Mkoa ya Mawenzi kwa tuhuma za kumtoa mimba msichana wa miaka 17. 
  


Tukio hilo linadaiwa kutokea juzi, ambapo Dk huyo anayedaiwa kuwa na umri wa miaka 50 (jina tunalo), alikamatwa saa 10:45 alasiri katika nyumba ya mjomba wake iliyopo eneo la Kiboriloni mjini hapa akiwa katika harakati za kufanya tukio hilo.

  
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Robert Boaz aliwaambia wanahabari jana kuwa, uchunguzi umebaini msichana aliyekuwa akitolewa mimba ni mhitimu wa Chuo cha Ualimu Masama Suni.
Kwa mujibu wa Kamanda Boaz, msichana huyo amelazwa katika Hospitali ya Mawenzi akiendelea kupatiwa matibabu baada ya jaribio hilo la kumtoa mimba kuzimwa na polisi kabla halijakamilika.
 
Katika tukio kama hilo, daktari mmoja aliwahi kumsahau mwanafunzi aliyekuwa akimtoa mimba na kwenda kunywa pombe na baadaye mwanafunzi huyo alipoteza maisha. Desemba 20,2012 Polisi lilimtia mbaroni daktari bingwa wa magonjwa ya akina mama pia.



TOA MAONI YAKO HAPA CHINI


Jalada la Sheikh Ponda lasimamisha kesi yake Mkoani Morogoro

 
Kesi yenye mashtaka matatu inayomkabili Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu nchini,Sheikh Ponda Issa Ponda katika Mahakama ya Hakimu Mkazi mkoani Morogoro ,imeshindwa kusikilizwa baada ya jalada halisi la kesi hiyo kuitishwa kwenda Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kwa ajili ya kulipitia upya. 
 
Sheikh Ponda alifikishwa mahakamani hapo mapema asubuhi kwa kutumia usafiri wa basi maalumu la magereza na safari hii kesi yake ilikuwa mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi,Mary Moyo baada ya hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi hiyo tangu awali, Richard Kabate kuhamishiwa mkoani Dodoma.
 
Akitoa maelezo ya kesi hiyo,Hakimu Moyo alisema jalada halisi la kesi hiyo liliitishwa na Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam Oktoba 15, mwaka huu kwa ajili ya mapitio na kwamba Mahakama Kuu inamamlaka ya kisheria ya kuitisha jalada lolote na kuongeza kuwa kesi hiyo haitaweza kusikilizwa hadi jalada hilo litakaporudi.
 
Hakimu Moyo alisema kwa sasa kesi hiyo itakuwa ikitajwa tu na suala la mshtakiwa kuletwa ama kutoletwa mahakamani liko chini ya magereza kwani dhamana ya mshtakiwa huyo imefungwa,hivyo ataendelea kuwapo magereza hadi Novemba 21,mwaka huu kesi hiyo itakapotajwa tena mahakamani hapo.
 
Mapema baada ya kufikishwa mahakamani hapo, Hakimu Moyo alimuuliza Sheikh Ponda kama ana taarifa zozote kuhusu kutokufika kwa mawakili wake watatu mahakamani hapo ambao ni Batholomew Tharimo, Ignas Punge na Juma Nassor hata hivyo, Sheikh Ponda alidai kuwa hana taarifa zozote kuhusu kutofika kwa mawakili wake.
 
Hata hivyo, upande wa mashtaka ukiongozwa na Wakili wa Serikali, Sunday Hiela ulidai uko tayari kutoa ushahidi ambao ungeanza na askari namba F4949 DC Kingazi wa Kituo Kikuu cha Polisi. Hata hivyo, shahidi huyo hakuweza kutoa ushahidi wake kutokana na jalada halisi la kesi hiyo kutokuwapo mahakamani hapo kwa sababu zilizotolewa awali.
 
Pamoja na kutokufika kwa mawakili wote watatu pia idadi ya wafuasi wa Shekh Ponda ilionekana kuwa ndogo.
 
Sheikh Ponda anakabiliwa na mashtaka ya kutokutii amri halali ya mahakama,kutoa maneno yenye nia ya kuharibu imani za dini na kushawishi watu,makosa hayo kwa pamoja anadaiwa kuyatenda Agosti 10, mwaka huu.

MKANDA MZIMA WA MAUAJI YA MFANYAKAZI WA TBC UBUNGO....STERING ALIKUA MWANAMKE.

MAJAMBAZI  wanne wakiongozwa na mwanamke juzi usiku walifunga barabara ya Ubungo Maziwa jijini Dar es Salaam na kupora Sh. 600,000 kwa mfanyabiashara wa duka la vyakula kisha kumua dereva la Shirika la Utangazaji (TBC) na kumjeruhi jirani kwa kumpiga risasi sehemu za makalio. 


Dereva aliyeuawa ametajwa kwa jina la Ramadhani Giza, mkazi wa Gongolamboto na majeruhi alifahamika kwa jina la Mwarami Mshana mkazi wa Ubungo Maziwa. 



Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura. 

Akisimulia tukio hilo, Hamdan Rajabu ambaye aliporwa fedha hizo pamoja na vocha za simu zenye thamani ya Sh. 400,000 alisema majambazi hao walifika mtaani hapo usiku wakiwa na bunduki na moja kwa moja walimfuata dukani na kumuaru awape fedha.
  
Alisema wakati akitoka nje ya duka lake mlangoni alikutana na jambazi moja na kumwamuaru arudi ndani ya duka na kumpa fedha haraka. Aliongeza kuwa baada ya kuambiwa hivyo alishikwa na butwaa na ghafla jambazi huyo alimtolea bastola mbili na bunduki moja iliyokatwa kitako na kumtaka alale chini kifudifudi.
  
Rajabu alisema baada ya kuona hali imekuwa ngumu, alilazimika kutii amri na kulala na kwamba aliambiwa atoe fedha zote za mauzo ya siku hiyo.
  
“Niliambiwa niwape fedha  na wakati huo jambazi mwingine alikuwa ameingia ndani na hivyo kufanya idadi ifikie wawili na niliwaambia wafungue droo na kuchukua chochote watakachokikuta humo na ndipo walipofungua na kukusanya mauzo yote yaliyofikia Shilingi laki sita,” alisema. 
  
Alisema kabla ya kumaliza uporaji huo, waliona gari la TBC alilokuwa akiendesha marehemu ambalo lilikuwa limeegeshwa pembezoni mwa barabara likiwasha taa na kuonyesha dalili za kuondoka ndipo jambazi mwanamke alipomfyatulia risasi na kumuua papo hapo. 

Mashuhuda wa tukio hilo waliongea na paparazi wetu kuwa tukio hilo lilikuwa kama sinema kwa kuwa kila jambazi alikuwa akifanya kazi yake kwa umakini huku madereva waliokuwa wamewabeba majambazi hao wakiwa wamebaki kwenye piki piki bila kuzizima. 

Majeruhi huyo amelazwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na kwamba hali yake inaendelea vizuri. 

 Marehemu alikuwa kwenye gari lenye namba za usajili STK 355 Toyota Land Cruiser mali ya shirika hilo lililokuwa limeegeshwa karibu na eneo la tukio akiwa na mwanamke aliyefahamika kwa jina la Mwanakombo Daud (41), mfanyabiashara na mkazi wa eneo la Ubungo maziwa. 

 Katika  tukio hilo majambazi hayo yalimjeruhi kwenye kiuno Mharami Rajabu (25) ambaye ni dereva wa gari kenye namba za usajili T.404 BLZ Mitsubish Fuso aliyekuwa ameegesha gari eneo hilo la tukio. 

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kinondoni, Camillius Wambura, alisema dereva huyo aliuawa na majambazi wanne ambao walivamia duka la Namanga Shopping Center linalomilikiwa na Hamdan Rajabu (45). 

Wambura alisema majambazi hao walifanikiwa kupora vocha za simu zenye thamani ya Sh. 400,000 na fedha taslimu na kwamba wakati wote wa tukio hilo la uporaji likiendelea  jambazi mwanamke ndiye alikuwa kiongozi wao wa kulinda eneola nje. 

Alisema kufuatia tukio hilo, Polisi wanaendelea  na msako mkali wa kuwasaka wahalifu wanaojihusisha na ujambazi wa kutumia silaha, unyanganyi wa kutumia nguvu, wauzaji wa madawa ya kulevya pamoja na uhalifu mwingine. 

CHANZO: NIPASHE

JIBU LA WAZIRI MKUU BAADA YA KUULIZWA BUNGENI KAMA TANZANIA ITAJITOA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI...SOMA ZAIDI



Serikali imesema licha ya kutokea  mvutano kati yake na nchi za Rwanda, Kenya na Uganda, hadi sasa haijafikia dhamira ya kujitoa kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki na kwamba mgogoro uliopo utamalizwa kidiplomasia kwa lengo la kudumisha uhusiano uliopo.

Leo bungeni  Dodoma, Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesema lengo la Tanzania ambayo ni walengwa wakubwa ni kuona muungano huo unakuwa wenye tija kwa wananchi wa nchi wanachama na si kwa upande mmoja  tu

MAPIGANO YA WAKULIMA NA WAFUGAJI HUKO MVOMERO, 7 WAFA NA 55 WAJERUHIWA VIBAYA..!!

https://blogger.googleusercontent.com/img/b/R29vZ2xl/AVvXsEiBBQAcVAahXqmG8pQTNVgBMtMH-6K5yN91cGn0KPoqAXGmZS7LZHIt6b9jlrmCuG7NSx7njYlh0Qm_J_opHCGn78gFoXV5T_PjsrH0lVY7RdtGlshmywezp-zD0wBuXyEQLG3bFHSpz5I_/s1600/mapigano+moro+still(2).jpg 
MAPIGANO makali yakihusisha silaha za kisasa na jadi yamezuka kati ya wanakijiji wa Hembeti na wafugaji jamii ya Kimasai wilayani Mvomero, Mkoa wa Morogoro na kusababisha vifo vya watu saba huku wengine 55 wakijeruhiwa vibaya.
Kutokana na hali kuzidi kuwa mbaya, taarifa zilizolifikia gazeti hili jana jioni zilisema kuwa Kamanda wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Makao Makuu alilazimika kufika eneo hilo akiwa na kikosi cha askari kujaribu kutuliza fujo hizo licha ya awali jeshi hilo kudaiwa kutoonyesha ushirikiano.
Awali, kwa mujibu wa Diwani wa Kata ya Hembeti, Juma Malaja na Ofisa Mtendaji Kata, Charles Chikuni, waliokufa walikuwa wawili; Yusuph Hamad (30) mkazi wa Mkindo aliyefariki akipata matibabu katika Hospitali ya Bwagala-Turiani na mfugaji ambaye jina lake halikupatikana mara moja.
Majeruhi waliokuwa wametambuliwa ni Hamiss Hussen, Athuman Mtaalam, Kibuyo Nasoro, Mveda William, Francis Laulent na Juma Adam wakazi wa Mkindo, Muya Paulo (Hembeti), Francis William (Dihombo) na Yusuph Hamad aliyefariki akihudumiwa.
Lakini baadaye jioni, hali ilibadilika na watu watano wengine zaidi kuuawa kwa kuchinjwa huku majeruhi nao wakiongezeka kutoka 28 wa awali na kufikia 55.
Gazeti hili lilielezwa kuwa miili hiyo mitano ilihifadhiwa katika kituo cha afya Mvomero huku majeruhi 27 wapya nao wakapatiwa matibabu hapo. Kwamba waliouawa ni wanakijiji wanne na wafugaji wa Kimasai watatu.
Mapema, baadhi ya mashuhuda waliopiga kambi katika ofisi za tarafa na Kituo Kidogo cha Polisi Mvomero na familia zao kwa hofu ya mapigano hayo, walisema vurugu hizo zinachangiwa na rushwa kukithiri kwa viongozi wa serikali kuanzia ngazi ya tarafa, wilaya na mkoa na kupuuza mawazo na mipango ya wananchi juu ya ulinzi wao na mali zao.
Zainabu Joseph na Seleman William ambao wamelazwa hospitali ya Bwagala, walisema tukio hilo lilianza juzi saa 3:00 asubuhi katika Ofisi ya Serikali ya Kijiji na Kata ya Hembeti wakati wafugaji hao wakiwa na silaha za kisasa zaidi ya saba kutaka kuwachukua kwa nguvu ng’ombe kwa kupiga risasi hovyo.
Walisema kuwa ng’ombe hao wapatao 300 walikamatwa jioni ya Oktoba 4 mwaka huu, wakiwa wameharibu chanzo cha maji Mto Dimamba, kingio la maji yanayotumika kwenye vijiji vya kata hiyo na shamba la mahindi  la mtu mmoja ambaye hakufahamika jina lake.
Waliongeza kuwa asubuhi ya Oktoba 5, wafugaji hao walimwagiza mmoja wao kuja kufanya mazungumzo ya suluhu, lakini akiwa kikaoni na viongozi wa kijiji na kata, aliwasiliana na wenzie kwa ujumbe mfupi wa simu, ambao walifika eneo hilo wakiwa na silaha hizo za kisasa.
Tukiwa tunalinda wale ng’ombe, ghafla walikuja vijana wa Kimorani zaidi ya 15 wakiongozwa na Kafuna Kandulu na silaha za kijeshi kama saba, wakaanza kupachika magazini kwenye bunduki zao na kufyatua risasi nyingi hovyo zilizojeruhi baadhi ya watu na mimi,” alisema William.
William ambaye amejeruhiwa kisogoni, shingoni, mkononi kushoto na tumboni ilikokwama risasi, alisema baada ya milio ile ya bunduki, wanakijiji walianza kutoka majumbani wakiwa na silaha za jadi zikiwemo pinde na mishale kisha kukusanyika katika eneo hilo.
Kufuatia hali hiyo, Wamasai hao walianza kuwalenga na kuwapiga risasi sehemu mbalimbali za miili yao, huku wanakijiji wakijibu kwa kuwarushia mishale iliyowasambaratisha wafugaji hao na kuanza kukimbilia porini huku wakiwarushia risasi.
Wakihusisha mgogoro huo na iliyopita, ukiwemo uliosababisha kufungwa barabara eneo la Dihombo, viongozi hao; Malaja na Chikuni kwa nyakati tofauti, walionyesha kusikitishwa na vyombo vya dola kuchelewa kuimarisha ulinzi eneo la tukio hadi kufikia maafa hayo.
Unajua wananchi walifanya kazi nzuri na kubwa sana, lakini wamekosa msaada kutoka vyombo vya dola, kwani baada ya taarifa ya kukamatwa ng’ombe wale, binafsi niliomba msaada wa nguvu ya ulinzi kwa OCD na Mkuu wa Wilaya, lakini mpaka sasa hakuna hata polisi,” alisema Malaja.
Kuhusu hali ya usalama katika vijiji vya kata hiyo, walisema mapigano hayo yamesababisha taharuki kubwa katika vijiji vya Hembeti, Msufini, Kwampepo, Dihombo na Mkindo ambako watu  wameyakimbia makazi yao na kwenda kusikojulikana huku wengine kujihifadhi katika ofisi ya tarafa na kituo cha polisi Mvomero.
Kwa mujibu wa Dk. Mashaka Issa wa hospitali ya Bwagala, hadi jana walikuwa na taarifa ya kifo cha Yusuph Hamadi (30) na juzi walipokelewa majeruhi wanane huku wengine 15 wakipokelewa jana mchana.
Alisema kuwa majeraha waliyonayo ni ya kupigwa risasi na kukatwa na vitu vyenye ncha kali kama mapanga au sime.
Mkuu wa Wilaya hiyo, Anthon Mtaka na Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustn Shilogile hawakupatikana kutoa ufafanuzi wa tukio hilo kutokana na simu zao kutokuwa hewani.
Imeandikwa na Joseph Malembeka, Mvomero

Monday, November 4, 2013

Lowassa afunguka: Adai kuwa vijana watawang'oa madarakani endapo serikali haitatoa ufumbuzi wa matatizo yao



Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa, ametahadharisha kuwa kama tatizo la ukosefu wa ajira kwa vijana halitapatiwa ufumbuzi, itakuwa chanzo cha serikali kupoteza madaraka.

Lowassa ambaye pia ni Mbunge wa Monduli (CCM), alisema hayo jana wakati akichangia mjadala wa Mpango wa Maendeleo wa Taifa wa Mwaka 2014/2015, uliowasilishwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu), Stephen Wasira.

Lowassa alisema serikali inapaswa kuangalia kipaumbele muhimu na kinachowezekana kutekelezwa cha kuanzia na kufuatia kingine.


Alisema kama angekuwa yeye (Lowassa), angeanza na kipengele cha ajira. “Huwezi kuzungumza mipango bila kuzungumza habari ya ajira,” alisema Lowassa.


Alisema serikali inapaswa kukiri kwamba, kuna  Watanzania wengi waliomaliza darasa la saba, kidato cha nne na cha sita, walioko mitaani hawana ajira. Tusipoangalia watakuja kula sahani moja na sisi. Tusipowashughulikia,” alitahadharisha Lowassa.

Alisema iwapo serikali haitokuwa macho juu ya hilo na kulishughulikia, yale yanayotokea katika nchi mbalimbali barani Afrika, yanaweza pia kutokea hapa nchini.

Ingawa Lowassa hakufafanua maana ya kula sahani moja wala kutaja nchi za Afrika ambazo zimesumbuliwa na vijana, Tunisia na Misri ni miongoni mwa nchi zilizokumbwa na vuguvugu la mageuzi kiasi cha kusababisha watawala kuondolewa madarakani.

Vijana kwa maelfu waliingia mitaani katika nchi hizo wakipinga hali mbaya ya uchumi hasa kukosekana kwa ajira na mwishowe serikali zilizokuwa madarakani ziliangushwa.  
 
Lowassa alisema katika mkutano wa Benki ya Dunia (WB) uliofanyika mwaka huu kulizungumzwa habari kuhusu mdororo wa kiuchumi uliolikumba bara la Ulaya.
 
Alisema moja ya nchi zilizokumbwa na tatizo hilo ni Hispania, ambayo alisema katika kujinasua, ilimbana kila mwekezaji aliyekuwa akiingia katika nchi hiyo kwa kumpa sharti la kuwekeza ajira ya vijana.
 
Kwa mujibu wa Lowassa, mkakati huo uliisaidia Hispania, ambayo katika miaka miwili mitatu iliyofuatia ilifanikiwa kujinasua kuondokana na tatizo hilo.
 
“Lazima tuangalie suala la ajira, ni muhimu sana. Mipango mingine haiwezekani bila kutizama suala la ajira,” alisema Lowassa.

Alimpongeza Mkuu wa Mkoa wa Tabora, Fatuma Mwassa, na Mkuu wa Wilaya ya Igunga, mkoani humo, Elibariki Kingu, ambao alisema wameanza kuhangaikia suala la ajira kwa vijana.  Alisema iwapo kila wizara ikiamua kushughulikia suala la ajira kwa vijana linawezekana.
 
“Yule mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya wameamua kuchukuwa vijana waliomaliza Chuo Kikuu, wamewatafutia mashamba, wamewatafutia trekta. Wale vijana wamefanya kazi nzuri sana. Kwa hiyo, inawezekana,” alisema Lowassa.

Kadhalika, alisema mipango mingi ya maendeleo nchini imekuwa haifanikiwi kutokana na serikali kutokuwa na msimamo wa kufanya maamuzi magumu.
 
Badala yake, alisema imekuwa ikiishia kupanga, lakini hakuna utekelezaji na hivyo kuungana na wananchi kulalamikia kukwama kwa mambo.

Alisema anapongeza sana uamuzi wa serikali kuanzisha kitengo maalumu kilicho chini ya Ofisi ya Rais, kijulikanacho kama ‘Presidential Delivery Bureau’ (PDB), kinachosimamia mpango wa Matokeo Makubwa Sasa (BRN) na kusema: “Hongereni sana.”

Hata hivyo, akaitaka serikali kujiuliza maswali kama kitengo hicho kina ‘meno’ ya kufanya maamuzi magumu?
 
 “Tatizo la nchi hii mnazungumza mambo hakuna utekelezaji. Tunazungumza, lakini discipline (nidhamu) ya (nchi ya) Malaysia na hapa (Tanzania) ni tofauti. Hapa kuna uswahili mwingi wa kukaa bila kutekeleza mambo, mnaamua hamtekelezi,” alisema Lowassa.

Alishauri kuwapo na chombo, ambacho kinaweza kufanya maamuzi magumu na yakawa magumu yanayotekelezeka kweli kweli. Alisema tabia ya kujivika joho la kufanya maamuzi ya utekelezaji, lakini bila kufanya, ni kazi bure.

Kwa hiyo, akasema uamuzi wa kuwa na PDB ni mzuri, lakini akasisitiza kuwa usipoangaliwa itakuwa ni sawa kufanya kazi bure, hivyo akashauri ni lazima kuwapo na meno ya kuuma.
 
“Tukikubaliana mambo yafanyike. Haiwezekani katika nchi kila mtu akawa analalamika. Kiongozi analalamika, mwananchi analalamika, haiwezi ikawa ni jamii ya kulalamika lalamika. Awepo mtu mmoja anayefanya maamuzi na anayechukua hatua,” alisema Lowassa.
 
Alisema bila kuchukua hatua, kazi ya serikali na wananchi itabaki kuwa ya kulalamikiana.

Alitoa mfano wa uhasama uliopo baina ya nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), akisema hakuna haja kwa Tanzania kugombana na marais; Paul Kagame (Rwanda), Uhuru Kenyatta (Kenya) na Yoweri Museveni (Uganda) kwa kuamua kushirikiana kiuchumi na Sudan Kusini na kuitenga Tanzania.

Alisema kwani Tanzania inaweza kushirikiana na Mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Goma, ambako alisema ni kuzuri zaidi ya Sudan.
 
 Lowassa alisema inachohitaji Tanzania kufikia hilo, ni kufufua reli ya kati ili kuzalisha kuliko nchi hizo.
 
VIPAUMBELE KATIKA MPANGO WA MAENDELEO
Kuhusu vipaumbele vilivyomo katika Mpango huo, alisema ni vingi na kushauri kwamba, vingechaguliwa vichache vikasimamiwa na kutekelezwa.
 
Alisema kupanga vipaumbele vingi kwa wakati mmoja ni vigumu kutekeleza vyote.
 
ELIMU
Alisema kipaumbele cha pili ambacho alishauri kipewe kipaumbele ni elimu. Lowassa alisema kinachozungumzwa juu ya elimu hakipaswi kupuuzwa na kusema lipo tatizo la msingi katika elimu ya Tanzania, kwani vitu vinavyochukuliwa havitoshelezi.

 
Alisema alitegemea kuwa Kamati ya Bajeti ingepata taarifa ya Waziri Mkuu iliyotolewa juu ya elimu kama ingetambua baadhi ya matatizo, serikali ikaangalia cha kufanya.
 
“Haitoshi kuchukua wanafunzi wengi wanaomaliza Chuo Kikuu wakati akienda sokoni uwezo wake wa kimasomo haupo sokoni” alisema Lowassa.
 
 Alisema hiyo inatokana na wanafunzi wengi wanaomaliza Chuo Kikuu kutokuwa na hakika ya ajira kwa sababu ya kutokuwa na uwezo wa kushindana katika soko.
 
Lowassa alisema kelele zinazopigwa na wananchi juu ya elimu nchini, inafaa ukafanyika mjadala kuangalia tatizo lililopo katika elimu na nini cha uhakika cha kufanya.
 
Alisema vinginevyo serikali isipoangalia, Tanzania itaachwa nyuma na EAC, Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika (SADC) na dunia kwa jumla, badala yake itabaki kuwa mbabaishaji katika soko la elimu.
 
“Tuwasaidie vijana wetu, tubadilishe mfumo wa elimu, tuangalie tunaweza kufanya nini vizuri zaidi,” alisema Lowassa. 
 
AMSIFU WAZIRI MAGUFULI
Alisema kipaumbele cha tatu kwa maoni ni reli ya kati na kwamba, anamsifu sana Waziri wa Ujenzi, Dk. John Magufuli, kwa kazi nzuri ya ujenzi wa barabara aliyoifanya.

 
Lakini akasema barabara hizo zimeanza kuharibika kwa kasi ya hali ya juu sana.  “Tumetoka Singida juzi, barabara imeharibika vibaya sana. Ile ya Shinyanga, imeharibika vibaya sana. Kwa sababu malori yanayokwenda yanayopasa kutembea kwenye treni yanatembea kwenye barabara…Naomba reli ya kati muiangalie kwa haraka sana,” alisema Lowassa.
 
FOLENI DAR, AMSIFU WAZIRI MWAKYEMBE
Akizungumzia tatizo la foleni jijini Dar es Salaam, kwanza alimpongeza Waziri wa Uchukuzi, Dk. Harrison Mwakyembe, kwa kazi nzuri anayoifanya ya kupambana na tatizo hilo.

 
Hata hivyo, alisema jitihada hizo za Waziri Mwakyembe pekee hazitoshi, kwani muda wa saa ambazo wakazi wa Dar es Salaam wanaoupoteza kwenye foleni zikipangwa kwa ajili uzalishaji ni nyingi sana.
 
Kwa hali hiyo, alisema serikali haiwezi kukaa hivi hivi, kwani hiyo ni hatari kwa uchumi wa nchi.
 
“Mtafute njia ya kuangalia tunafanyaje foleni ya Dar es Salaam, sasa si kungoja, it has to be done now (inatakiwa kufanyika sasa),” alisema Lowassa. 
 
MBUNGE AMUUNGA MKONO
Mbunge wa Pangani (CCM), Saleh Pamba, akichangia mjadala huo, alimuunga mkono Lowassa, kwa kusema urasimu uliomo serikalini ni wa kuchukua maamuzi na kusema kwa mwenendo huo kamwe nchi haiwezi kuendelea.  Alisema Malaysia wamefanikiwa na kupiga hatua katika maendeleo kwa sababu kuu moja tu ya kuchukua maamuzi kwa haraka.
 
CHANZO: NIPASHE
 

Mambomseto Copyright © 2011 -- Template created by MAMBOMSETO TEAM -- Powered by MAMBOMSETO

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter