Friday, November 1, 2013

HUKUMU YA MASOGANGE YAPINGWA KWASABABU NI NDOGO NA HAIENDANI NA KOSA ALILOLIFANYA....


MAKAMANDA wa vitengo vya kudhibiti madawa ya kulevya kwa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) wamemaliza kikao chao jana kujadili mustakabali wa uhalifu ikiwemo hukumu iliyotolewa kwa Mtanzania Agness Gerald ‘Masogange’ aliyekamatwa na malighafi haramu aina ya Ephedrine, Julai 5, 2013 nchini Afrika Kusini kwamba ni ndogo.
Taarifa za ndani kutoka Jeshi la Polisi Tanzania zimeeleza kuwa makamanda wa nchi hizo 15 walikutana jijini Arusha kuanzia Jumatatu iliyopita lengo kubwa likiwa kutokubaliana na adhabu zinazotolewa na baadhi ya nchi wanachama kwa wanaokutwa na hatia ya kukamatwa na madawa ya kulevya ‘unga’.

WALICHOJADILI
Kwa mujibu wa chanzo kilicho ndani ambacho kiliomba hifadhi ya jina kwa kuwa si msemaji, makamanda wa nchi hizo walikuwa na kibarua kizito cha kujadili mbinu mbalimbali za kukabiliana na uhalifu pamoja na hukumu inayotolewa kwa watu wanaokutwa na hatia ya kukamatwa na unga.
“Walijadili matukio mengi ya uhalifu likiwemo suala la madawa ya kulevya, wakajadili mbinu za kukomesha biashara hiyo haramu ili waweze kupata suluhisho la kudumu,” kilisema chanzo hicho.

NZOWA
           WATAKA HUKUMU KWA NCHI WANACHAMA IWE MOJA
Ilidaiwa kuwa, malighafi aliyokamatwa nayo Masogange na mwenzake kwa nchi nyingine kifungo chake kinafanana na kile cha mtu aliyekamawa na madawa ya kulevya, lakini kwa Afrika Kusini ni cha chini sana.

Chanzo hicho kilizidi kumwaga data kuwa, miongoni mwa masuala yaliyokuwepo kwenye ajenda ni pamoja na umoja katika suala zima la hukumu hususan kwa watuhumiwa wa madawa ya kulevya kwani kumekuwa hakuna uwiano baina ya nchi moja na nyingine ndani ya Jumuiya hiyo.
“Tumeona ilivyokuwa kwa Masogange, nchi nyingi zimepinga kabisa ile hukumu kwani ilikuwa haifanani na kosa husika. Mtu anatozwa faini ya shilingi milioni nne na laki nane (Sh. milioni 4.8) kitu ambacho hakiingii akilini kabisa, makamanda wengi wameonesha kupinga hukumu ile,” kilisema chanzo hicho.
MASOGANGE AJIFICHA
Wakati makamanda wa nchi hizo wakimaliza kikao chao, habari zenye utata zimesambaa kwamba, Masogange alitua Bongo katikati ya mwezi uliopita lakini anaishi Dar au Mbeya kwao kwa kujificha.
Agness Gerald ‘Masogange’.
Baadhi ya watu, wakiwemo marafiki zake wamekuwa wakisema kwa mkato staa huyo yupo Dar huku wengine wakisema baada ya kutua Dar alikwenda kwao Mbeya kwa sababu hataki kujulikana kuwa amesharudi Bongo.
Mwenyewe anapopatikana kwenye simu na kuulizwa amekuwa akijibu bado yupo Afrika Kusini lakini siku yoyote atatua Dar.

NZOWA ATOA UFAFANUZI
Kamanda wa Kikosi cha Kuzuia na Kupambana na Madawa ya Kulevya Tanzania, Godfrey Nzowa alipoulizwa kwa njia ya simu juzi kuhusu mkutano huo alijibu kuwa yupo safarini kikazi akiwa katika mazingira mazuri atatoa ufafanuzi.
“Nipo safarini kikazi, naomba unitafute siku nyingine nitakupa ufafanuzi mzuri sana,” alisema Kamanda Nzowa ambaye naye ilidaiwa alikuwepo kwenye kikao hicho.

KUMBUKUMBU
Masogange na Mellisa Edward walikamatwa Julai 5, mwaka huu kwenye Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Oliver Tambo uliopo Kempton Park jijini Johannesburg  nchini humo wakidaiwa kuingiza madawa ya kulevya aina ya Crystal Methamphetamine yenye thamani ya shilingi bilioni 6.8.
Hata hivyo, mahakama kuu nchini humo ilidai madawa hayo si ya kulevya bali ni malighafi haramu iitwayo Ephedrine ambapo kwa sheria za Afrika Kusini mtu akipatikana na hatia ya kuyaingiza nchini humo ni kifungo cha miezi 32 jela au faini ya shilingi milioni 4.8 kama alivyohukumiwa Masogange ambayo ni ndogo.

KICHAKA CHA NGONO:MADADAPOA WAKUTWA NA WATEJA WAO,WENGI NI WAKE ZA WATU NA MADENTI.....


UCHAFU unaendelea kufichuliwa! Safari hii Oparesheni Fichua Maovu (OFM) kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Wilaya ya Temeke wamekifyeka kichaka cha ngono maeneo ya Mbagala-Zakhem jijini Dar, Risasi Jumamosi linakupa habari kamili.
Tukio hilo limetokea juzikati usiku wa manane baada ya wakazi wa kitongoji hicho kuchoshwa na tabia za madadapoa hao waliokuwa wakifanya vitendo vichafu karibu na nyumba zao na kutoa taarifa kwa OFM.

Kikosi hicho kiliwasiliana na Kamanda wa Polisi Kanda ya Temeke, Englebert Kiondo na kupewa askari wa Kituo cha Mbagala Kizuiani na kwenda kukifyekelea mbali kichaka hicho.
Kondom zikiwa zimezagaa eneo la tukio.
Kichaka hicho kilikuwa na akina dadapoa wenye umri wa kuanzia miaka 16 hadi 38 ambao walikuwa wakitoa huduma kwa wateja wao kwa shilingi 5,000 kwa raundi moja.
Walionaswa wakiwa katika difenda.
Mara baada ya polisi na timu ya OFM kufika eneo husika waliwakuta akina dadapoa wakiwa wamekaa tayari kwa ajili ya kutoa huduma hiyo.
Pia, kikosi hicho kilimkuta mteja mmoja akiwa anapewa huduma hiyo ndani ya kichaka hicho kilichotapakaa kila aina ya kondom katika kona zote.
Ndani ya kichaka hicho, kulikuwa na sehemu maalum ya kufanyia ngono ambayo ilikuwa imetandikwa boksi chafu huku sehemu ya mlango ikizibwa na gunia aina ya ‘salfeti’.
OFM ilibaini kwamba kabla ya dadapoa na mteja wake kuingia ndani ya kichaka hicho, kulikuwa na malipo ya fedha kwa  mmiliki wa kichaka hicho ambaye alifahamika kwa jina maarufu la Babu ambaye hata hivyo, alifanikiwa kukimbia baada ya kuona madadapoa hao wakikamatwa.
Pamoja na hayo, oparesheni hiyo ilimnasa kahaba mdogo kuliko wote aliyejitambulisha kwa jina moja la Sarah (16) ambaye alidai kuwa ni yatima kutoka Mkoa wa Mtwara na alijichanganya katika biashara hiyo haramu kwa ajili ya kutafuta kipato kwa kuwa hana ndugu wa kumsaidia.
Oparesheni hiyo pia ilimnasa mama mtu mzima aliyejitambulisha kwa jina moja la Joyce (38).

Pamoja na mama huyo kuhojiwa sababu ya kuingia katika biashara hiyo aligoma kuzungumzia kutokana na aibu.
Watuhumiwa wengine  pia waligoma kutoa ushirikiano kwa OFM kwa kuhofia kuvunja ndoa zao kwa kuwa ilibainika kwamba wengi wao ni wake za watu.

Madadapoa hao pamoja na mteja aliyenaswa walipelekwa katika Kituo cha Polisi cha Kizuiani na kufunguliwa jalada la kesi namba MBG/RB/11343/13 KUFANYA VITENDO VYA UMALAYA, kabla ya kupandishwa kizimbani kwa hatua zaidi za kisheria.

LULU AANGUA KICHEKO CHA NGUVU WAKATI MISA YA MSIBA IKIENDELEA....

Lulu (wa pili kushoto) akiangua kicheko na shosti wake wakati misa ya msiba ikiendelea.
KATIKA hali isiyotarajiwa, staa wa sinema za Kibongo, Elizabeth Michael ‘Lulu’ amenaswa na kamera yetu akiangua kicheko cha nguvu huku misa ya msiba ikiendelea.
Tukio hilo lililowaacha midomo wazi waombolezaji lilitokea Jumanne iliyopita nyumbani kwa marehemu baba wa mwigizaji Wema Sepetu ‘Madam’, Isaac Abraham maeneo ya Sinza-Mori, jijini Dar wakati Lulu alipokuwa amekwenda kumfariji mwigizaji mwenzake huyo.

Lulu ambaye alikuwa amevalia sare maalumu waliyovaa watu wa karibu na familia ya marehemu, alinaswa akiwa amejisahau kabisa kama yupo msibani na kuanza kupiga stori na dada mmoja ambaye jina lake halikuweza kupatikana mara moja.
...Wakizidi kupiga stori na kufurahi wakati wa ibada.
“Mh! Sasa mwenzetu pale amepitiliza haiwezekani ajisahau kiasi kile wakati hapa ni msibani. Atachekaje kiasi kile, hii ni aibu jamani bora hata wangeenda kuchekea pembeni,” alisikika mmoja wa waombolezaji.
Baada ya kugundua papararazi wetu anawafotoa picha, ghafla wawili hao walihamaki na kuacha kucheka huku wakijiziba usoni wasiweze kunaswa sura zao kiurahisi na kamera.
Katikati ya wiki hii, Lulu aliripotiwa kuwa amevurumusha matusi kwa mapaparazi katika msiba huohuo hali ambayo inawafanya mashabiki wahoji kulikoni?

DIAMOND NUSURA AWEKWE CHINI YA USALAMA WA TAIFA KWA KUVURUGA MSAFARA WA RAIS...

STAA wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’, Alhamisi iliyopita alijikuta akiutibua msafara wa Rais wa Zanzibar, Dk. Mohamed Shein kufuatia kuondoka kwenye msiba wakati ilitangazwa kiongozi huyo ndiye aliyetakiwa kuanza kuondoka.
Ishu hiyo iliyotafsiriwa kama jeuri ya staa huyo ilitokea Mbuzini Mjini Magharibi, Zanzibar baada ya kumalizika kwa mazishi ya baba wa Wema Sepetu, aliyewahi kuwa Balozi wa Tanzania Urusi, Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo na Waziri wa Elimu wa zamani katika Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, marehemu Isaac Abraham Sepetu.

DIAMOND AINGIA
Awali, wakati waombolezaji wamekaa wakiusubiri mwili wa marehemu ufike, ghafla Diamond aliibuka akisindikizwa na kundi la wapambe mpaka alipokaa.
AWEKWA MSTARI WA MBELE
Diamond alipofika aliwekwa mstari wa mbele ambako walikaa ndugu wa karibu na watoto wote wa marehemu.

MC ATANGAZA ITIFAKI YA SERIKALI
Mwili ulipowasili, ratiba ya mazishi ikatangazwa na MC ambapo alitaja utaratibu wa mazishi mpaka watu watakaotakiwa kuweka mashada ya maua kaburini, akiwemo Rais Shein.
Baada ya mazishi, Mwongoza Shughuli ambaye jina halikujulikana aliwaomba watu wote wazingatie itifaki ya usalama wa taifa kwamba ni lazima viongozi wote wa serikali waondoke ndipo waombolezaji wengine watawanyike.
“Jamani naomba sana itifaki izingatiwe, asiondoke mtu yeyote kabla ya viongozi wetu wa serikali, akiwemo Rais Shein hawajaondoka,” alisema MC huyo.

DIAMOND APUUZA, ANYANYUKA
Baada ya MC huyo kutoa mwongozo, watu wote walitulia wakisubiri kiongozi wa kwanza kuondoka ambaye alikuwa ni Rais Shein kama itifaki ilivyotaka.
Lakini kabla Rais Shein hajaanza kusimama, Diamond alinyanyuka na kuzua kasheshe kwa sababu baadhi ya watu, hasa wa umri wake walianza kumkimbilia huku wakikanyagana na kusababisha hali ya taharuki.

MC AWATULIZA WATU
Baada ya watu kuanza kukimbizana hovyo muongozaji wa msiba huo aliwaomba watulie na kusema kuwa wasiogope ila kuna staa ambaye anapita ndiyo maana watu wamemkimbilia.
“Naomba utulivu huyo ni staa f’lani kapita huko ndiyo maana watu wanamkimbilia hivyo tulieni kwanza viongozi wetu waondoke,” alisema.

USALAMA WA TAIFA NUSURA WAMKAMATE
Baada ya kuona watu wakikimbia hovyo baadhi ya maofisa wa usalama wa taifa walitaka kumkamata msanii huyo wakisema alisimama kwa makusudi licha ya kusikia tangazo la kiitifaki.

WATU WAMSHANGAA DIAMOMD
Baadhi ya watu waliohudhuria msiba huo walionekana kushangazwa na kitendo cha Diamond na kusema kuwa ni vyema angesubiri viongozi wote waondoke ndipo na yeye atimke lakini kufanya vile si sahihi.
“Huyu Diamond kwani ana nini? Nakumbuka kwenye msiba wa Kanumba kule Dar pia aliingia kipindi ambacho ilitangazwa kuna kiongozi anakwenda, utaratibu ukatibuka, watu wakawa wanamshangilia yeye,” alisema mtu mmoja aliyetoka Dar kwenda Zanzibar kumzika mzee Sepetu.

MWANAMKE ANUSURIKA KUUAWA BAADA YA KUKUTWA UCHI HUKU AKIWA AMESHIKA KOPO LENYE MAVI NA DAWA HUKO BUNDA...

(Picha  ya  Maktaba.)

JESHI la Polisi wilayani Bunda, jana lililazimika kutumia mabomu ya machozi kuwatawanya wananchi wenye hasira kali waliotaka kumuua mwanamke mmoja mkazi wa mtaa wa Cha Nyerere katika mamalaka ya mji mdogo wa Bunda.
 
Mwenyekiti wa mtaa huo, Maxmilian Bwire, alisema kuwa tukio hilo lilitokea saa 10 usiku nyumbani kwa mwanamke huyo, Sarafina Nyamboko, maarufu kama mama Nyamboko.

Alisema kuwa siku ya tukio mama huyo alikutwa na mpangaji wake, Robert Msilimu, akiwa uchi wa mnyama na kopo tupu la amboni lita tano, lililodaiwa kuwa na dawa ambayo alikuwa ameimwaga katika kila mlango wa wapangaji wake.
 
“Baada ya kumhoji alisema alikuwa anawamwagia dawa ya baraka wapangaji wake kwani kila tarehe moja huwa anafanya hivyo ili waweze kupata baraka kwa Mwenyezi Mungu.
 
“Dawa hiyo inaonekana ilikuwa imechanganyikana na kinyesi maana mji mzima ulikuwa unanuka kinyesi,” alisema mpangaji huyo ambaye alimkuta mwenyenyumba wake akifanya mchezo huo.
 
Alifafanua kuwa kitendo hicho kilimshtua sana ndipo alipowaamsha wapangaji wenzake ambao waliamua kupiga yowe na majirani walifika na silaha mbalimbali za jadi na kuanza kumshambulia.
 
Alisema kwa kushirikiana na mwenyekiti wa mtaa huo, walipiga simu polisi ambao walikuja na baada ya kukuta hali ni mbaya, waliamua kutumia mabomu ya machozi ili kuwatawanya wananchi hao na kumchukua mama huyo kwenda naye kituo cha polisi.
 
Hata hivyo, baadhi ya majirani walidai kuwa hii ni mara ya tatu sasa kwa mama huyo kukutwa anafanya mchezo huo na kwamba hata kwenye mikutano ya hadhara ya mtaa huo, ameshaonywa mara kwa mara lakini alikuwa hajaacha.
 
Polisi walisema kuwa wanaendelea kumhoji kwa kina kuhusu kitendo hicho cha kukutwa uchi na pia kufahamu ukweli wa dawa hiyo aliyokutwa nayo.
 
Kama ikithibitika kuwa kuna kosa ndani yake watamfikisha kwenye mkondo wa sheria.

UFUSKA NDANI YA BONGO MOVIE....WASANII HULIPWA NA KUHONGWA MAGARI ILI KUTOA "PENZI" BILA KINGA...


KINACHOONEKANA kwa sasa Bongo ni ugumu wa serikali kupambana na vita dhidi ya maambukizi ya Virusi vya Ukimwi baada ya jamii kushindwa kubadilika na kuona ugonjwa huo ni wa kawaida kama ilivyo kukohoa au kichwa kugonga.Hilo limedhihirika baada ya juzi chanzo chetu cha habari kupasha kwamba, baadhi ya wafanyabiashara na wabunge wameingia ‘kazi’ ya kuwanasa mastaa wa kike Bongo, hasa waigizaji wa filamu. 
Kwa mujibu wa chanzo hicho, wafanyabiashara maarufu wa jijini Dar na baadhi ya waheshimiwa wabunge wamekuwa wakiwaibukia mastaa wanapokuwa kambini wakirekodi filamu na kuwahonga fedha nyingi sanjari na kuwanunulia magari ya kifahari ya kutembelea.
Inadaiwa wanachofanya baadhi ya mastaa, hasa wakiwa kambini, hupiga picha chafu wakiamini zina mvuto na kuzitundika BBM kwenye simu zao ambapo wafanyabiashara na wabunge hao wanapoziona huweweseka na kuanza msako wa kuwapata.
Chanzo kilisema: “Zamani mapedeshee ndiyo walikuwa wanaongoza kwa kuwachukua mastaa wa kike kwa kutumia picha za mitandaoni na kwenye magazeti, siku hizi mastaa wenyewe wamewashtukia, hawawataki mapedeshee, wanasema fedha zao ni za msimu.

“Siku hizi mastaa wakiwa kambini hupiga picha za hasarahasara na kuzitupia BBM, wafanyabiashara na wabunge wakiziona wanakimbilia kupanga foleni kwenye mahoteli ambayo mastaa hao wamepiga kambi.”

Aidha, chanzo kikasema kuwa baadhi ya wafanyabiashara huhonga kuanzia shilingi 1,000,000 hadi 5,000,000 kama staa ana jina kubwa.

“Kama staa ana jina kubwa, anaweza kuhongwa kuanzia milioni moja hadi tano, kama ni supastaa kama Wema, Wolper, Odama, Rose Ndauka hawa wanaweza kuhongwa hata magari ya kifahari,”kilisema chanzo hicho.


Chanzo kikasema kuwa, mbaya zaidi wanaume hao wamekuwa wakigoma kufanya mapenzi kwa kutumia kinga (kondom) kwa madai kwamba, hawawezi kuhonga pesa nyingi halafu kitandani wakatumia kondom kwani wanakosa raha.
“Kinachouma zaidi ni kwamba, hao wanaume wakiwachukua mastaa hadi chumbani wanakataa kutumia kondom, madai yao pesa wanazohonga ni ndefu (nyingi) kwa hiyo ni afadhali wafaidi, wanasahau kwamba Ukimwi upo.

“Kwa sababu ya tamaa ya pesa, dada zetu (mastaa) wanashindwa kuwa na msimamo wa kutumia kondom. Anaweza kukataa sana, lakini mheshimiwa anaahidi kumnunulia gari, hapo ndipo masharti yanalegezwa,”kilisema chanzo.


Chanzo kikasema kumekuwa na vilio na kusaga meno kwa baadhi ya mastaa kwani wanaponunuliwa magari, kadi zinakaa kwa wanaume hao, baadaye wanawanyang’anya.

“Mbaya zaidi, wapo mastaa waliwahi kushawishika na kutoa penzi bila kinga kwa ahadi ya kununuliwa gari, waliponunuliwa hawakupewa kadi ya kumiliki, baadaye wakanyang’anywa,” chanzo kilitoboa.

Baadhi ya mastaa waliozungumza na paparazi wetu walikiri kuwepo kwa wanaume wenye tabia hiyo, lakini kila mmoja akasema yeye haijamtokea.
Wolper:
 “Ni kweli, wapo wanaume wanabembeleza sana kutotumia kondom na kuahidi fedha au gari, lakini kama staa anakubaliana na ombi hilo ni kujiangamiza, Ukimwi unaua. Ila mimi sijawahi kukutana na mwanume wa hivyo, kwanza nilishasema ndani ya gari natembea na kondom.”

Jack wa Chuz: “Wewee, uamuzi wa kufanya hivyo ni wa mtu mwenyewe na umri wangu huu nikubali kufanya mapenzi bila kinga kwa sababu ya gari? Kwani gari kitu gani bwana.”

Nisha: “Mh! Nimewahi kusikia kuna wasanii waliingia kwenye mtego huo na sasa wanajuta maana hawana uhakika na afya zao, kwenda kupima wanaogopa, magari walishanyang’anywa, mimi aku!”

Flora Mvungi“Mimi siwezi kusema kitu maana nina wangu, kama ni gari au pesa ananipa yeye, pole yao ambao hawajajipanga hadi leo.”

Aidha, chanzo kilisema kuwa, maeneo hatari ya kufanyika kwa michezo hiyo ni hoteli kubwa ambazo wasanii hupiga kambi kwa ajili ya kurekodi filamu. 


src utamu specially

HII NI LAANA....!!! CHEKI WAKINA DADA WAKINYONYANA "DENDA" MBELE ZA WATU BILA AIBU...


Hizi picha tumezipata facebook wakiwa wamepost kwenye kurasa zao, ina maana hii hali ipo kwa dada zetu, jamani wanaume wameisha au ni nini...???
These are the kind of pictures  you see our beautiful African ladies posting on their wall...
Well if they are able to share it on their wall that means they don't mind the whole world seeing them, right? Behold.


<<BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI>> 
 

Mambomseto Copyright © 2011 -- Template created by MAMBOMSETO TEAM -- Powered by MAMBOMSETO

Like Us On Facebook
Follow Us on Twitter